Elections 2010 Mama Salma Kikwete alalamikia kuonyeshwa alama ya CHADEMA

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
Nilikuwa nasikiliza mapitio ya magazeti leo asubuhi Tumaini FM wakanitabanisha kuwa huyu Dada akitoka Sumbawanga alipita katika moja ya miji huko Mbeya kuelekea Mbeya mjini...akaamua kuwapungia wao wakmuonyesha V sign ya vidole...

Kufika Mbeya katika mkutano wa UWCCM akadai anashangaa watu lkumuonyesha alama ya CHADEMA wakati yeye alitaka asalimiwe ki-CCM....sasa hii si dharau...ina maana yeye hajui kuwa kuna mfumo wa vyama vingi Tanzania na kikatiba kila mtu ana uhuru wa kupenda chama chake?...

Mimi ameniudhi kwa kweli

Na Thobias Mwanakatwe

Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.
Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.
"Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana," alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.
Mama Kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania Chama cha Mapinduzi (CCM).
"Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,"alisema Mama Salma Kikwete.
Alisema wanawake ambao kura hazikutosha wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM hawana sababu ya kuendelea kukaa na kinyongo na badala yake wawape ushirikiano walioshinda kuhakikisha CCM inapata ushindi.
Aliongeza kuwa wanawake wana kila sababu ya kujivunia na kutembea kifua mbele kutokana na mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na wanawake wenyewe kuinuliwa katika ngazi za maamuzi.
Alisema wanawake wana kila sababu ya kujivunia maendeleo ya wanawake kama ilivyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa Tanzania.

CHANZO: NIPASHE
 
Naogopa kuwa banned tu ila ningekuwa mimi ningempa ile alama ya kidole kimoja cha kati kutoka kushoto na kulia then V
 
Dharau za mmewe ndizo analeta hapa. Hata wafanyeje, wazt wamechoka kulaghaiwa.
 
Mimi pia nimesikia kwenye mapitio ya magazeti, nikashindwa tu kuelewa kwani yeye mategemeo yake yalikuwa nini? Kuwa kila anakopita watu wote ni CCM? Unless aseme hao waliofanya hivyo walikuwa na sare za CCM!
 
Kwanza CCM kumruhusu huyu mama kupiga kampeni ilikuwa kosa kubwa, kwanza yeye ni nani na amefanya nini katika taifa hili mpaka asimame mbele za wananchi kuinadi CCM na Mumewe?
 
Yeye anadhani kila mtu ni mwana CCM. Halafu hiyo salamu ya ki-CCM ikoje?
 
Kwanza CCM kumruhusu huyu mama kupiga kampeni ilikuwa kosa kubwa, kwanza yeye ni nani na amefanya nini katika taifa hili mpaka asimame mbele za wananchi kuinadi CCM na Mumewe?

Angalizo: JK alisema urais wake ni ubia na 'familia yake' tu kwa hiyo usishangae mama wa kwanza kuchanja mbuga kona zote za nchi huku wakipishana na kijanawao Riz 1!
 
Mimi pia nimesikia kwenye mapitio ya magazeti, nikashindwa tu kuelewa kwani yeye mategemeo yake yalikuwa nini? Kuwa kila anakopita watu wote ni CCM? Unless aseme hao waliofanya hivyo walikuwa na sare za CCM!
HATA wakiwa na SARE za CCM, KAMPENI Kuendeshwa KIFAMILIA haina tofauti na UKABILA,UDINI, na UBAGUZI MWINGINE wowote ambao Nyerere aliuita UKABURU. UKIANZA KUMPIGIA KAMPENI MUMEO, UTAENDA KABILA LAKO, DINI YAKO, CHAMA CHAKO BILA KUJALI NI FISADI, MWIZI, RAIA, MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA ALBINO? WAO WANACHO JALI NI MWENZAO
 
Mfa maji haachi kutapatapa!ukweli ni kwa hata hao watu wachache waliopo ccm wapo kwa ajili ya njaa tuu!wameichoka ccm
 
Nilikuwa nasikiliza mapitio ya magazeti leo asubuhi Tumaini FM wakanitabanisha kuwa huyu Dada akitoka Sumbawanga alipita katika moja ya miji huko Mbeya kuelekea Mbeya mjini...akaamua kuwapungia wao wakmuonyesha V sign ya vidole...kufika Mbeya katika mkutano wa UWCCM akadai anashangaa watu lkumuonyesha alama ya CHADEMA wakati yeye alitaka asalimiwe ki-CCM....sasa hii si dharau...ina maana yeye hajui kuwa kuna mfumo wa vyama vingi Tanzania na kikatiba kila mtu ana uhuru wa kupenda chama chake?...Mimi ameniudhi kwa kweli
Kwanza huyo amesababisha upungufu wa walimu arudi kwenye kazi yake!
 
Mimi ameniudhi kwa kweli

Hasira zetu tuzielekeze kwenye vituo vya kupiga kura. Mimi ninawaahidi J2 hiyo nitakuwa kituo cha kuppiga kura saa 12 asubuhi. Sitaki utani kwenye hilo. Mambo mengine yatafuata baada ya hapo..............
 
Mke wa Rais , Salma Kikwete, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya wanawake wa vijiji vya wilaya ya mpya ya Momba mkoani hapa ukiwemo Mji wa Tunduma kumuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiwa njiani akitokea kwenye ziara mkoani Rukwa.

Akizungumza jana na wanawake wa Jiji la Mbeya wakati akiwa njiani akitokea Sumbawanga, alisema aliona kundi la wanawake ambapo alipojaribu kuwasalimia kwa kuwaonyeshea mkono juu, lakini nao walijibu kwa kumnyooshea alama ya vidole viwili ambayo inatumiwa na Chadema katika salamu zao.

“Nimeshangaa kuona katika mkoa wa Mbeya, sijawahi kuona katika mkoa mwingine… nilivyofika karibu na Tunduma wanawake wananionyeshea vidole viwili, wakati maeneo mengine kila ninapopita wananishangilia sana,” alisema.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake walimfariji na kumhakikishia kuwa watake wasitake lazima CCM itashinda kwa kishindo.

Mama Kikwete alisema wanawake waonyeshe msimamo kwa kukipigania Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Wanawake wanafahamika ni watu wenye msimamo, huwezi kukuta mwanamke anahama CCM na kuhamia vyama vya upinzani na hata kama wapo ni wachache sana, lakini wanaume wao ni kawaida yao kila kukicha ni kubadilisha vyama,”alisema Mama Salma Kikwete.

POLE MAMA NA WEWE UNATAKIWA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI SIO UNAJIPITISHA TU...ZAMA HIZO ZIMEKWISHAPITWA HAHAHA
 
Bora asingesema , kwani ndio katuma msg hata kwa wale waliokuwa hawana chama
 
Huyu mama aligawa khagha, vitenge na kofia na kufanya mikutano ya kampeni kwa kina mama ile ya Shuka kwa Shuka - sasa wakati anaondoka Tunduma wale wale wamama aliowapa nguo hizi wakajipanga barabarani na kumnyooshea vidole viwili juu - yaani wakimpa vijembe kwamba hawanunuliki kwa vijinguo na vikofia - hiki ndicho kimemuuma sana festi ledi wetu.
 
Back
Top Bottom