mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi, hakuna taifa ambalo lingeweza kuvistahimili kama ilivyoonyesha Urusi. Hata mataifa ya magharibi ikiweo Marekani yameachwa midomo wazi, hawakutegemea!! Urusi imepata wapi jeuri hii??
Jibu lipo kwenye utajiri wa mali asili ilizo nazo urusi na ambazo zinahitajika duniani kote na ni vigumu kuzisusia kiuhalisia. Nchi za magharibi zimeyagomea mafuta ya urusi lakini bila aibu zimesema si harama kuyanunua kupitia nchi ya tatu!! India inanunua na kuyachakata kisha kuyauza tena kwa nchi za magharibi kwa bei ya juu!! Hata gesi ni hivyo hivyo! Wakati nchi za magharibi zinalia na mfumuko wa bei, urusi fumuko wake wa bei uko chini sana!
China ni taifa tajiri sana mara nyingi kuliko urusi lakini halina utajiri kubwa wa mali asili kama urusi. China inategemea bidhaa za viwandani ambazo soko lake kubwa ni nchi za magharibi! Halafu bidhaa hizo si za lazima katika maisha japo zina bei nafuu. China haiwezi kustahiili vikwazo kama urusi ilivyoweza!! Ndiyo maana piga ua, china haina ubavu wa kuivaia Taiwan maana japo ina uwezo mkubwa wa kuivaia na kuinyoosha Taiwan, lakini inajua haitakuwa na uwezo wa kustahiili vikwazo vya kiuchumi!! Itaendelea kuwa mpole!