Malezi ya Mama pekee husaidia kugundua kipaji kuliko ya wazazi wote wawili

beatboi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
457
1,125
Naamini kila binadamu amezaliwa na kipaji ila ukija kwenye uhalisia inakuwa tofauti,

1. Watoto waliolelewa malezi bora(baba na mama) wanakosa muda wa kuangalia vipaji vyao kwa kubanwa pande zote mbali. huwa na vipaji vya elimu? wenyewe wanakwambia wana vipaji vya kusoma japo wengine wananunua vyeti kama bashite hilo nitalielezea baadae, na wakisoma wamesoma kweli na ndio hao wanapishana angani kila siku wakirudi mavyuoni huko ughaibuni. Na wengine wanapishana mjengoni kujadili hoja za bandari, wengine madaktari, marubani, mainjinia nk. inawezekana ikawa ni vipaji lakini vipi kuhusu mhasibu nae alizaliwa na kipaji cha kuhesabu hera😂, japo kuna wa masingle mother lakini ni wachache sana. Maono yangu kusoma sio kipaji ni kushughulisha ubongo wako na kujituma utapata matokeo chanya, hilo tunalitoa kwenye kipaji sababu walikosa muda wa kuonyesha vipaji vyao

2. Watoto waliolelewa na mzazi mmoja (i mean single mother).
hawa ndio huwa na kipaji na ndio watu maarufu zaidi duniani. Malezi ya Mama huwa yanampa uhuru sana mtoto kwa kuamua kufanya anachokipenda, tofauti na wanaopata malezi ya baba. mfano wa vipaji hivyo ni kama kuimba,kucheza soka,kuigiza nk. Hawa ndio wenye nguvu ulimwenguni kama wasanii,wanasoka,waigizaji nk. ili nyimbo ipendwe wasifiwe wakina mama au wadada au pisi kali kila mtu ataipenda sababu asilimia 75 ya waTz wengi wamelelewa na wamama pekee. Hivyo wamama husaidia kusapoti vipaji vya watoto wao ili kuwafurahisha kwa kuwaacha kufanya wakipendacho.

Kama mtoto wako analelewa na single mother mtengenezee mazingira mapema kwa kupitia kipaji cake.
Huo mtazamo wangu kwako wewe unaonaje...
 
Back
Top Bottom