Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Kila tarehe 22 ya Mwezi Septemba, nchi ya Mali inaadhimisha siku ya uhuru, ambapo kwa mwaka huu 2023, Kikosi tawala cha Mali, kimefutilia mbali sherehe zilizopangwa kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru huo, kufuatia kuongezeka kwa wasiwasi wa mashambulizi yaliyotokea Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi ya Mali ilipata uhuru wake kutoka kwa Mfaransa mwaka 1960 tarehe na mwezi kama huu.
Tangazo hilo lilitolewa kwenye baraza la mawaziri wa nchi hiyo.
Mwaka jana, kiongozi wa kijeshi wa Guinea alihudhuria gwaride la kijeshi lililoandaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Mali.
Wakati wa baraza la mawaziri, kiongozi wa kijeshi wa Mali aliamuru serikali kutenga fedha zilizopangwa kwa sherehe za mwaka huu kusaidia wahasiriwa wa safu ya mashambulio ya hivi majuzi na familia zao.
Baraza pia lilijadili uwezekano wa uhamasishaji wa askari wa akiba.
Mali ilitumbukia katika machafuko mwaka 2012 baada ya watu wanaotaka kujitenga na maasi ya Kiislamu kuzuka kaskazini. Na mpaka sasa kumekuwa na vikundi jihad ambavyo vinahusishwa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Al-Qaida kama Jihadist Alliance Support Group for Islam and Muslim ambacho kwa kifupi uitwa GSIM (Group to Support Islam and Muslims)