Mamba mkubwa auawa hotelini jijini Mwanza

Yaani sisi Waswahili suluhisho letu la kwanza kwa kila tatizo siku zote ni kuua tu.

Sidhani kama kulikuwa na juhudi zozote za kumkamata na kumrudisha alipotoka, sisi ni kuua tu.

Mwizi tukimkamata na kumdhibiti bado tunaishia kumuuwa, hata kama wangesaidia taarifa muhimu za kuwakamata wenzake.
Angekwapua mkono wako usingetetea huu uozo.
 
Kwa habari niliyopata hivi punde :

Inasemekana Mamba ameuawa pembezoni mwa hoteli ya Tilapia jijini Mwanza leo mchana.

=====

Mamba huyu ameuawa kwa kupigwa risasa na Maliasili baada ya kuibuka katika eneo la kivuko cha kwenda Hifadhi ya Saanane pale Capri point wilayani Nyamagana mkoani Mwanza na hivyo kuleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

8b56da22a9283cb6ac3f312dcf9bd0dc.jpg


7e33e2b4ad30a503ed2c18b9889f9a90.jpg


10c85ba24285dca6a0bb38f84fc63b66.jpg
Tumechoka!wapigwe tu
 
Yaani sisi Waswahili suluhisho letu la kwanza kwa kila tatizo siku zote ni kuua tu.

Sidhani kama kulikuwa na juhudi zozote za kumkamata na kumrudisha alipotoka, sisi ni kuua tu.

Mwizi tukimkamata na kumdhibiti bado tunaishia kumuuwa, hata kama wangesaidia taarifa muhimu za kuwakamata wenzake.
unamjua mamba au unadhani huyo ni kenge angeua mtu ungesema ni uzembe tena
 
Mbona USA wanaingia mpaka swimming pool lakini wanawakamata na kuwapeleka sehemu za mbali?
Kwanini wamuuwe?
Hebu maliasili watoe mafunzo kwa wananchi kwamba pindi wanapoona mnyama wapigiwe na kuja kumkamata
Kumshika Mamba ni rahisi sana
Inasikitisha kwa kweli
mamba wa kizungu hawana njaa hawa wa huku vyuma vyao vimekaza wana viburi kama watu wao
 
nakumbuka kulikuwa na el nino 98, kijiji chetu kimezungukwa na mito na mabwawa na sisi tulikuwa tumejenga kiasi cha mita mia tano kutoka mtoni, tulikuwa na eneo kubwa ambalo mzee alikuwa amejenga kwa mtindo wa motel maana ni pembezoni mwa barabara kubwa, sasa mafuriko yalipo ingia ilikuwa ni alfajir flani, tukaja okolewa na mitumbwi, nyumba zote zilimezwa na maji, na wakati maji yalipoondoka yote na kubaki madibwi, ndipo nasi tuliporudi, sasa wakati tukisafisha majengo ndipo katika jengo moja ambalo baadae lilikuja kuwa kama ukumbi, tulimkuta mamba mkubwa mno kapozi hana wasi, nakumbuka tulimtoa na trekta...kuna watu wakaenda kumla
Hahaha.. Aisee.. Mulimvuta na trekta... Hatari sana!
 
Ukweli ni kwamba hao maliasili waliomwua wanatakiwa kufikiri mara ya pili. Kumuua hakuzuii wengine kuja Mwanza. Tena si ajabu ndio watafurika sasa. Huenda makao yao wamevamiwa na uvuvi haram hivyo wakaanza kutafuta mahali salama.
Zoezi ni kuwakamata na kuwarudisha walikotokea na kupatengenezea mazingara salama wafurahie kukaa huko. Jiulize swali, wadhani huyo mamba mkubwa hivyo ni wa umri gani?? Sasa kwa nini hujiulizi kuwa mpaka awe mkubwa hivyo, mbona hakuwahi kufika hapo Mwanza mjini?? Kuna sababu hivyo askari aliyemuua afunguliwe mashitaka
 
Back
Top Bottom