Kwanini Mzee Malecela alijulikana ghafla kama “Jumanne”?

Mlalahoi,

Mwaka jana kwenye kugombea nafasi ndani ya CCM, inaeleweka kuwa JM hakuondolewa kihalali, we ulikua hujui hilo?, na hata akigombea tena hawatampa, nimesikia sikia kuwa ana visasi, wanamuogopa. Kama ni uongo au kweli mi sijui. Jamani mtafanya tuandike tusiopenda kuandika, tunaomba hizi personal topics zifungwe!

Kwahiyo hiyo point ya pili nai crash, ile ya kwanza unaweza kuwa sahihi.

FD
 
Katika kipindi chake cha miaka zaidi ya arobain serikalini, Malecela amekuwa na record nzuri na mbaya. Ninadhani kuwa record yake mbaya ndiyo imemletea doa katik effort zake za kutaka urais wa Tanzania. Katika miaka ya sabini alipokuwa waziri wa mambo ya nje kabla hajahsmihiwa Kilimo, nasikia kuwa aliboa kitu fulani katika kuiwakilisha Tanzania katika mkutano mmjawapo kwa namna ya kujikweza zaidi ya bosi wake. Nyerere akamuondoa mara moja na kumweka Mkapa, kazi ambayo Mkapa alikaa nayo kwa muda mrefu sana kabla ya kumpisha Salim na baadaye kuichukua tena.

Mwanzoni mwa miaka ya 80 akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi, alikuwa kwenye hafla ya TRC. Baada ya kunywa bia moja au mbili tu, mzee akaboa kusema kama watu wanaodai kuwa usafiri wa reli ni mbaya "they can go to hell."

Vile vile inasemekana kuwa mara baada ya kifo cha Sokoine, Mzee Timothy Apiyo alimwuliza kama angekuwa tayari kubeba madaraka ya uwaziri mkuu. Mzee Malecela kusikia huvyo akaweka pati na rafiki zake kusherehekea kuwa atachaguliwa kuwa Waziri Mkuu hata kabla watanzania hatujamaliza maombolezo.

Inawezekana kuwa huyu Mzee anaweza kuwa na busara na nguvu ya kushawishi, ila lakini tamaa yake ya madaraka na kuropoka kwake mambo yasiyokwa na maana vimechangia kumrudisha nyuma kisiasa.
 
kazi ni kubwa sana .Ila issue hapa ni kwamba ni kweli JM aliitwa Jumanne hata kama ni kwa masaa na je sababu ipi ? Mama yule kusema JM anaitwa J4 hamwezi kuona kaukweli ndani yake maana yeye alikuwa analala naye na hivyo siri zake atakwua alizijua ? Madai kuitwa J4 kwa kuwa aliahidiwa ama hata kupatiwa pesa toka Iran ama Uarabuni ili atumie kwenye kampeni yake kuna ushahidi wowote ama ni maneno ya kupelekea ku justify jina la J4 ?
 
Kwa kweli na mimi nilisikia kuwa Malecela aliwahi kubadili dini kwa ajili ya kupata Urais.By the way,hakuna sababu nyingine ya yeye kuitwa Jumanne if he didnt take up that name when aliposilimu.However,nasisitiza kuwa nilisikia tetesi tu na inasemekana uamuzi wa kubadili dini ulitokana na conditions alizopewa na Wairan.Same story as ile ya Rostam kutumiwa na Wairan.Panapofuka moshi...
 
Mlalahoi
Nyerere alikuwa hampendi Dr.Salmin mbona hakuweza kuzuia hadi alipofika? hata Mwinyi alikuwa hampendi na alikuwa akim frasturate kila dakika hadi Mzee Thabit Kombo akaamua ugomvi. siamini kuwa Nyerere alikuwa Mungu ambaye angemzuia Malecela.
Na kuhusu kusilimu kwa ajili ya urais labda alihisi ukiwa muislam unakuwa muadilifu sana ktk majukumu yako hakutaka kufuata nyendo za mwalimu.
 
mswahili said:
Mlalahoi
Nyerere alikuwa hampendi Dr.Salmin mbona hakuweza kuzuia hadi alipofika? hata Mwinyi alikuwa hampendi na alikuwa akim frasturate kila dakika hadi Mzee Thabit Kombo akaamua ugomvi. siamini kuwa Nyerere alikuwa Mungu ambaye angemzuia Malecela.
Na kuhusu kusilimu kwa ajili ya urais labda alihisi ukiwa muislam unakuwa muadilifu sana ktk majukumu yako hakutaka kufuata nyendo za mwalimu.

Kama ni kweli kuwa Malecela aliwahi kusilimu ilikuwa ni kwa ajili ya tamaa kutaka petrodollars za kuendeshea kampeini ya uraisi; hakuna lolote. Mbona baada ya kuukosa uraisi alirudi mtaani? Inawezekana alikuwa anataka kuwabluff wairan kusudi wampe hela halafu akisha ukwaa urais ageuke kurudi mtaani tena. Kwa vyovyote tu hiyo ilikuwa ni tamaa na kukosa uaminifu
 
Mswahili unasema kuwa Rais muislam ni uadilifu ? Haya makubwa jamaa yangu . Kama kweli Uislam ni uadilifu basi mimi sina la kusema
 
mswahili said:
Kichuguu
mimi ni mmoja wa wadhamini wa Masjid Nuur.niko mimi. mkobo na alikuwepo Mituro wangine sitaki kuwataja.
Malecela alikuja lini pale? Mkristu aliyeingia pale ni Ritta Mlaki akiwa na kofia ya ukuu wa wilaya ya kinondoni wakati huo BM akimtangaza lakini nae hatasau siku ile.
Wewe wazungumza miaka ya juzi, tunasema mwishoni mwa mwaka 1994 hadi katikati ya 1995 kuelekea uchaguzi uliomleta BM madarakani; inawezekana mara nne tano zikawa nyingi zaidi lakini at least mara mbili aliwahi kufika pale. Najua hakuja kama mtu wa kusali kwa vile alikuwa amevalia Chou En-Lai Suti siyo kanzu, kwa hiyo huenda hakuingia kwenye sehemu ya kufanyia ibada, lakini alifika pale msikitini. Mimi nilmwona kwa macho yangu wakati tukiwa tunakunywa bia pale kwenye container iliyokuwa pembeni mwa barabara karibu na Kumekucha Auction Mart. Kufika kwake kulikuwa kunatukera sana wengine kwa vile barabara zilikuwa zinafungwa na hivyo kusababisha congestion iliyokuwa inatuaharibia starehe zetu pembeni mwa barabara.
 
tibwilitibwili said:
Mswahili unasema kuwa Rais muislam ni uadilifu ? Haya makubwa jamaa yangu . Kama kweli Uislam ni uadilifu basi mimi sina la kusema
Kama kweli kila rais muislamu angekuwa ni mwadilifu basi Loliondo ingekuwa bado ni sehemu ya Tanzania; lakini sasa hivi Loliondo ni sehemu ya ufalme wa uarabuni.

Inasemekana kuwa marehemu Professor Kighoma Malima (RIP) alikuwa amefungua account binafsi kwa jina lake eti kutunza pesa za serikali; huo kweli ndio uadilifu.
 
Muislam na Uislam hauwezi kukosa shukrani kwa kiongozi aliye chaguliwa na wengi .Watu wote walio mtukana baba wa taifa hawafanyi kwa faida ya waislam na uislam . Sisi Waislam tunasema jina letu linatumika kwa maslahi ya binafsi na kurani tukufu haiwezi kamwe kukubali kashfa dhidi ya kiongozi alye chaguliwa na watu . Uislam ni amani na upendo leo ndugu zanguni akina Mswahili hata majina mnaficha kumshambulia marehemu Nyerere na kuacha kupambana na udhalimu unao fanywa na Waislam wenzetu ni makosa . Leo hii Muislam mwenzetu rais Kikwete anampa mwanaye ukurugenzi mbele ya macho yeti waislam tunakaa kimya ni haramu kubwa .

mimi si msemaji humu nimekuja baada ya kuona ndugu yetu Mukandara kajaribu kuwapa Elimu dunia lakini bado mnaendelea mbegu ya ubaya na ubaguzi .haya ni mambo ya waarabu ambao pamoja sisi ni Waislam kama wao lakini hawatukubali kamwe kuchangamana leo tunabadilikla tunaanza kumtafuta Mwalimu ? Tuache swala hil walisema wakristo lakini sisi Waislam tuangalie ambayo yanafanywa na waislam wenzetu ambayo hayampendezi mola wetu na yanayo enda kinyuma na kurani tukufu
 
Mswahili Sheikh Muislam kusema uongo ni dhambi kubwa .Mimi ninakumbuka Mzee Jumanne Malecela kuja msikitini akiwa na nia kubadili dini na sote tulisikia kwa pembeni labla ya kumuona msikitini.Mzee alikuja mara nyingi sana na alikuwa anavaa kofia akishuka ndani ya gari lake na baada ya sala aliondoka na kuagana na wamumini kwa muda mwingine wa ibada . Kuja msikitini mzee huyu alikuja na si mara moja .Rita mimi sikuwahi kumuona
 
Hussein Abdallah said:
Mswahili Sheikh Muislam kusema uongo ni dhambi kubwa .Mimi ninakumbuka Mzee Jumanne Malecela kuja msikitini akiwa na nia kubadili dini na sote tulisikia kwa pembeni labla ya kumuona msikitini.Mzee alikuja mara nyingi sana na alikuwa anavaa kofia akishuka ndani ya gari lake na baada ya sala aliondoka na kuagana na wamumini kwa muda mwingine wa ibada . Kuja msikitini mzee huyu alikuja na si mara moja .Rita mimi sikuwahi kumuona
Afadhali wewe umesema ukweli. Wewe ndiwe mwislamu halisi kama wale ambao nimekulia mikononi mwao pale Tabora.
 
Unajua Mwalimu Baba wa taifa, baada ya kutembea na yule mama wa Shinyanga, yaani originally hawara wa Professor Makene daktari wake, ambaye alimyanga'anya, aliamua kumuweka under arrest, kule Shinyanga ili wanaomchukia wasiongee naye na akampa amri ya kuonana na watoto wake tu Noella na Doris, hakuna mtu mwingina liyeruhusiwa na Mwalimu kuongea na huyo mama,

Hakuishia hapo tu Mzee ambaye alikuwa rais wetu wa kwanza na ambaye alimuta Malecela muhuni kwa sababu ya wakuwa na vimada, sasa akaanza kutembea na Mama Mary Mackeja, naye kutoka huko huko Shinyanga na kumfanya Katibu Mkuu wa Red Cross Tanzania, huku akisafiri naye kwenye kila msafara wa nje na kujimwaga naye,

To be continued...........!
 
Mzee Es said:
Unajua Mwalimu Baba wa taifa, baada ya kutembea na yule mama wa Shinyanga, yaani originally hawara wa Professor Makene daktari wake, ambaye alimyanga'anya, aliamua kumuweka under arrest, kule Shinyanga ili wanaomchukia wasiongee naye na akampa amri ya kuonana na watoto wake tu Noella na Doris, hakuna mtu mwingina liyeruhusiwa na Mwalimu kuongea na huyo mama,

Hakuishia hapo tu Mzee ambaye alikuwa rais wetu wa kwanza na ambaye alimuta Malecela muhuni kwa sababu ya wakuwa na vimada, sasa akaanza kutembea na Mama Mary Mackeja, naye kutoka huko huko Shinyanga na kumfanya Katibu Mkuu wa Red Cross Tanzania, huku akisafiri naye kwenye kila msafara wa nje na kujimwaga naye,

To be continued...........!


Mzee ES na wewe umefiliskika kimawazo.
 
Hapana ndivyo nilvyoaihidi, halafu hayo maneno yako ninayaita NONESENSE, maana kumtukana Malecela kwako wewe na Rufiji, Tafiti, ni kuwa na heshima kwenye hii forum na hii forum inakuwa namba moja,

isipokuwa akiguswa Mungu wenu aliyewafundisha matusi ya uongo dhidi ya Malecela, basi nimefilisika mawazo, na hii forum inashuka hadhi what a standard!

Hongera bro kwa kuongezeka mawazo na heshima kwa kumtukana Malecela!
 
mimi ni mgeni humu lakini nimeshangaa sana na michango yenu . Nimeona wengi wana heshima kwa baba wa taifa na wachache hawana na labda wanalinda maslahi ya watu wao . Lakini swali moja ni kwamba baada ya hadith za mtaani dhidi ya mwalimu mzee es unategemea kuvuna nini ?Unadhani mzee malecelea anaweza kumfikia mwalimu Nyerere hata robo ? Hivi ndiyo unazidi mumharibia maana kwanza kwa maoni sijaona kama ni sahihi kumlinganisha Mwalimu na Mzee malecela . Mwalimu hata sisi waislam na watu wa nje wachilia mbali Watanzania tuna mtambua sana pamoja na kejeli na dhihaka zako na kikundi chako.Mwalimu alikuwa mtu wa pekee .Lakini pia naona unaongelea maneno ambayo wewe uliyasapotu huko nyuma.Leo mwalimu na wanawake unapiga kelele na wewe baba yako umesema alikuwa na wanawake na wewe pia una wengi na malecela anao wengi sasa kipi cha ajabu kwa mwalimu? Kumweka mtu kifungoni kwamba asiseme si ni sehemu ya maisha ya wana CCM il kulinda maslahi ya Chama na wenyewe akiwemo malecela ?Huwezi kamwe kusema malecela anafaa lolote mbele za mwalimu hata ukija na hadithi utanakuwa unaji dhalilisha zaidi .Maoni yangu nimesema baada ya kutumia siku kusoma majibizano yenu nimegundua es anajibu kwa jaba kulisha hadhi ya shemeji yake Malecela maana mke wa kwanza katoka kwenu Mbeya.
 
Vipi mke wa Mwalimu ametoka kwenu ndio maaan unameteta? Hayo maneno yako ninayaita ya chooni, hakuna anyekataa kuwa Mwalimu was the man ninachokataa ni kuwa hakuwa Mungu kama wewe na wenzio kina tafit, na Rufiji mnavyotaka kutuambia hapa, alikuwa na makosa kama wengine na hasa Malecela aliyekuwa akimshambulia all the time na kuwaachia watu kama nyinyi ambao mpaka leo hamuwezi kuona nje ya mawazo ya Mwalimu,

I am sorry kwamba mimi sio mmoja wao, Mwalimu alikuwa rais na Malecela likuwa waziri wake utawafananishaje unless una akili finnyu za siasa kama zako, halafu in the future weka maoni yako bila kunitaja maana watu kama nyinyi na mawazo yenu ya chooni nasikia kutapika, Mwalimu alikuwa binadamu kama wewe na mimi, alimkemea Malecela kuwa hafai kwa sababu ni mhuni ana wanawake wengi kumbe yeye mwenyewe ndiye nambari one wa wanawake na kuwaweka under arrest, Malecela hakufanya hayo, hzio ni baadhi za tofauti yao,

Kwa hiyo nikisema Malecela alibdili dini kama alivyosema Mwalimu ndio ninakuwa na busara, nikikataa basi hii forum imsehuka, yaani huna busara unajishusha, unatetea masilahi yako, on and on and on!

The rest kwangu ni NONESENSE!, na niatrudi kesho bro siendi kokote nipo hapa na nyinyi wapuuzi wa siasa!
 
Majuzi tulusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Mzee Jumanne ilibidi akimbie ukumbi baada ya Msekwa kuwa nominated kuwa mgombea pekee wa nafasi yake. Hadi leo sijajua kwa nini Mzee alikimbia ukumbi ule wakati jana alisifiwa baada ya kukatwa mtama kwamba ni mvumilivu wa vishindo kama Kawawa.

Lakini siku za nyuma niliwahi kuuliza Mzee John Jumanne Samwel Malecela atakumbukwa kwa lipi. Leo narudia kuuliza what will be his legacy ndani ya Chama na Serikali?

Mzee aliluwa mtemi na busara chache. Alikuwa na maneno machafu lakini alitumiwa kugombea majimbo na kuzima migogoro ndani ya CCM. Mzee yeye CCM kama JK ilikuwa ya kwanza Tanzania na Watanzania baadaye. Ndiyo maana aliwahi kutamka maneno ya dharau dhidi ya Watanzania sawa na Msuya kwamba "Go to hell".

Msuya alisha sahaulika na hata kuingia katika migogoro ya kidini huko kwao. Malecela kapewa kifuta jasho kuwa mjumbe hadi kufa ila sijajua na Ubunge sasa ataachia kwa kuwa kazeeka ama ataendeleza kulifanya mali yake.

Baada ya haya yangu naomba kusikia toka kwako. Ni nini itakuwa Legacy ya Mzee huyu aliyeshindwa kusoma alama za Nyakati sawa na Msekwa ilivyo tokea?
 
Malecela atakumbukwa na CCM kama kiongozi aliesaidia sana kurejea majimbo yaliyochukuliwa na wapinzani.

Moja ya sifa zake mzee huyu ktk kampeni huwa anakwenda mpaka ktk ngazi ya mtaa kijijini kabisa ambako hakuna hata Hotel na atajibanza na wanakijiji kulala kwenye nyumba za nyasi na tope ktk kukitumikia chama.

Hayo ya Jumanne mapya kwangu....
 
Back
Top Bottom