Songwe: Bibi wa miaka 70 auawa, akatwa kichwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
MKAZI wa kijiji cha Itumba, Ileje mkoani Songwe, Namanga Mwambene (70), ameuawa kikatili kwa kukatwa kichwa na watu wasiojulikana, huku wauaji wakiondoka nacho, hivyo kusababisha kuzikwa bila kichwa.

Taarifa ya kifo hicho imezua taharuki kwa wakazi wa wilaya na mkoa huo kutokana na mzingira ya mauaji ya bibi huyo huku simanzi na majonzi vikitawala kila kona.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Itumba, Pitros Mshani, alisema wauaji hao walitenda unyama huo mapema wiki hii kwa kumkata kichwa bibi huyo ambaye alikuwa mjane.

Alisema tukio hilo lilitokea katika Mlima Simu, ambako bibi huyo alikwenda kuokota kuni na baada ya kusikia taarifa hizo, walifika eneo hilo na kumkuta bibi huyo akiwa amekufa huku kichwa chake kikiwa kimechukuliwa.

Alisema baada ya kushuhudia tukio hilo, waliliarifu Jeshi la Polisi wilayani humo, ambao walifika na kufanya uchunguzi wa awali na kuubeba mwili huo hadi hospitali ya wilaya ambako ulitunzwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na siku iliyofuata familia iliuchukua na kuuzika.

Kutokana na tukio hilo, kumeibuka mambo mengi yasiyo na ushahidi wa kina na kwamba wamepanga kuitisha mkutano wa kijiji ili kulizungumzia suala hilo ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Mshani alisema kumekuwapo na taarifa za waganga wa kienyeji wanaojiita ‘Rambaramba’, waliovamia wilaya za Ileje na Mbozi wakiendesha ramli chonganishi.

Waganga hao wanadaiwa kuwa chanzo na kwamba walifika kijijini hapo kwa kupelekwa na watu licha ya serikali ya kitongoji na kijiji kukataa na baada ya siku kadhaa limetokea tukio la kuuawa kwa bibi huyo.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buswesi, ambako bibi huyo alikuwa mkazi wake, Yasinta Mshani, amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na wananchi kumtuhumu kwa sababu ya kukithiri kwa matukio hayo.

Akitangaza uamuzi huo, Yasinta alisema amechoka kutuhumiwa kwa mambo mbalimbali, hivyo ameona ni vyema aachie ngazi ili aishi kwa amani.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude, alikiri kutokea kwa tukio hilo la bibi kuuawa huku akisema chanzo kikubwa ni imani za kishirikina kuwa kichwa kinaleta utajiri baada ya wauaji hao kupigiwa ramri chonganishi.

Mkude alisema taarifa za bibi huyo kuuawa zilipatikana baada ya siku nne kupita na kwamba matukio kama hayo yalikuwa yakijitokeza miaka ya nyuma na mwaka 2016 yalikuwa mengi zaidi na mwaka jana lilitokea moja na sasa limetokea tena.

Alisema kutokana na hali hiyo, wamepiga marufuku kikundi cha Rambaramba ambacho kimekuwa kikipiga ramri chonganishi na kujipatia fedha kwa watu wanaoamini kuwa wamelogwa kitu ambacho si kweli.

Mkude ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo, alisema wanaendelea na uchunguzi na kwamba kutokana na kuibuka kundi hilo, vijana 13 ambao walipewa adhabu mbalimbali na mahakama, ikiwemo ya kupigwa viboko, baada ya kubainika wako kwenye kikundi hicho, wamekamatwa.

“'Hivi ni kweli mtu mwenye akili timamu unaambiwa na mganga wa kienyeji kuwa kichwa cha mtu kinaleta utajiri na wewe unaenda kuua mtu na kuchukua kichwa kupeleka kwa mganga kweli? Hii si sawa kabisa. Kamati ya ulinzi na usalama haitalifumbia macho suala hilo, tutawashughulikia,” alisema Mkude.

Chanzo: Nipashe
 
Hawa ndiyo Wanyiha. Mwanzo walikuwa wanachuna ngozi za binadamu pamoja na kuvizia wenye vipara ili wachukue ngozi za kipara. Sasa wamehamia kwa wabibi. Masikini sijui kwa Bibi wanataka kuchukua nn?
 
Japo ulikuwa umekula chumvi nyingi ila tulikuwa bado tunakuitaji.

Mungu akuweke unapostahili bibi.
 
Hawa ndiyo Wanyiha. Mwanzo walikuwa wanachuna ngozi za binadamu pamoja na kuvizia wenye vipara ili wachukue ngozi za kipara. Sasa wamehamia kwa wabibi. Masikini sijui kwa Bibi wanataka kuchukua nn?
Ileje ni wandali mkuu,wanyiha wako mbozi
 
Hao Rambaramba kuna mkono wa watu wa serikali hasa mkoa wa mbeya na songwe,kwani tokea 2017 wamezunguka vijiji vyote vya wilaya ya rungwe wakiwabambikia raia uchawi na kujichumia pesa ya bure
Hao waganga wanakuja nyumbani kwako wanapekuwa ndani au shambani kwako na wanawatangazia wananchi kuwa wew ni mchawi hivyo ili watoe uchawi huo ni lazima ulipe ng'ombe mmoja au mbuzi na kuku kadhaaa ndani ya wiki moja.Baada ya kutoa hiyo faini wanatoa uchawi eti na kuenda kutungua maisha mjini tukuyu.
Kwa sasa wapo wilayani mbozi wakizunguka vijiji vya jirani na mji wa mlowo,Matajiri wa mlowo walichanga pesa na kuwapa hao Ramambaramba ili wasije mlowo kutoa misukule na vichwa vya watu madukani mwao.SERIKALI PIGA MARUFUKU WAHUNI HAO
 
Watu wengine bwana"... hata mchawi ana nafuu"....binaadamu unaweza vipi kuwa na roho mbaya kiasi hicho".....
 
Back
Top Bottom