Enigmatic_
Member
- May 12, 2023
- 16
- 13
Sio mbali sana. Ni miaka mitatu kurudi nyuma bei za vifurushi vya intaneti ilikuwa ya kawaida sana. Kwa 1000 mtu angeweza kupata kifurushi cha GB1 kwa wiki. Leo hii, GB1 ni 3000.
Hebu fikiria kwa sasa, ni watu wangapi wameathirika na mabadiliko hayo? Mimi kipindi hicho, kulingana na bei kuwa rafiki, nilipata wasaa mzuri wa kusoma online courses mbalimbali. Lakini kwa sasa imekuwa vigumu. Siwezi kumudu gharama!
Kuna watu wanatengeneza pesa kupitia mtandao. Bloggers na youtubers wanategemea site visitors/viewers ili walipwe. Sasa gharama za vifurushi zinapokuwa juu maana yake automatically watazamaji wanapungua.
Serikali, kwa upande wake ni kama imeziba masikio. Danadana haziishi. Mwaka jana Rais aliagiza bei ziangaliwe lakini sijui hili jambo liliishia wapi.
Hili jambo, kwa upande wangu, naona ni kama njia ya kuzuia uhuru wa kutoa na kupata taarifa, Kitu ambacho ni kinyume na katiba yetu!