Malalamiko ya Wananchi kuhusu mabadiliko na gharama za vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo mwaka 2021

Mimi Nina lain za mitandao minne tofaut huwa ninahama kutafuta unafuu mwanzo huwa ofa zao ni nzuri ila nikitumia lain zao kwa miez miwili wananifutia ofa zote na kubaki na vifurush vya gharama kubwa naona ndo mbinu zao
 
Halotel wako vizuri shida ni coverage yao ni ndogo ukilinganisha na hao KALIO icho ndo kinachowapa jeuri
 
Nimwhamia halotel, Yaani 100,00/= Tigo walikuwa wanatoa gb 7. Kwa mwezi . Wamebadilisha kutoka gb 7 mpaka 2.5 . Hela hiyo hiyo 100,00/=. Kweli hapa kuna uhalali upi. Napenda kasi ya mtandao wa Tigo but for now let me switch to another side .
 
Nina laini za mitandao yote inayopatikana kwenye mazingira yangu lakini cha ajabu nazunguka tu humohumo hakuna mwenye nafuu

TTCL walikuja moto ila ikawa kifurushi hakifanyi kazi mpaka kinaexpire (yaani ukituma sms haiendi au unafungua data internet haifunction labda kwa mara chache tu)

Zantel nao wako vizuri lakini dakika unaweza kushangaa tu paap! zimeisha. saa zingine una kifurushi ila wanakata vocha yako bila sababu na ukipiga customer care unakutana na majibu yaleyale ya kukaririshwa darasani

Airtel kwa kachenji kadogo ti utapata bonge la kifurushi (hasa internet) ila ndo utajua mwenyewe utaenda kuipata wapi access ya mtandao

Tigo ndo hata sijui nianzie wapi maana kila uozo ni wao. Kifurushi cha kawaida kabisa lakini kinagawanywa dk nyingine kwa ajili ya usiku tu (yaani unalazimishwa kupiga simu usiku) wakati hii tumezoea inawekwa kwenye vifurushi vile vingine vya ziada kama ofa nk

Halotel nao ndo walewale

Voda kama kawaida yao wao ni wazee wa ghali

Basi nimejikuta nahama mtandao fulani kwa muda tu mara huko kwingine wakileta ujinga nakuja kuurudia tena.

Lakini kuna mtandao mmoja katika hiyo nimeapa sitakaa nije kurudi tena!
 
Dah kazi tunayo mana maisha yetu bila simu hayaendi,
Na ukijaribu kujikwamua angalau vocha ya book upate muda wa mahongezi anglau na sms na na mb kidogo, majibu utakayopata hutarudia mtandao huo tena, Lakin wote sawa ila TIGO sitarudia tena na tena...
 
Airtel wale wenye laini za 4g kwa kutumia uni ofa tunakula bata namna hii
IMG_20210129_101550.jpg
 
Tigo tuachane nao moja kwa moja maana gakuna faida ya kuishi na asiyejua thamani yako kama mteja.
 
Mimi hali inayo ni kwaza na kunikirihisha ,ni hii ya kununua kifurush na kupangiwa sijui dakika kumi za longa nae ,mara usiku kuanzia saa NNE, huu ni upuuzi ,kwanini tupangiane na thamani ya kifurushi chenu mlioieka nimelipa ,napaswa kutumia nitakavyo
 
Kwanza mtandao wao hii ni wiki ya pili unasumbua sana na hawajasema chochote kwa wateja wao.

Pili, ni kuongeza gharama kwenye vifurushi vyao. Hapo mwanzo walikuwa wakinipa GB 2 kwa Tsh 3000 kwa wiki sasa umekuwa nu GB 1 tu
 
Back
Top Bottom