Malawi paper calls Kikwete a 'Bloodthirsty Leader'

Malawi paper calls Kikwete a 'Bloodthirsty Leader'

Status
Not open for further replies.
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

kwenye national issues wenzenu huwa wanaweka tofauti zao za kimaslah ya siasa pembeni_na ndio maana umeona jinsi walivyo pamoja mpaka media_ninyi na u.b.w.e.g.e wenu na media za uchwara mnazikashifu jitahada za taifa_kwa mfano wewe unaona kosa la Rais ni lipi? Rais asingesema ingefuta hoja ya malawi kuwa ziwa lipo kwao? tusingeenda Congo_wakimbiz wasingekuja TZ? madhara ya wakimbiz unayajua? au simply unakula na kunya basi unadhan unayo haki ya kuropoka? achen ufara
 
Tukiwa wakweli inatupasa tuzungumze na Malawi kwa amani maana kisheria hatuna haki. Nguvu za jeshi pia hazitatupa haki maana ingekuwa hivyo marekani angevamia majirani wake wote
 
i want to witness the way TPDF taught madam Banda self discipline and respect ...
 
Nadhani NYASA TIMES hawakutafsiri hotuba ya JK in its context. JK alisema hayo akiwa Kagera, tena Biharamulo na Ngara ambako kumekuwa na matukio ya ujambazi. Lakini piam haya ni maeneo yaliyopakana na Rwanda, ambapo siku chache Kagame alitishia kumpiga kikwete. That is why Kikwete alichagua kutoa kauli hiyo akiwa Mkoani kagera, mkoa unaopakana na Rwanda. Malawi wangetishika kama kikwete angetoa kauli hiyo akiwa Ikulu. Lakini pia JK was very specific: kuwa operation ni Kigoma, Geita na Kagera!

Kwa habari ya Malawi, Kikwete amewahi kusema yeye kama hamili jeshi mkuu, hana mpango wa vita na Malawi, licha ya Malawi kutoa matamko ya kuudhi sana.

Lakini pia sioni ajabu iko wapi: Wajibu mkuu mmojawapo wa mkuu wa Nchi ni kulinda mipaka ya nchi yake. Malawi wao wamesema wamejiandaa, tena kuwa mkuu wao wa majeshi amewahakikishia Wamalawi usalama wao. Hiyo ndio kazi yake.

Naona NYASA TIMES ni mchechezi wa vita, na nadhani ni kukosa uelewa kwa sababu vita ikipigwa hata hiyo rasilimali watakula wauza silaha.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

Mungi; Kwa hili sidhani kama Kikwete ana makosa. Tumseme kwa mengine mengi ambayo kathibitika kuwa na udhaifu lakini hili la Malawi na Rwanda ni lazima kama jemadari mkuu aonyeshe kuwa anaongoza na kuilinda nchi yetu.
 
Wee endelea kama unavyoamini lakini elewa sie tumekuwa watu wa kuhamisha pesa zetu kifisadi na kuweka huko Uswizi na kusahau kuimarisha jeshi letu, na pale tunapoliimarisha basi 10% ni za kufa mtu sio ten tena bali ni 50% ...angalia hata hao wanyarwanda wana expenditure kubwa jeshini kuliko inchi kubwa Tanzania

Rwanda
Military expenditures:
2.9% of GDP (2006 est.) (Tanzania 0.2%)
country comparison to the world: 47
[see also: Military expenditures country ranks ]



Mkuu hyo 2.9 % inaweza kuwa ni ndogo sana kwa 0.2% ya kwetu, sababu GDP ya Tanzania haiwezi kulingana na GDP ya Rwanda, Na hizo percent ni percent za GDP.
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

Acha chuki binafsi wewe. Mgogoro wa Ziwa Nyasa ulianza tangu enzi za Mwl. Usipotoshe Umma.
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.
Kwa sababu unamatatizo ya kufikiri ndiyo maana unasema haya usemayo.
 
Tukiwa wakweli inatupasa tuzungumze na Malawi kwa amani maana kisheria hatuna haki. Nguvu za jeshi pia hazitatupa haki maana ingekuwa hivyo marekani angevamia majirani wake wote
Hakuna mtu anayekataa mazungumzo tena sisi ndiyo tunatafuta mazungumzo malawi wanadengua hatimaye wanaishia kutoa maneno kipumbavu hawa watu hawana jema.
 
Waache Hao malawi wanakihoro..huyu kagame ataki wale wakimbizi walikimbilia DRC warudi kwao Rwanda ndo maana anawa support m23..waache watutafute watatupata tu..huyo mama wa malawi alibahatisha madaraka..tutawanyoosha

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hivyo viinchi vidogo, vikija hapa tunapiga, hatubakizi hata kitu, na mtu yeyote anaebeza kile kikwete amesema, ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine, kwenye mambo ya kitaifa kama haya we should stand as one. Mtu unaleta fact za Expenditure za jeshi in respect to GDP, haujui kuwa hyo inayegemea na ukubwa wa hyo GDP. Majeshi yetu ni imara. Na hakuna cha kutufanya tushindwe kuwapiga hao majirani wanaoleta *****. Najivunia utanzania.
 
Hii balaa sasa. Hili ndio tatizo la viongozi wa Tanzania kutoa kauli za kibabe kwa kila jambo. Wamezoea ubabe ndani kwa vyamba vya upinzani sasa wanafikiri hata kimataifa wanaweza kufanya hivyo. Never underestimate Malawi. Tunaweza tikachapwa hapa kama watoto wadogo. We should not take for granted kuwa tutaipiga Malawi kama tulivyoipiga Uganda.

Wakati ule tulikuwa na uongozi imara, umoja, mshikamano na jeshi imara. Sasa hivi tuna uongozi dhaifu, mshikamano umepungua, umoja nao ni dhaifu na jeshi letu sio kama lile la wakati ule. Hili la sasa umaarufu wake ni kupiga raia hovyo(Refer Mtwara na sehemu nyingine uraiani) litaweza kuikabili nchi yoyote kivita Vita sio ukubwa wa nchi bali ni sayansi na teknologia. Membe, Lowassa na Kikwete wote ukiwasikiliza ni kama wamejiandaa kwenda vitani. Kama wanataka vita waende wao.

Vita ya Uganda tuliambiwa tufunge mikanda mpaka leo tunateseka hakuna wa kutuambia tufungue mikanda badala yake tunaambiwa tukaze zaidi kwa kuongeza kodi kwenye laini za simu. Tumekaza mpaka tundu la mwisho sasa inabidi kutoboa tundu jingine la kodi za laini za simu. Wakati sisi tunataka kukatika viuno, viongozi wanalegeza mikanda kwa raha zao mpaka inabidi waitoe kabisa.

Membe, Lowassa na Kikwete acheni kauli za kutishiana vita ma majirani ninyi hamtaathirika na vita! Rwanda na Malawi sio nchi za kuzidharau!
 
Kikwete amesababisha Tanzania iwe na ugomvi na jirani zake Malawi na Rwanda.

Kwa mara ya kwanza tumekuwa na maadui dhidi ya jirani zetu.

Mungi, unaweza kuniambia kosa la Kikwete liko wapi? Je, unakubaliana na mameno ya yule mwanamke wa Malawi kuwa Ziwa Nyasa lote ni lake? Je, ungekuwa wewe ungekaa kimya?
Je, unakubaliana na matusi ya Kagame na Mawaziri wake, eti kwasababu Kikwete katoa ushauri? au kapeleka maheshi Kongo, kwani Kongo vipo vikosi vya TZ peke yake?
 
Seems absurd, doesn't it? Tanzania should restore lake Nyasa, no matter at what cost even though it may temporarily embarrass the economy of the country!
 
Mkuu tusiwapotoshe wanajamvi kwa uvivu tu wa kusoma na kufanya research. Kwanza kabisa lazima uelewe uwezo wa kijeshi au military strength wa nchi huwa unaangaliwa kwa kuchukua vigezo vingi na si kuangalia kigezo kimoja au viwili tu. Hiyo percentage of GDP uliyoweka ni sehemu moja tu kati ya vitu karibia kumi vya kuangalia ili ujue nchi moja inaizidi military strength nchi nyingine. TATU,data za GDP ulizotumia ni za mwaka 2005 na wamekuambia ni estimation tu. Je unajuaje kama kila nchi imefanya update zipi mpaka kufikia hii mwaka 2013?. Ndio maana kwenye research wanakuambia ukiona una andiko au kitabu cha kufanya reference cha mwaka 2005 basi jitahidi utafute andiko la karibuni i.e at least year 2010. SASA BASI: Kwa mujibu wa Report ya Mwaka 2013 ya taasisi ya Stockholm International Peace Research Institute(Yearbook 2013), msimamo/rank kwa kigezo cha world rank,amount spent na %GDP kwenye mabano ni hivi: Kenya (78)(Usd 594000,000)(2.0%),Uganda(95),(Usd 276,000,000)(1.8%),Tanzania(103),(Usd 217,000,000),(1.1%),Rwanda (125),(Usd 77,200,000),(1.4%),Burundi(137) (Usd 46,900,000)(3.8%). Sasa, tazama nyingine chache za nje kidogo ya EAC: Malawi (136)(Usd 48,600,000)(1.2%),DRC (110) (Usd 163,000,000) (1.0), Seycheles (154)Usd 6,600,000) (1.2%). Nimekuwekea figure hizo ili uelewe kidogo kwamba military strength haiangaliwi kwa kigezo kimoja tu. Mfano, kwa kutumia kigezo cha amount spent nchi inayoongoza kwa Africa ni Algeria(29 in world ranks) (Usd 5,586,000,000) but has %GDP 3.8 equivalent to Burundi!. Also Malawi %GDP is 1.2 which is equal to that of Sycheles,does it mean Malawi military strength equal to that of Sycheles?.
Kumalizia ni kwamba,uwezo wa kijeshi wa nchi unapimwa kwa vigezo au parameters nyingi na si tu unatumia kiasi gani cha GDP yako. Je kama hiyo %kubwa unayojivuna kutumia unawalipa askari tu na haununui zana imara itakusaidia nini. Mfano mdogo ni Vita vya Kagera ambapo Iddi Amini kwa kusaidiana na Ghadafi walikuwa na zana za kisasa kuliko Tanzania. Lakini askari wao hawakuwa na ujuzi mkubwawa kutumia zana mbalimbali na pia hawakuwa na nidhamu. Matokeo yake unayajua.Au kama country yako iko vurnerable due to geographic position,weather,small population,number of able and active military personel etc bado hiyo %GDP spent itakuwa kigezo kimojawapo kidogo tu cha nguvu ya kijeshi.
(
Hawa jamaa kiukweli wamejitayarisha na tutapigwa...Kwanini??? compare and contrast on CIA figures

Tanzania Military expenditure
Military expenditures:
0.2% of GDP (2005 est.)
country comparison to the world: 169
[see also: Military expenditures country ranks ]

Malawi Military Expenditure
Military expenditures:
1.3% of GDP (2006)
country comparison to the world:
112
[see also: Military expenditures country ranks ]


 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom