Makulumbembe gani humtisha kila rais anayetaka kuandika katiba mpya na kumfanya aonekane hayawani?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Hili la Samia kurukaruka kama maharage ya Mbeya kuhusu kuandika katiba mpya, kinyume kabisa na dhamira yake ya awali, siyo jambo geni kutokea. Likitokea pia chini ya utawala wa Kikwete mwaka 2014.

Rais Kikwete alikuwa na nia ya dhati kabisa ya kuwaachia watanzania katiba mpya. Akaanzisha mchakato uliotumia fedha nyingi Sana, lkn dakika za mwisho kabisa Kikwete akaanza kuongea kama hayawani baada ya makulumbembe kumtisha na kumtoa kwenye reli. Pesa zetu zikapotea.

Amekuja huyu mama amenzisha kikosi kazi cha bara, akanzisha na kikos kazi cha visiwani, makulumbembe yanamwangalia tu, ili yajiridhishe kama amedhamiria kweli ama la.

Yalipoona amepokea mapendekezi ya vikosi kazi hivyo viwili pamoja na yale ya Chadema makulumbembe yakaona kumbe yuko serious juu ya suala la katiba. Yakamvagaa mama wa watu Kisha yakamtisha na kumuondoa kwenye lengo.

Jana akaanza kubwata kama mtoto mdogo. Eti yatupasa kuwaelimisha watu wote wajue katiba ya nchi ndipo tuandike mpya . Hata hakuelweka alikuwa anaongea nn. Unaona kabisa mwili na maneno yaliyokuwa yakimtoka kinywani vinagombana. U aina kabisa huyu katishwa.

Haya makulumbembe ni akina nani? Kwann yana nguvu kuliko taasisi ya urais?

Usijidanganye kwa kusema ni deep state. Hapana. Na kama ni wao basi tuna deep state uchwara inayolinda maslahi ya ccm na siyo maslahi ya nchi. Kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi.
 
Back
Top Bottom