Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Katika Dunia nimejifunza mambo kadhaa, hasa kazi ya uanasheria na uandishi wa habari.

Inaleta uhasama ambao unaweza utambua na ule ambao hauwezi kuutambua.

Katika kutekeleza kazi zetu (sisi watoto), tukumbuke kuwa tuna watu wanaotutegemea i. e. Mama/wazazi , wake zetu, watoto.

Kuna mda unajitahidi kufanya mema, na hata kuna mabaya yanatokea, ila uwezo wa kufikiria mbali matokeo hasi yakitokea, hata kama sisi tupo tayari kukabili changamoto hizi zitokanazo na kazi kiasi cha kuteseka na kesi, ajali na vifo.

Je, walioko nyuma yetu, wapendwa wetu na tegemezi, wapo tayari kuona mwisho wako wa namna hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wote wanaofanya mambo kinyume hawakulelewa vizuri? Sidhani kama kuna mzazi anamlea mwanae ili aje kupata matatizo mbeleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo sio mwanae wa kwanza wa mama kabendera kupata matatizo ndio maana anasema Katika watoto wote Kabendera ndio Yuko vizuri kwake aliwalea watoto wake ki hooligan huyo mama bila kujua urembo una mwisho
 
Unaomba mtoto wako atolewe then unasema Rais naye ni mtoto, are you serious? Watu wazima na akili zao wanamtumia kwa mtaji wao. Hivi kama kila mvunjishi sheria ambaye akifanya makosa anaombewa msamaha nani atakuwa jela? Kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, tena huyu Kabendera ame plea bargain ie amekubali makossa, sasa huyu mama yake anasema nini? Ati analala saa saba kwani nani hafanyi kazi na kulala usiku wa manane? People should realise that this country had reached a point of no return na kuendekeza uvunjifu wa sheria, itakuwa laana kubwa kwa kiongozi yeyote yule kuwahurumia watu ambao kwanza wanajiona wako juu ya sheria kushirikiana na mataifa ya magharibi kukandamiza Maisha ya Watanzania.

Yeye asubiri tu hiyo plea bargain yake hadi itakapoamuliwa. Kama rais alivyosema hatuwezi kuendelea kwa kubembelezana.
 
Hayo mambo ya laana kuna watu hawayafikirii aise! Muhimu ni kutii mamlaka na kujiepusha kushindania na wenye mamlaka vinginevyo mnyonge utaishia kuumia

Sent using Jamii Forums mobile app

Wale waliokuwa wakishirikiana naye wakiamini wanampa ujanja vyombo vya sheria visiweze kumchukulia hatua yoyote leo hii wanakula kuku mitaani na yeye yuko rumande. Inawezekana ndio wameona wamtumie mama yake awe ngao ya kumwonea huruma. Tuache kutumiwa jamani.
 
Mtoto usimchekee kwenye malezi aweza kupangisha shida mbeleni.Mama kabendera ajilaumu mwenyewe kulea watoto hovyo
Mkuu
Haya Mambo ya kupimana ubabe na mamlaka za kidunia, zilileta madhara makubwa hata kwa Yesu Kristo mwenyewe.
Nimeona pia na kusoma mauaji na mateso makubwa unapotaka ku 'prove wrong' serikali yeyote. Hata mbinguni ushindani huu kimamlaka na nguvu kulifanya Lusifer na malaika wengine waasi. Mwenyezi Mungu akamtupa huku ulimwenguni.

Steve Biko na vijana wa aina yake leo ni history kule Africa Kusini, no one cares whether they were fighting for justice or not.. Ni kovu kwa familia zao.
Kupingana na utawala, kuuchongea au kushawishi wengine waupinge, hata kama upo sahihi au hapana, lazima matokeo yake uwe tayari kuyakabili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka ale kibano sioni tena makala za ku_attack serikali .
Mama yake anasema eti alikua haendi kunywa pombe kama vijana wengine,alikua hubaki nyumbani na hulala saa zikiwa zimeenda,kumbe alikuwa anatumikia mabeberu,hafai
Kumtukana Rais nje ya mipaka ya nchi ni kulitukana Taifa, kuungana na wahujumu wa rasilimali zetu (ACACIA) na kudidimiza juhudi za mkuu wa nchi wa kuzipigania ni swala lisovumilika, alivuka mipaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yake asaugu aliumia mpaka akafariki kwa kujua mwanae kaonewa kafungwa kwa sababu ya amri kutoka juu, na kweli baada ya kumaliza kifungo mahakama ile ile iliyo muhukumu na kusababisha kumpteza mzazi wake ikasema hakuwa na hatia, hata Kabendera hana hatia ila ni amri ya fulani, Mungu wetu huwa analipa ubaya kwa ubaya atayapata yake kabla hajaiaga dunia.
 
Mkuu
Haya Mambo ya kupimana ubabe na mamlaka za kidunia, zilileta madhara makubwa hata kwa Yesu Kristo mwenyewe.
Nimeona pia na kusoma mauaji na mateso makubwa unapotaka ku 'prove wrong' serikali yeyote. Hata mbinguni ushindani huu kimamlaka na nguvu kulifanya Lusifer na malaika wengine waasi. Mwenyezi Mungu akamtupa huku ulimwenguni.

Steve Biko na vijana wa aina yake leo ni history kule Africa Kusini, no one cares whether they were fighting for justice or not.. Ni kovu kwa familia zao.
Kupingana na utawala, kuuchongea au kushawishi wengine waupinge, hata kama upo sahihi au hapana, lazima matokeo yake uwe tayari kuyakabili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi Yohana mbatizaji alikatwa kichwa aliposhindana na Herode.Mtu akishindana na mamlaka awe tayari kichwa chake kuwekwa kwenye gogo la mchinja kichwa na asipige yowe kikiwekwa kichwa chake kwenye gogo la chinja chinja
 
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."


View attachment 1291137
Naunga mkono hoja, Erick asamehewe bure!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujafa hujaumbika , hivi kama kweli Kabendera ni mtakatisha pesa huyu mama angelia namna hii ? endeleeni na ukatiri wenu lakini mtakuja kulipa tu
Myopic thinking! Unadhani mtakatishaji anagawa pesa kwa mama! Waulize akina Sigh kama wana access na hizo pesa.
 
Nimemuonea huruma sana huyu bibi na sisi watoto tujifunze tunapokuwa sehemu tujifunze tutii mamlaka tunawapa tabu sana wazazi wetu
Hata mm namuonea huruma Sana bibi yangu huyu

Ila nawakumbusha cheo ni dhamana... Kina muda.. Nguvu hizi walizotumia kumshitaki kwa kumtengenezea makosa Erick ipo siku hawatakuwa nazo


Albashir alikuwa nazo.. Ziko wapi sasa????


Muda utatuambia... Bibi yangu mama kabendera ipo siku itafurahi tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom