Malawi paper calls Kikwete a 'Bloodthirsty Leader'

Malawi paper calls Kikwete a 'Bloodthirsty Leader'

Status
Not open for further replies.
jamani tuwe tunafikiria mbali kdogo tusiwe na akili fupi.........., jaribu kutofautisha jambo la kitaifa na usichanganye siasa katika jambo lenye mustakabali wa taifa, hata kama humkabali kikwete kisera na kiitikadi, angaalia ni mahali gani pa kuonesha hivyo, ugomvi wa Malawi na Tanzania kuhusu lake Nyasa hujaanza wakati wa kikwete, ni toka Enzi za kamuzu Banda during Nyerere era, sasa huyo kikwete kafanyeje hapo..... hapo wamalawi wanafanya propaganda yao they have unite agaist us, sisi tumekalia maneno mbofu mbofu, yaani tatizo letu watz kila jambo tunaweka siasa tu na kulaumu.
 
Pheeeew! At least Kagame can have a couple of days sleep without hearing tanzanians whinning. When more than one man says you have a problem then probably you do. Huku mnagombana na Malawi, huku mnagombana na Rwanda, huku Wakenya mara Wazanzibari...c'mon i mean doe it mean all these countries ndio wakorofi? You need to check yourself before you break yourself.
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

ucwe na akili fupi, ya kufikiria ndani ya box la siasa tu. maana cku hata kichwa kikiuma utasema kikwete kasababisha.
 
Hawa jamaa kiukweli wamejitayarisha na tutapigwa...Kwanini??? compare and contrast on CIA figures

Tanzania Military expenditure
Military expenditures:
0.2% of GDP (2005 est.)
country comparison to the world: 169
[see also: Military expenditures country ranks ]

Malawi Military Expenditure
Military expenditures:
1.3% of GDP (2006)
country comparison to the world:
112
[see also: Military expenditures country ranks ]




Kwani GDP zinalingana?

Pia huyo Mwandishi wa NyasaTimes ni mwehu.Anaandika kwa kiburi na uzuzu wa kujifurahisha na kujifariji tu

Much like the the peacock which refuses to alter its dignified manner of walking when told the forest is on fire, it comes as no surprise that there commentators like this Editor who care little for the truth. Continue deluding himself with claims like the "Tanzania knows it has no chance in hell of getting even an inch of Lake Malawi if a more civilised way of dealing with the matter is employed ", even as unassailable facts prove otherwise

Tumezungukwa na maadui wakubwa,ni lazima sasa tuongeze bajeti ya jeshi.Pia serikali sasa iache ufisadi na itumie raslimali zetu kulinda mipaka na usalama wa raia wetu.Hapa hakuna siasa na hakuna compromise.Nakerwa sana na vitisho vya majirani zetu ambao kimsingi sina uvumilivu nao
 
Sasa wewe, hivi ugomvi wa Kikwete uko wapi hapo? Yeye anatetea maslai ya nchi ya Tz, kwahiyo hawezi kuka kimya! Kwako we ni bora ziwa liende Malawi sio?
Mkuu hao wengine sio wa Tanzania, hawa ni wale wakimbizi tulio wapa uraia miaka elee.
 
To.me I think it is high time Malawi is beaten once and for all and make them behave and respect neighbours. Surely Malawi is a neighbour from hell. What is wrong with their woman president? She should be advised to.deal with her opposers and leave us alone. Currently we have enough on our plate.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Make the same advice to jk for another neighbour in the north west if you can! But do not forget the war within for corruption and drug dealers! if what you say can be a good sln anyway!
 
Malawi wanajihami kwa sababu wanajua makosa yao yakutaka kumega ziwa nyasa au ziwa malawi kama wanavyoliita wao. Tanzania hatutishiki hata kidogo ila hali ya tahadhri inhitajika zaidi katika mipaka yetu.

Naona historia ya miaka ya sabini inataka kujirudia hapo, alianza kamuzu hastingi banda kudai ziwa kama anavyofanya mama banda, baadae kidogo kenya chini ya mzee kenyata wakadai mlima kilimanjaro ni wao (sasa yupo mtoto wake), hatujakaa vizuri uganda ikamega eneo la kagera wakati huo ukijulikana kama mkoa wa ziwa magharibi.

Niamini aliyeonyesha kuhatarisha uhuru wetu, tukamshugulikia mara moja kakimbia na asijue alikokuwa anaelekea, mara libya mara saudi arabia. Wengine wote wakafyata mkia, sasa naona wameanza kwa mfuatano ule ule, tutasimama.
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.


Are you serious? Kwani hawa malawi wameanza leo kusema kuwa ziwa nyasa lote la kwao? Umesahau tulipigana na mreno msumbiji hakua adui yetu jirani? Vipi kuhusu Idd Amin? Vipi kuhusu sera za mwalimu za kijama dhidi ya za kibepari za Kenyatta hatukufikia hatua ya uadui? JWTZ imepigana Zambia, Angola, Namibia,Zimbabwe na tulikuwa maadui namba moja ya makaburu wa south africa. Hivi nyie kizazi cha Mulugo hamfundishwi haya darasani?????
 
Wamalawi wanasema "fire should be met by fire",naona wanasubiri wao ndo wavamiwe?kama wanaamini ziwa lote ni lao,si tayari washavamiwa?wanachosubiri ni kitu gani?

Nadhani JK naye alizungumzia "wavamizi",sasa sijui nani ataanzisha hiyo fire itakayokuwa met by fire?

Wao wana upande wao wa ziwa na sisi tuna upande wetu.Kama wanaamini kuwa upande wetu ni wao,basi ina maana tayari kwao hiyo ni "fire",tunasubiri fire yao sasa?
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.
Mungi, Heshima yako mkuu. Sio kweli kwamba JK ndiye kasababisha tuwe na ugomvi na Malawi.

Mgogoro wa Malawi na Tanzania ulianza toka ya kwanza ya Mwalimu Nyerere. Nakumbuka kuna wakati tulipeleka mjeshi yetu eneo moja linaloitwa Manda wilayani Ludewa mkoani Iringa sasa Njombe, na kufanya mazoezi ya kijeshi mpakani hapo. kuanzia siku hiyo Rais wa Malawi kipindi hicho akafyata mkia na kutuliza chokochoko zake. Kwasasa mgogoro huo unakuzwa kutokana na Gas na Oil inayohisiwa kuwemo ndani ya ziwa Nyasa/Malawi. Na mgogoro huo unakuzwa kutokana na support Wamalawi wanaipata kutoka UK, hii ni kwasababu kampuni ya waingereza ndio waliopewa kibali cha kutafiti uwepo wa nishati hiyo, ambapo kwa asilimia 70% inaaminika kuwa ipo.

Vilevile, Dada Joy anataka urais na kura yake ya turufu ni kulichukua ziwa lote. Kumbuka mitaalaya Elimu nchini Malawi hailitambui ziwa nyasa hata kidogo wala hailijui ziwa hilo liko wapi, bali wao wanalitambua na wnawafundisha watoto wao tangu wamepata uhuru kuwa kuna ziwa Malawi.

Lakini Mungi, hivi ulitaka serikali ya Tanzania ikae kimya dhidi ya chokochoko za Malawi na Rwanda?, Hivi ushauri alioutoa JK juu ya kagame kuzungumza na waasi ni kosa? Hivi dharau alizoonyesha Kagame dhidi ya nchi (JK) yetu ni sawa? Au unataka kutuambia kuwa ni sawa na haki sisi kudharauliwa na kuingiliwa mipaka yetu na nchi jirani kuliko sisi kurespond dhidi ya dharau zao na chokochoko zao?

Kwa ushauri tu, hili suala la Malawi na Rwanda tuondoe tofauti za kisiasa na tuubebe uzalendo kwa pamoja kwa kumuunga mkono JK na kuwaonyesha hao mahafidhina kuwa sisi sio wapole hata kidogo, bali tumekomaa kidplomasia.
 
Kwasasa mgogoro huo unakuzwa kutokana na Gas na Oil inayohisiwa kuwemo ndani ya ziwa Nyasa/Malawi.
Mkuu una maana Malawi hawalitambui ziwa Nyasa kwenye mitaala yao ya elimu bali wanalitambua ziwa Malawi? Would the name make any difference?
 
To be honest I am one of those Hawkish and hard-line individuals when it comes to international policies.

My political stand on International affairs is firmly based on modernizing our military abilities and weapons' capabilities.I like to see my Countryis investing heavily on air military force,land military force and sea military force. I like to see my Country buying war-ships with highily advanced technologies. I like to see my Country increasing its military budget to cover military spending. I like to see my Country's Intelligence Agency reformed and more modernized interms of its operations.

The Agency should focus more on spying on other Countries for both security and economic as well as technological purposes/reasons. This would be a long term security programs. I would like to see my Country conducting a military shows to showcase its its highly advanced military weapons' capabilities to the world to see.

At this particular in juncture Malawi would have never dared to say anything stupid about my Country.



I agree with you Mkuu!! Ikiwezekana hata bajeti ya mwaka mmoja watu tuishi kwa mishahara tu lakini hela nyingine zote zipelekwe jeshini,hilo linawezekana kabisa maana tumekuwa tukilishuhudia mwaka wa uchaguzi mkuu huwa wanafanya hivyo!Tuchome kama U.S.D BIL 5 hivi tununue vifaa vya ukweli, hata kelele za majirani zitapungua tukifanya hivyo.
 
Asante sana mkuu umempa somo na kama anayo AKILI amekuelewa.
Mkuu tusiwapotoshe wanajamvi kwa uvivu tu wa kusoma na kufanya research. Kwanza kabisa lazima uelewe uwezo wa kijeshi au military strength wa nchi huwa unaangaliwa kwa kuchukua vigezo vingi na si kuangalia kigezo kimoja au viwili tu. Hiyo percentage of GDP uliyoweka ni sehemu moja tu kati ya vitu karibia kumi vya kuangalia ili ujue nchi moja inaizidi military strength nchi nyingine. TATU,data za GDP ulizotumia ni za mwaka 2005 na wamekuambia ni estimation tu. Je unajuaje kama kila nchi imefanya update zipi mpaka kufikia hii mwaka 2013?. Ndio maana kwenye research wanakuambia ukiona una andiko au kitabu cha kufanya reference cha mwaka 2005 basi jitahidi utafute andiko la karibuni i.e at least year 2010. SASA BASI: Kwa mujibu wa Report ya Mwaka 2013 ya taasisi ya Stockholm International Peace Research Institute(Yearbook 2013), msimamo/rank kwa kigezo cha world rank,amount spent na %GDP kwenye mabano ni hivi: Kenya (78)(Usd 594000,000)(2.0%),Uganda(95),(Usd 276,000,000)(1.8%),Tanzania(103),(Usd 217,000,000),(1.1%),Rwanda (125),(Usd 77,200,000),(1.4%),Burundi(137) (Usd 46,900,000)(3.8%). Sasa, tazama nyingine chache za nje kidogo ya EAC: Malawi (136)(Usd 48,600,000)(1.2%),DRC (110) (Usd 163,000,000) (1.0), Seycheles (154)Usd 6,600,000) (1.2%). Nimekuwekea figure hizo ili uelewe kidogo kwamba military strength haiangaliwi kwa kigezo kimoja tu. Mfano, kwa kutumia kigezo cha amount spent nchi inayoongoza kwa Africa ni Algeria(29 in world ranks) (Usd 5,586,000,000) but has %GDP 3.8 equivalent to Burundi!. Also Malawi %GDP is 1.2 which is equal to that of Sycheles,does it mean Malawi military strength equal to that of Sycheles?.
Kumalizia ni kwamba,uwezo wa kijeshi wa nchi unapimwa kwa vigezo au parameters nyingi na si tu unatumia kiasi gani cha GDP yako. Je kama hiyo %kubwa unayojivuna kutumia unawalipa askari tu na haununui zana imara itakusaidia nini. Mfano mdogo ni Vita vya Kagera ambapo Iddi Amini kwa kusaidiana na Ghadafi walikuwa na zana za kisasa kuliko Tanzania. Lakini askari wao hawakuwa na ujuzi mkubwawa kutumia zana mbalimbali na pia hawakuwa na nidhamu. Matokeo yake unayajua.Au kama country yako iko vurnerable due to geographic position,weather,small population,number of able and active military personel etc bado hiyo %GDP spent itakuwa kigezo kimojawapo kidogo tu cha nguvu ya kijeshi.
(
 
Ni sawa... kwa hili la Malawi naweza kubaliana na point yako so far uadui ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa.
Lakini kulikuwa na ulazima gani kwa Kikwete kuwa na uadui na Kagame?
Kulikuwa na ulazima gani kwa Kikwete kuwapeleka wanajeshi wetu kwenda kuwapiga wakongo wanaopigana na wakongo?
Mediation ya mtutu wa bunduki sijaufahamu. Imagine yule anayempiga akifika mahali akawa rais wa Kongo unadhani nini kitatokea?
Kikwete amekuwa na maadui wengi ndani ya nchi, mmojawapo waalimu, ndiyo maana waalimu wakatuhukumu collectively kwa upuuzi wa mkuu wa nchi. division 0 kama sala...............
Kujua kwingi kunapoteza maarifa! Kosa la Kikwete katika hili ni lipi:
  1. Kumshauri Kagame kufanya mazungumzo na wapinzani wake?! Mbona hili ni jambo la kawaida duniani kote kuwaweka wapinzani katika meza ya mazungumzo ili amani ipatikane! Karume na Maalim Sefu walikaa meza moja na kukubalianza kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa na hivi sasa amani angalau kwa kiwango fulani imerejea Zanzibar!
  2. Kupeleka jeshi letu Goma - Congo ili kuwalinda raia wasio na hatia ni kosa?! Mbona tumepeleka majeshi yetu nchi nyingi duniani kulinda amani na hakuna utawala wo wote ulioonyesha wa nje uliowahi kutishia amani yetu!
Tanzania kama moja ya jamii katika dunia hii tuna wajibu wa kulinda na kudumisha amani ya dunia!
 
Mungi, Heshima yako mkuu. Sio kweli kwamba JK ndiye kasababisha tuwe na ugomvi na Malawi.

Mgogoro wa Malawi na Tanzania ulianza toka ya kwanza ya Mwalimu Nyerere. Nakumbuka kuna wakati tulipeleka mjeshi yetu eneo moja linaloitwa Manda wilayani Ludewa mkoani Iringa sasa Njombe, na kufanya mazoezi ya kijeshi mpakani hapo. kuanzia siku hiyo Rais wa Malawi kipindi hicho akafyata mkia na kutuliza chokochoko zake. Kwasasa mgogoro huo unakuzwa kutokana na Gas na Oil inayohisiwa kuwemo ndani ya ziwa Nyasa/Malawi. Na mgogoro huo unakuzwa kutokana na support Wamalawi wanaipata kutoka UK, hii ni kwasababu kampuni ya waingereza ndio waliopewa kibali cha kutafiti uwepo wa nishati hiyo, ambapo kwa asilimia 70% inaaminika kuwa ipo.

Vilevile, Dada Joy anataka urais na kura yake ya turufu ni kulichukua ziwa lote. Kumbuka mitaalaya Elimu nchini Malawi hailitambui ziwa nyasa hata kidogo wala hailijui ziwa hilo liko wapi, bali wao wanalitambua na wnawafundisha watoto wao tangu wamepata uhuru kuwa kuna ziwa Malawi.

Lakini Mungi, hivi ulitaka serikali ya Tanzania ikae kimya dhidi ya chokochoko za Malawi na Rwanda?, Hivi ushauri alioutoa JK juu ya kagame kuzungumza na waasi ni kosa? Hivi dharau alizoonyesha Kagame dhidi ya nchi (JK) yetu ni sawa? Au unataka kutuambia kuwa ni sawa na haki sisi kudharauliwa na kuingiliwa mipaka yetu na nchi jirani kuliko sisi kurespond dhidi ya dharau zao na chokochoko zao?

Kwa ushauri tu, hili suala la Malawi na Rwanda tuondoe tofauti za kisiasa na tuubebe uzalendo kwa pamoja kwa kumuunga mkono JK na kuwaonyesha hao mahafidhina kuwa sisi sio wapole hata kidogo, bali tumekomaa kidplomasia.

Sipingani na hilo mkuu, ndiyo maana kwenye bandiko langu la pili nilisema kwa suala la Malawi ni sawa kama yupo kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa.
Kinachonishawishi niseme hivyo ni kitendo cha yeye kukaa kimya huku anashikwa kalio na hawa jamaa wawili, tena kwa udhaifu na uzembe uliotukuka.
Tatizo la usalama wa nchi kwa maana ya jeshi la wananchi na polisi badala ya ku concentrate maslahi ya nchi, wao wanakuwa wame concentrate kuwashughulikia CHADEMA.
Kuna wapumbavu humu wamesema kwa suala la Maslahi ya nchi Kikwete hajakosea, lakini wanakuwa wavivu wa kuunganisha dots ya kwanini Kikwete amekuwa chanzo cha serikali yake kuwa na maadui wengi ndani na nje.
Kikwete ni Rais dhaifu nchi hii tokea ipate uhuru wa bendera hatajawahi kuwa na kiongozi wa namna hii.
 
Asante mkuu,ni watu smart wachache tu wanaona hilo.Hotuba yake imeonyesha kuwatisha majirani wote.Tunakwenda wapi.kwa nini hiyo bajeti ya vita hisiende kwenye kilimo na mashuleni,na afya?.Kumbe serikali ina pesa alafu wanadai hawana pesa.hiyo bajeji ya vita imetoka wapi?.Hatutaki vita tutakaa meza moja na majirani zetu na kuongea tu.kwani sisi ni ndugu.Wananchi wa pande zote hawataki vita.Ila mkuu wetu anaonyesha ana ugomvi na Kagame,na sasa unaonekana unasambaa kwa majirani wengine.
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

unaonyesha labda umri wako ni mdogo na huna historia ndefu kuhusu huu mgogoro wa ziwa nyasa, mwishoni mwa miaka ya 1960s kamuzu banda aliyekuwa rais wa malawi alileta chokochoko hizi za kumiliki hili ziwa lote nadhani tanzania wakati chini ya baba wa taifa ilitoa kibano fulani,tangia wakati huo tumeishi vizuri na malawi kwa kumiliki ziwa nusu kwa nusu, nadhani huyu joyce ana dna za banda anataka kibano kidogo, hata kama wewe ungekuwa rais ungekubali tu ziwa liende kwa kuogopa uadui!!!kumbuka jk ameapa kulinda nchi hii na mipaka yake!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom