Viongozi wawili ambao wote waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamebakia kuwa ishara ya "kilichotokea" CCM.
Dr. Malecela bado ni kiongozi wa CCM, yaani makamu wa mwenyekiti wa CCM, na pia Mbunge wa taifa wa Mtera(CCM), Chancellor wa Open University Dar-Es-Saalam, Dr. Salim, pia bado ni mjumbe wa NEC wa CCM, kwa hiyo si kweli kwamba wamebaki kuwa inshara ya kilichotokea CCM, in fact wote wawili bado ni inshara ya yanayotokea CCM sasa hivi, na mfano mzuri ni uchaguzi wa bunge kule Tunduru, hivi karibuni ambako Dr. Malecela ndiye aliongoza kampeni hiyo upande wa ushindi, yaani CCM.
Dr. Salim, yeye hayupo nchini yupo Abuja, kama muwakilishi wa kimataifa wa Darfour, kwa hiyo hashiriki sana kwenye shughuli za kila siku za CCM, lakini huhudhuria vikao vyote vya maamuzi ya juu vya CCM, hapa bongo.
Wote wawili waliwahi kuwa mawaziri wakuu, na pia waliwahi kuwa wawakilishi wetu kule UN, na to this day heshima waliyoiacha kule kwa taifa letu, ni kubwa sana mpaka haikuwa tatizo kwa UN kutupatia nafasi nyingi za uongozi mkuuu wa UN na OAU, kutokana na misingi ya uongozi walioionyesha huko, leo wabongo tunawakilishwa huko na Mama Tibaijuka, Mama Mongella, Mama Migiro, Balozi Manongi, na bwana Yusuf. Na ni hivi karibuni tu Balozi Mahiga, alikuwa mwenyekiti wa Security Council wa Dunia huko UN, sasa wakati hawa wabongo waki-enjoy matunda ya uongozi uliowekwa na Dr. Salim na Dr. Malecela katika miaka ya nyuma, tumesikia nchi kama Kenya, Nigeria, na South Africa, wakilia wivu kwamba kwa nini wabongo tu ndio wanaopewa nafasi hizo kubwa za dunia, ukweli ni kwamba wazungu hujali references katika kutoa nafasi hizo za dunia, sio ukubwa au utajiri wa nchi.
......Itaendelea........!