Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mamba anayesadikiwa kula zaidi ya watu wanane na kuendelea kutishia maisha ya binadamu na mifugo kandokando ya Ziwa Victoria katika Kata ya Mkuyuni jijini Mwanza kwa muda mrefu. Hatimaye ameuawa baada ya kunaswa na ndoano iliyotegwa na wananchi kwa siku tatu mfululizo
Mamba huyo ameokotwa na wavuvi hii leo majira ya Alfajiri akiwa amekufa huku akielea juu ya maji katika mwalo la Butimba uliopo mtaa wa Kang'ata kata ya Mkuyuni jijini Mwanza
Kunaswa na kuuawa kwa mamba huyo kumeibua furaha kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa miaka mitatu iliyopita walilazimika kuchukua tahadhari kila wanapofanya shughuli zao kwenye mwalo huo
Katibu wa Kitengo cha Kudhibiti na kuzuia Uvuvi Haramu na Utunzaji wa Mazingira ya Ziwa Victoria (BMU), Robert Charles alisema mamba huyo alinaswa baada ya kuwekewa mtego wa ndoano eneo la Butimba
Mamba huyo ambaye hakujulikana kama ni dume au jike, anakisiwa kuwa na urefu wa futi 18, sawa na mita tano na nusu
Mwenyekiti wa BMU kata ya Mkuyuni, Lornard Mpemba amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mamba huyo alikuwa akifika eneo hilo akitokea eneo la Saanane, umbali wa kilometa mbili kutoka eneo mamba alikouliwa.
Chanzo : ITV channel