Mali asili ni mali ya uhakika: Bila utajiri wa mali asili saa hii tungekuwa tumeisahau Urusi.

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,040
Vikwazo vya kiuchumi alivyowekewa Urusi, hakuna taifa ambalo lingeweza kuvistahimili kama ilivyoonyesha Urusi. Hata mataifa ya magharibi ikiweo Marekani yameachwa midomo wazi, hawakutegemea!! Urusi imepata wapi jeuri hii??

Jibu lipo kwenye utajiri wa mali asili ilizo nazo urusi na ambazo zinahitajika duniani kote na ni vigumu kuzisusia kiuhalisia. Nchi za magharibi zimeyagomea mafuta ya urusi lakini bila aibu zimesema si harama kuyanunua kupitia nchi ya tatu!! India inanunua na kuyachakata kisha kuyauza tena kwa nchi za magharibi kwa bei ya juu!! Hata gesi ni hivyo hivyo! Wakati nchi za magharibi zinalia na mfumuko wa bei, urusi fumuko wake wa bei uko chini sana!

China ni taifa tajiri sana mara nyingi kuliko urusi lakini halina utajiri kubwa wa mali asili kama urusi. China inategemea bidhaa za viwandani ambazo soko lake kubwa ni nchi za magharibi! Halafu bidhaa hizo si za lazima katika maisha japo zina bei nafuu. China haiwezi kustahiili vikwazo kama urusi ilivyoweza!! Ndiyo maana piga ua, china haina ubavu wa kuivaia Taiwan maana japo ina uwezo mkubwa wa kuivaia na kuinyoosha Taiwan, lakini inajua haitakuwa na uwezo wa kustahiili vikwazo vya kiuchumi!! Itaendelea kuwa mpole!
 
Marekani haina kabisa ubavu wa kupambana na Urusi kijeshi, lakini inajua ina uwezo wa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, japo haikujua kuwa uwezo wa urusi wa kustahimili vikwazo hivyo ni mkubwa kiasi hicho!
Sawa mchambuzi kutoka buza kwa mpalange
Nakukumbusha Afrika ina utajiri mkubwa wa tasilimali ila ni maskin wa kutupa na sio tishio hata kidogo
 
USA 🇺🇸 ni viwango vya Uganda 🇺🇬, naona soon USA 🇺🇸 ataanza kupeleka mashoga wake Uganda 🇺🇬 ili wakawafundishe Waganda uchafu ambao haukubaliki hata kidoogo
 
Sawa mchambuzi kutoka buza kwa mpalange
Nakukumbusha Afrika ina utajiri mkubwa wa tasilimali ila ni maskin wa kutupa na sio tishio hata kidogo
.
JamiiForums-2066617636_111746.jpg
 
Mnapouzungumzia Urudi,
Mnaizungumziaje Tanzania na hizo maliasilia😁
Sisi Bado kuisha?
 
Marekani haina kabisa ubavu wa kupambana na Urusi kijeshi, lakini inajua ina uwezo wa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, japo haikujua kuwa uwezo wa urusi wa kustahimili vikwazo hivyo ni mkubwa kiasi hicho!
Sio puti aliye tamka kwamba atakaye msaidia Ukraine naye atampiga????
Mwaka umekatika Ukreine anaendelea kusaidiwa na mzigo wa leo leo Umeingia!

 
Hvi nyie washabiki wa Urusi bhana , nyie mnapambana na ukraine au Urusi, kivita chenyewe ndo kina miez kadhaa sjui mwaka mmoja , vita huwa zinaenda miaka 5,6 mpak 20 huko ndo mshindi anaonekana ,
 
Back
Top Bottom