Mama wa Kambo

Mama wa Kambo

Asante kwa hii post,nina watoto pia nina mtoto nipo na mama wa kambo,nilihisi sasa napata uhakika,nachukua hatua
 
Mkuu hivi ile hali ya uoga inakuaje sijui..
Maana uwezi funguka unahisi ukimwambia mzee,
Yeye atamface maza moja kwa moja na hapo watagombana alafu badae baba akiwa kazini show inarudi kwako.

Nakumbuka kuna kipindi mama mzazi alikuja nisalimia. Sasa kama unavyojua imefika asbhi nikasahau kumsalimia yule mama wa kambo..

Akaniambia wewe unisalimii kwakuwa upo na mama yako eeeeh haya tutaonana..

Na kweli tulionana mkuu hi siku ndo nilishikwa korodani nakubamizwa hovyo hovyo mbele ya wadogo zangu na hapa ilikua mda wa kula...

Me mpaka leo nina ule uwoga hata wa kupanda baskeli nahisi kama takalia korodani..
Jamni maumivu ya korodani yaacheni 🙌🙌🙌🙌🙌
Mwanamke muuaji huyo....
 
Daaah mpaka nimehisi huruma..
Mambo ni mengi sana nakumbuka hata mimi niliwahi toroka nyumba kisa mama alitishia kuniua..

Ilikua hivi siku hiyo mama alimdaka mwanae ambaye tulikua tunasoma shule moja , akamleta shule.

Kufika shule yule mama akawa anawambia walimu kuwa mimi namfundisha mwanae tabia mbaya.

Walimu wakatuma wanafunzi waje nitafuta. Mimi kuona ule msala nikakimbia hapo mama akatuma watu kwamba akinidaka nitakiona..

Mkuu nilikuambia kusikojulikana mpaka inafika jioni nilikua nipo mazingira mbali na nyumbani. Hiyo ilikua forest ya zamani wanapaita kwa mabula maeneo ya mahakamani kule.

Usiku ukafika sijala cha maana hapo nikalala tu nje. Plass bardi la mbeya lile nipo na nguo za shule tu.
Hapo yanakuja majibwa yanabweka na kuondoka

Just imagine kama ingekua ni mwezi wa wapiga nondo sijui ingekuaje au wachuna ngozi..

Inafika asbhi nikasema hapa sirudi nyumbani naenda moja kwa moja kwa bibi. Huko kwa bibi ni iyunga ambako anakaa bibi mlezi wa baba yangu.

Nilitoka forest mpaka iyunga hiyo napita ndani kwa ndani kuanzia kadeghe, meta, simike nzovwe.. nashuka mtoni pale kwa shitindi mpaka naikuta iyunga..

Nilikua hoi sijiwezi kuna mda walikuta nimelala mtoni wakaniamsha ili nitoke maana mda ulikua umekwenda...

Nafika kwa bibi namueleza kuwa naogopa kurudi nyumbani mama atanichapa .
Wakiniulizwa kama nilikua nateswa mimi nilikua nakataa... Sijui kwanini sikusema.

Wakamuita baba, baba amefika alikua mkarimu sana pale akawa ananiambia "" mwanangu wewe ndo ulinishauri nioe shida nn"" hapo sikua na neno.

Baada ya hapo akaenda moja kwa moja na mimi polis post pale meta hospital
Kufika pale nikatishiwa tishiwa nahisi alilipoti kama nimepotea..

Kwa haraka nikajua baba tushamalizana.
Aiseee tunafika karibia na hom alinishusha mabao hayo..

Baba ana mikono migumu sijapata ona kwanza vile vidole sijui vilikua vyake au bandia.. alinizabua mpaka tunaingia ndani nilikua sielewi..

Kesho yake asbhi naambiwa kwenda madrassa kufika madrasa ndo ikawa ishu nyingine maana yule ostadhi kama aliambiwa na baba kama mimi nilitoroka.

Madrassa ilikua pale msikiti wa mahakama kuu..
Kuna msikiti kwa chini hapa kama ushafika mahakama mbele kidog ya mahakama kuna ofisi ya mkuu wa polisi hapo kwa chini ndo kuna msikiti.

Yule ostadh alinichapa mkononi sio kwenye kiganja ila ni maeneo ya saa inapovaliwa..

Alinichapa sana sana sana mpaka miaka mwaka wa pili mama anakuja anakuta alama alitaka aende kumshtaki yule shekhe
Daah hapana kwakweli
 
Pole sana brother.
We have the same case ..little bit different. But pole sana. Na Mungu akupe hitaji LAKO.
 
Tatizo hapo ni huyo aliyekua singo mama ambaye aliolewa na mzee.
Kwanza nikuhakikishie singo mama akiolewa yule mzazi mwenzie akitaka uroda anapewa bila masharti, hii nakuhakikishia na hapewi hata Mia sana sana eye ndio atampa pesa mzazi mwenzie.
Speaking from experience.
 
Back
Top Bottom