Poor Brain
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 27,402
- 54,846
- Thread starter
- #41
AgainSingle maza tena
AgainSingle maza tena
Pole sana mkuu, kuna wazazi wengu huwanyima watoto wao malezi ambayo ni haki yao na huleta mapenzi kati ya mtoto na babaMkuu afadhali wewe ulikua upo karibu na watoto wako..
Mzee wangu alikua hana habari na mimi..
Yeye akishakamilisha madaftari na peni hapo kuonana tena mpaka mwakani naingia darasa lingine.
Niseme kuwa baba angu alikua hazingatii kitu mpaka kuna kipindi nikawa nawaza au bana aliwekewa limbwata na yule MAMA
Anafunga 40 yupo nyumban Kwa baba na mama kazalisha watoto huko kawatelekeza huyo unamsemaje?
Usiwe Mbishi! Hata sisi tunao ila kulea mtoto ambaye analelewa na mama wa kambo ni mtihani mkubwa hususan wa kiume akiwa mdogo. Atanyanyasika tu. Mtoto anatakiwa alelewe na mama yake mzazi, kinyume na hapo ni msala kwa baba. Inabidi iwe FBI maana mtoto anaweza akawa ana tabia mbaya kweli au mama wa kambo anamuonea!Mwanaume akizaa then akashindwa kulea mwaanwe, huyo ni mwanaume mpumbavu.
Mwanaume akio na kisha mwanamkw wake akanyanyasa mwana alie mkuta kabla hajawa alafu mwanaume asitambue.... huyo ni baba mpumbavu.
Yaani....
Mwanaume unawezaje kuzaa alafu mwanao aka kelelewe na mwanaume mwingine 🤔🤔
Duh, ulikuwa jehanam! Na baba naye alikuwa ndezi! Sasa hivi umeshawasamehe?Let share something iwe kama kumbu kumbu hapo baadae (4/6/2025 Wed 3:26)... Malezi ya mama wa kambo
Nimezaliwa mkoani dsm Kizuiani hospital miaka ya 90 mwoshoni. Baada ya wazazi kutengana nikachukuliwa na baba kwenda mkoani, ambako huku baba alikua bachelor yaani hakua na mke hivo kazi ya kunilea ilikua jukumh lake japo sikua mdogo kiasi hicho maana nilikua la kwanza.
Nikisoma shule ya msingi inyala pale iyunga. Nilianza darasa la kwanza mpaka la pili baba akahama ile sehemu.
Na hapo nikaona.mbona baba kama anasumbuka sana maana kila anapirudi kazini anakua na kazi zaidi ya moja, atapika atafanya usafi na bado kuna kuniandaa mimi na shule.
Nilijikuta namuonea huruma na kumshauri baba aoe, bila kujua kumbe ndio najitengenezea moto ambao ulikuja kuniumiza badae.
Basi siku zikasogea ikapita miaka kama mitatu hivi na hapo tayari nilikua nipo darasa la 4.
Baba rasmi akaoa mwanamke kutokea kiwira.
Yule mama alikua mnyakyusa pure an baba yake mnyaki na mama yake mnyaki.
Mda huo wanaowana wote walikua na mtoto mmoja mmoja baba ana mimi na mama ana mdogo angu wa kike ambaye umri tupo sawa.
Maisha yalianza kubadirika kwani sheria zilikua very complicated sikutegemea kama yule mama angebadilika.kiasi kile hata week haikupita nikaanza kuona maisha magumu.
Mama alikua mkari, siwezi kujipendelea hata mi pia nilikua nina dharau hi ni mpaka sasa.
Mama alianza kuwa hatari kiasi ambacho kwangu shule ikawa ngumu.
Nilichanganyikiwa nikawa natoroka shule, sikuwahi kupenda tena kusoma kwani nyumbani niliona.mtiti na hata shule mtiti pia.
Mama huyu alikua akunyimi chakula,
Mama huyu alikua anajua kupiga alikua anapiga kiasi ambacho nilikuwa navuja damu.
Kisa.... Kuna siku tupo chumbani mimi, mama yule mtoto wake wa kwanza na mdogo wetu mdogo ambaye ni mtto wa kwanza na baba yangu.
Hiyo siku tulikua nae chumbani tunapiga story, baada ya kuongea akanituma nikaangalie chakula jikoni (wali) kama maji yashakauka.
Nafika jikoni nikafanya kama alivyonituma ila cha ajabu nilikuta mafuta yamemwagika chini.
Kuchunguza mafuta yanatokea wapi,
Nilikuta ni kabatini ambako yalikua yanaanguka tone kwa tone.
Yale mafuta yalikua hayajafungwa vizuri lakini pia lile dumu liliwekwa kwa ubavu ubavu kwa kuwa kabati lilikua dogo hivo kwa kusimama ilikua ngumu.
Mi nilitoka moja kwa moja na kumuita yule mwanae tukaenda jikoni. Baada ya kuona ule mtiti tuka shauriana tufute yale mafuta.
Basi ikafanyika hiyo kazi kwa dakika kama tano hvi mambo yakawa safi.
Akili za utoto, mda tunafuta yule mdogo wetu ambaye mi mdogo kati ya miaka mitatu hv ila alikua bado awezi kuongea
Alishuhudia tukio.la sisi kupiga deki pale ndani(jikoni)
Hatukuweka akilini maana alikua hawezi kuongea.
Baada ya sisi kumaliza ndipo tukamuita mama ili aendelee na hatua zingine kama ni.kupalilia au kupakua
Mama anafika jikoni hakugundua kitu, ila yule mtoto akawa ananyoosha kidole na kumwambia mama ""mama mama mmmmh mmmh"" alirudia sana mpaka mama akahisi.kitu
Mama akauliza "kuna nini hapa" kwa jinsi tulivyokua tunamuogopa.tukaanza kutetemeka.
Hapo hapo akauliza kwa ukali ile sauti ilifanya mwenzangu aseme kuwa.mimi.nimemwaga mafuta...
Hapo sikuwa na la kujitetea mama alishika mwiko na kunipiga.
Kichapo kilianzia jikoni mpaka nje.
Nyumba yetu ilikua ina Fance hvyo ni nje ya jiko. Mama alikua anauliza kama nimemwaga mafuta ila mimi nikawa nakataa
Yule mama alinipiga wakuu, yule mama alinipiga hiyo siku mpaka nikahisi kufa, wakuu yule mama alishika jaro alinipiga mpaka likaharibika.
Bado akatafuta vyekeo lakini kila akirusha kamba za nguo zikawa zinazuia lisifike kwangu.
Akanishika shingoni na kuanza kunikaba ile siku sitosahau alinikaba huku akilazimisha kunipeleka chumbani maana nilikua napiga kelele mno 🥺 🥺 🥺 🥺
Kiukweli na mimi kwenda chumbani nilikua sitaki kwani najua kule naweza kuuliwa kabisa.
Ila alifanikisha na kunifikisha chumbani. Huku akishika gongo lile ambalo hata sijui lilikua na kazi gani.
Alinipiga miguini nikajikuta naanguka chini.
Nililia sana huku namshika miguu kama ni kweli nimemwaga mafuta... Nilipigwa sana hii siku mpaka nikaenda kulala
Kiufupi kile kipigo kilidumu ndani ya masaa mawili. Baada ya kipigo nikaenda kulala mida ya saa 3 au 4 hv nakuta naamshwa naitwa jikoni..
Kufika jikoni nakutana na kesi ya kumwaga mafuta na anae soma kesi ni mama kumwambia baba kuwa nimemwaga kama lita mbili hivi .
Baba hakuuliza mara mbili alitoa mkanda akaanza kunipiga aiseee baba alinichapa ila nikiri baba alikua awezi kupiga kama huyu mama..
Baba alikua akinipiga mi mda wote nazuia sehemu moja tu ambayo ni mkononi maana nilihisi mkono ushavunjika kwa kipigo cha mama.
Baba nae alinipeleka sebureni na akaniacha akaenda kuchukua mkande wake special huo mwingine
Huo mkanda unafanana na ile mikanda ambayo.ukienda mashine za kusaga unaona.kuna.mikanda ina drive machine
Aiseee nilipigwa mnoo mnooo baada ya hapo nikaambiwa nikalale🥺🥺🥺
Seriously niliweka chuki kwa baba,
Nilimchikia sana baba yangu, nilimchukia sana baba angu.. hii chuki mpaka leo inanitafuna niliteseka sana sana sana..
Nilikuwa nawaza kurudi kwa mama.
Niliwaza hata nikajifiche kwenye buti nirudi dar ila wapi.
Hapa kati visa vikawa vingi vingi mno
Nishawahi toroka hom
Nishawahi kosa kupigwa jiwe la kichwa na mama
Nishawahi banwa korodani
Mama alikua anipendi
Mama alikua ananichukia sana......
Mungu si athumani nikapata likizo hii likizo nikaomba niende kwa.mama mzazi
Na wao wakakubali.
Hapo ndo ukawa mwanzo wa ukombozi.wangu nimefika dar sikutamani tena kurudi nikamwambia mama nipo radhi mnikate mkono.ili tu nibaki na wewe.
Bibi yangu upande wa mama alishangaa kauli zangu kwani.niliwambia kule kwa mama wa kambo mimi nakula sana , kuhusu chakula utakula utaacha wewe..
Mbeya mtu akikunyima chakula.huyo.mchawi.maana kuna vingi vya kufanya tumbo lijae
Ila kile kipigo nikasema bibi siwezi kurudi..
Hapo ndio nikabadili.jina rasmi kutoka lile jina la ubabani.na.kutumia.jina la umamani..
Majina.yana.maana.sana.katika.maisha yetu.. mimi si kwamba nilikua sina akili ila ni maisha na life style ilikua sio nzuri kwa mtoto kukua .
Nilikua na kisasi kwa huyu mama wa kambo kwanini alinifanyia vile
Why hakunipenda... Kile kisasi nilikaa nacho na nikasema ipo siku
Nitaendelea
Somo kwa ndugu zangu ambao wanatarajia kuwa na familia hapo badae.
Kwanza Mimba sio kitu cha bahati mbaya tambua hilo, usije kusema hujajipanga bado..
Pili... Wewe ndio unayeamua kesho mwanao kwa kumchagulia mama bora ambaye atatunza watoto wako...
Tatu... Mtoto kwa mama, ni wanawake wachache sana wana moyo wa kukaa na mtoto wa mwanaume... Sijui kwa sasa kama mambo yamebadilika
Ila kwa niliyopitia mimi Naomba Mungu anipe mke mwema ambaye huyo atakua mama wa watoto wangu milele.. kiufupi kuvunja ndoa hiki kitu kinaleta negative effects nyingi kuliko faida na ndio maana kwa uislam kuna vikwazo vingi kabla ya kumpa mke taraka....
Upo sahihi! Kiuhalisia mtoto alelewe na biological father and mother. Kinyume cha hapo ni mateso kwa mtotoUnavuojisifia hapa hujui tu wanao wanavyoishi na Mama wa kambo. Wewe ukirudi ukawakuta shwari basi unatulia na kuja kutype JF. Kuna mambo mengi hujui.
Daaah mpaka nimehisi huruma..Kuna jamaa ni jirani aliachana na mkewe akaoa mwanamke mwingine sasa akamleta mtoto wake aliyezaa na mke wake wa kwanza aje aishi naye pamoja na mke mpya.
Aise mtoto alikuwa anapigwa vibaya mno tena bila kosa lolote. Ni mtoto wa darasa la kwanza tu lakini anaweza kukalishwa nje hadi saa tano usiku hajalala na kesho yake anapaswa kudamka kujiandaa na shule.
Aise uvumilivu ulinishinda ilibidi nimuite mume na mke nikawaeleza kwamba ikiwa wataendeleza manyanyaso na vipigo kwa mtoto tutakutana polisi kisha mahakamani.
Maana mwanaume naye alikuwa kama fala fulani akiambiwa na mkewe tu jambo lolote kuhusu mtoto naye anaruka na mtoto kumpa kichapo. Tangu niwachimbe mkwara yule dada hakuchukua hata wiki mbili akafa akiwa anajifungua.
Yule dada mwenye kumnyanyasa mtoto mwezi uliopita alifariki akiwa anajifungua hivyo ameacha kichanga.
Watu wakawa wanasema 'alichokuwa anamfanyia mtoto wa mwanamke mwenzake sasa ni zamu ya mtoto wake wakumzaa kunyanyaswa kwasababu hayupo tena duniani '.
Kwanza mimi sibishani mkuu.Usiwe Mbishi! Hata sisi tunao ila kulea mtoto ambaye analelewa na mama wa kambo ni mtihani mkubwa hususan wa kiume akiwa mdogo. Atanyanyasika tu. Mtoto anatakiwa alelewe na mama yake mzazi, kinyume na hapo ni msala kwa baba. Inabidi iwe FBI maana mtoto anaweza akawa ana tabia mbaya kweli au mama wa kambo anamuonea!
Wanaume hawakai nyumbani .Pole sana... Ila Kwenye wazazi wa kambo lawama nyingi ni kwa wanawake tofauti na wanaume
We jamaa mi sio ndama...Humu ndani Kuna misiba mingi watu wanatembea nayo.
Siku wakipata Mkeka mtasikia vilio vipivyodumu kwa MUDA mrefu.
Baba ni Baba Mwanetu ( Ndama ).
Hakun mkuuDuh pole sana ndg poor brain
Nb hakuna mwanamke atakayehisi uchungu wa uzazi kwa mwanamke mwenzie.
Hakuna mkuu hakuna...Mkuu Poor Brain pole sana. Wewe ni kati ya wengi wanaoteseka kwa sababu ya kuvunjika kwa mahusiano ya wazazi wao. Ndio maana zamani wanawake walikuwa wako tayari kufia kwa waume zao ili mradi tu asiache watoto wake kulelewa na mwanamke mwingine. Wanaume waelewe kuwa hakuna mwanamke mwenye utayari wa kulea mtoto wa mwanamke wanaechangia bwana
Baba amekuja kubadilika mda huu ambao mimi nishakua...Pole sana mkuu, kuna wazazi wengu huwanyima watoto wao malezi ambayo ni haki yao na huleta mapenzi kati ya mtoto na baba
Kabisa.mwanaume ukiwa na mtoto wa nje na unahitaji kuishi nae mpeleke kwa bibi yake lakini kwa mkeo huwezi kuyajua yote anayopitia mtoto.Na wanaume mkishapenda huwa hamuoni kasoro kwa wake zenu sijui mnalogwa hamuelew kabisa kitu chochote hata muambiwe kwa upanga.🙌🙌🙌Mungu awasaidie watoto wanaolelewa na wale wasio wazazi wao halisi.Unavuojisifia hapa hujui tu wanao wanavyoishi na Mama wa kambo. Wewe ukirudi ukawakuta shwari basi unatulia na kuja kutype JF. Kuna mambo mengi hujui.
Hata mimi huwa sikubali kitu inaitwa divorce kwa wanangu hasa wakishakuwa na Watoto! Mtoto ni baba upande wa kulia na mama upande wa kushotoMkuu Poor Brain pole sana. Wewe ni kati ya wengi wanaoteseka kwa sababu ya kuvunjika kwa mahusiano ya wazazi wao. Ndio maana zamani wanawake walikuwa wako tayari kufia kwa waume zao ili mradi tu asiache watoto wake kulelewa na mwanamke mwingine. Wanaume waelewe kuwa hakuna mwanamke mwenye utayari wa kulea mtoto wa mwanamke wanaechangia bwana
Nishapoa mkuu..Doh! Polee sana Poor Brain
Mkuu yaani acha kabisa..Hata mimi huwa sikubali kitu inaitwa divorce kwa wanangu hasa wakishakuwa na Watoto! Mtoto ni baba upande wa kulia na mama upande wa kushoto
Ameeen..Kabisa.mwanaume ukiwa na mtoto wa nje na unahitaji kuishi nae mpeleke kwa bibi yake lakini kwa mkeo huwezi kuyajua yote anayopitia mtoto.Na wanaume mkishapenda huwa hamuoni kasoro kwa wake zenu sijui mnalogwa hamuelew kabisa kitu chochote hata muambiwe kwa upanga.🙌🙌🙌Mungu awasaidie watoto wanaolelewa na wale wasio wazazi wao halisi.