Elections 2010 Mama Salma Kikwete alalamikia kuonyeshwa alama ya CHADEMA

Huyu mama ameshusha heshima yake kwa baadhi yetu kwa kujiingiza katika mchezo mchafu wa siasa. Afhadali kaonyeshwa hivyo vidole vya Chadema ingekuwa vingine angesemaje?
 
Safi sana aende tu akaseme kwa mme wake. msafara wa mme wake uliwahi kutimuliwa na mawe huko Mbeya mwaka juzi naona wamesahau. Mbeya watu hawataki unafiki.
 
Nilikuwa nasikiliza mapitio ya magazeti leo asubuhi Tumaini FM wakanitabanisha kuwa huyu Dada akitoka Sumbawanga alipita katika moja ya miji huko Mbeya kuelekea Mbeya mjini...akaamua kuwapungia wao wakmuonyesha V sign ya vidole...kufika Mbeya katika mkutano wa UWCCM akadai anashangaa watu lkumuonyesha alama ya CHADEMA wakati yeye alitaka asalimiwe ki-CCM....sasa hii si dharau...ina maana yeye hajui kuwa kuna mfumo wa vyama vingi Tanzania na kikatiba kila mtu ana uhuru wa kupenda chama chake?...Mimi ameniudhi kwa kweli

Mimi hajaniudhi hata kidogo kwani uki-trace historia yake ni kwamba alifeli diploma ya ualimu pale moro.....sasa in such circumstances hahitaji hata kulaumiwa, nina hamu sana yakuona maandalio yake alipokuwa akifundisha....alikuwa akiwafundisha sumu tu watoto wetu
 
mke wa rais , salma kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya momba mkoani hapa ukiwemo mji wa tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani rukwa.

Akizungumza jana na wanawake wa jiji la mbeya wakati akiwa njiani akitokea sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na chadema katika salamu zao.

"nimeshangaa kuona katika mkoa wa mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana," alisema.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima ccm itashinda kwa kishindo.

Mama kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania chama cha mapinduzi (ccm).

"wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama ccm na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,"alisema mama salma kikwete.

pole mama na wewe unatakiwa kusoma alama za nyakati sio unajipitisha tu...zama hizo zimekwishapitwa hahaha

usijali mama ushindi wa kishindo ni lazima!
 
Nilikuwa nasikiliza mapitio ya magazeti leo asubuhi Tumaini FM wakanitabanisha kuwa huyu Dada akitoka Sumbawanga alipita katika moja ya miji huko Mbeya kuelekea Mbeya mjini...akaamua kuwapungia wao wakmuonyesha V sign ya vidole...kufika Mbeya katika mkutano wa UWCCM akadai anashangaa watu lkumuonyesha alama ya CHADEMA wakati yeye alitaka asalimiwe ki-CCM....sasa hii si dharau...ina maana yeye hajui kuwa kuna mfumo wa vyama vingi Tanzania na kikatiba kila mtu ana uhuru wa kupenda chama chake?...Mimi ameniudhi kwa kweli

Mama Salma Kikwete alalamikia kuonyeshwa alama ya Chadema

Na Thobias Mwanakatwe

21st October 2010

email.png

Salma%20Kikwete(6).jpg

Mke wa Rais , Salma Kikwete

Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
“Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana,” alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
Mama Kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,”alisema Mama Salma Kikwete.
Alisema wanawake ambao kura hazikutosha wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM hawana sababu ya kuendelea kukaa na kinyongo na badala yake wawape ushirikiano walioshinda kuhakikisha CCM inapata ushindi.
Aliongeza kuwa wanawake wana kila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na wanawake wenyewe kuinuliwa katika ngazi za maamuzi.
Alisema wanawake wana kila sababu ya kujivunia maendeleo ya wanawake kama ilivyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa Tanzania.

CHANZO: NIPASHE
 
“Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,”alisema Mama Salma Kikwete.
Hivi huyu mwanamke ndivyo alivyotumwa na mumewe kusema wanaume hawana msimamo?
UWEZO WA KUFIKIRI WA WANANDOA HAWA NAUTILIA MASHAKA.
 
Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
“Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana,” alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
source:NIPASHE
 
Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
"Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana," alisema.

Kweli alisema hajawahi kuona kwingine?................mh, alichakachua! ndy kusema lisahau yaliyomtokea Maswa?!!!:biggrin1::biggrin1:
 
Haiwezekani ukashangiliwa kila mahali kwani tuko kwenye vyama vingi....hizi ni siasa za ushindani...hatahao wengine sio ajabu wanakudanganya tu....the moment you know the truth the better.:dance:
 
Na bado sana,

Asuburi baada ya 31 Oct ataanza kupewa the real things...Hizo ni rasha rasha..mvua ya mawe inakuja!
 
"Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,"alisema Mama Salma Kikwete.
Hivi huyu mwanamke ndivyo alivyotumwa na mumewe kusema wanaume hawana msimamo?
UWEZO WA KUFIKIRI WA WANANDOA HAWA NAUTILIA MASHAKA.

Akili ya kuambiwa alisahau kuchanganya na ya kwakwe, lol!
 
Bado anaishi kwenye historia ya kidumu chama cha mapinduzi,,,lol!si walisema chadema haijulikani vijijini,acha wamuonyesheeee:A S thumbs_up:
 
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
source:NIPASHE

Watatujua tarehe ya uchaguzi kuwa kweli HATUDANGANYIKI SAFARI HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
"Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana," alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
source:NIPASHE
Hakutakiwa kushangaa..........hi 'nji' ina vyama vingi................. au hatambui uwepo wa vyama vingine......???
 
Back
Top Bottom