Wazazi wajikite kujenga misingi bora ya malezi ya watoto wao

prince basho jr

New Member
Jul 29, 2022
3
6
WAZAZI WAJIKITE KUJENGA MISINGI BORA YA YA MALEZI YA WATOTO WAO.

Kasi ya mabadiliko ya hali ya maisha imekuwa ikitengenisha wazazi na watoto wao hadi kufikia wazazi kukosa muda wa kutosha kukaa au hata kuishi na familia zao kwa muda mrefu katika Dunia ya sasa.

Katika Dunia ya sasa sio jambo la ajabu kuona wazazi kwa juma zima hawana muda wa kukaa na watoto wao hata kwa masaa mawili na kuona maendeleo ya vijana wao ya kitaaluma na kitabia pia kutokana na harakati za maisha.

Familia nyingi zimekuwa chini ya malezi yasiyokuwa ya wazazi zaidi ya yale ya wadada na wakaka wa ndani (house boy na house girl) kwa zile zilizokuwa na kitapato kikubwa sehemu kubwa ya malezi ya familia zao zimekuwa ni kwenye taasisi za elimu.

Lakini zile ambazo ni za vipato vya chini vimeachagua mitaa kuwalelea watoto wao, kule maeneo ya uswahilini sio jambo la ajabu kuona mtoto wa miaka 4 na kuendelea akibadilisha baraza na mitaa kuanzia asubuhi hadi jioni kwa kuwa wazazi wapo katika utafutaji wa maisha.

Malezi yote haya yamekuwa na changamoto mbali mbali kwa watoto wa sasa kwa kuwa watoto wamekuwa wakiiga tabia mbali mbali zikiwemo tabia nzuri na tabia mbaya ambazo zimekuwa changamoto za kwa mustakabali wa maisha yao.

Wale wengi wao wanaopata malezi kutoka kwa watumishi wa ndani na shule wamekuwa wahanga wa kujiingiza katika tabia za watu wa Ulaya magharibi kwa kiasi kikubwa mfano wa tabia hizo ni aina ya mavazi na chakula ila mbaya zaidi ndio wametumbukia katika dimbwi la mahusiano katika umri mdogo na yasio na stara.

Wale wanapata malezi kutoka mtaani na baraza mbali mbali za uswahili nao wamezama katika dimbwi la Ulevi, wizi na unyang’anyi wa aina mbali mbali lakini mbaya zaidi jamii imepata zao kubwa la madada poa uko mitaani.

MISINGI BORA YA MALEZI.

Dhana ya misingi bora ya malezi imejipambanua kwa upana zaidi ila wengi wamekuwa wakiitafsi kwa namna tofauti dhana hiyo.

Sehemu kubwa ya watu wengi wamekuwa wakitafsi dhana hiyo kwambo miongoni mwa misingi bora ya malezi kwa mtoto ni kupata elimu katika shule kubwa na mambo mengine mengi.

Lakini dhana ya misingi bora ya malezi ni mzazi kumlea mtoto katika muelekeo na tabia njema na zenye kulinda na kuthamini utu wake na jamii yake.

VYANZO SABABISHI VINAVYO SABABISHA UKOSEFU WA MALEZI BORA.

Kuna sababu mbali mbali zinazosababisha ukosefu wa malezi bora kwa watoto baadhi ya sababu hizo ni wazazi kuwa na kazi zinazofanana mfano unaweza kukuta wazazi wote ni madaktari, wanajeshi nk. kuvunjika kwa ndoa, mimba za mitaani.

NAMNA BORA YA KUTOA MALEZI BORA KWA MTOTO.

Tenga muda wa kukaa na familia yako ilikujua tabia za mtoto wako ikiwemo uwezo wake wa kufikiri mambo anayopenda kuyafanya kwa muda wake mwingi.

Tenga muda wa kukaa na mtoto wako na kumpa elimu mbali mbali juu ya mambo yanayozunguka jamii na kubainishia matokeo chanya na hasi juu ya matendo mbali mbali ndani ya jamii.

Kuwa rafiki wa mtoto wako ili aweze kukuambia mambo mbali mbali anayokutana nayo anapokuwa peke yake au kwenye makundi ya watoto wenginie.

Kemelea matendo maovu papo kwa papo pindi yanapotokea au unapoona vishiria vya matendo hayo.

JINSI YA KUHIMILI CHANGAMOTO ZA MAISHA NA MALEZI.

Wajuzi wa maswala ya malezi na mahusiano wanashauri kuwa ili kupata malezi bora kwa watoto ni jambo jema wakati wa kuingia katika mahusiano na ndoa haswa kwa waajiriwa ni vyema kuangalia aina ya kazi mnazofanya je zinawapa muda wa kumpuzika na familia, kuepuka mahusiano holela yanayopelekea mimba za mitaani, kuepuka migogoro isiyo ya msingi inayoweza kuvunja ndoa.

8AF553B4-3267-49B2-AD1C-D3F9D8D3878A.jpeg
 
Back
Top Bottom