Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Mola anaumba kwa ukamilifu,huko unakofikiri wewe si ukamilifu ndio maana Allah akaumba mambo mengi kwa uwili.

Yaani ukiambiwa Mola ni mbora wa kuumba ndio hivi sasa.

Ameleta ugonjwa na akaleta na dawa,akaleta huzuni halikadhalika akaleta raha.

Akaleta usiku na kadhalika mchana. Sasa ukiwa unafikiri kwa kuhisi udhaifu bali fikiri kwa kinyume chake,kwani ukweli uko ndani yako kama ukiwa wewe ni mpembuzi wa mambo kweli kweli.
Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Unahubiri.
 
Wapi umethibitisha?

Wweka link hapa tujadili uthibitisho wako.
Huu utoto ndio huwa siupendi bro,usicheze na akili za watu.

Mimi nimewahi kukuthibitishia na muda wowote naweza kukuthibitishia.

Suala la kuleta link sina elimu nalo na muda huo sina. Ndio maana niliwahi kuweka masharti hapa ili tukubaliane usije kuleta uhuni kama huu unao uleta sasa hivi.

Niliweka masharti ili kudhibiti maneno.

Sasa narudia tena leo kwa mara ya mwisho bro,na sitarudia tena baada ya leo hii.

Tuweke masharti ya kujadiliana kuhusu suala hili.

Mimi niwe nathibitisha uwepo wa Mola mlezi na wewe uthibitishe kutokwepo kwake ?

Tuanze kaka.
 
Kaka tuweke masharti ili tudhibiti mjadala usikimbie maswali kaka mkubwa.
Sharti moja la mjadala ni kujibu maswali. Hata kama jibu ni "sijui jibu" tu.

Wewe nakuuliza maswali, badala ya kujibu, unahubiri.

Hatuwezi kuwa na mjadala hapo.
 
Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Unahubiri.
Yafuatayo ndio masharti yangu.

1. Tukubaliane kuhusu rejea.

Yaani katika mjadala huu nataka tukubaliane rejea za kuegemea kutoka kwenye vitabu. Hapa namaanisha mimi marejeo yangu ni vitabu vya kiimani na hoja za kiakili.

Wewe niambie marejeo yako ni wapi katika kila hoja utakayokuwa unaitoa.

2. Lazima tujikite katika mada.

Hapa hakuna kuhama mada mpaka mada moja iishe.

3. Hakuna kukwepa maswali

Hakuna kwenda mbele mpaka swali uliloulizwa ulijibu.

4. Lugha

Hapa lazima zitumike lugha za staha na kuheshimiana.

5. Mifano

Lazima utoe mifano sawia.

6. Ukishindwa hoja

Hapa lazima ukiri wazi kabisa kama hojs imekushinda au la,ili tuepuke kupoteza muda.

Je wewe unakubaliana na masharti yangu haya ? Kama unapinga niambie ili tukubaliane kielimu.
 
Sharti moja la mjadala ni kujibu maswali. Hata kama jibu ni "sijui jibu" tu.

Wewe nakuuliza maswali, badala ya kujibu, unahubiri.

Hatuwezi kuwa na mjadala hapo.
Nimekuwekea masharti hapo yasome kwanza ili tuingie kwenye mjadala.
 
First things firts. Kwani wapi tulikuwa hatujakubaliana kuhusu rejea?

Kuna mahali nilikukataza kutumia rejea yoyote?
Bro usipoteze muda,nani amesema hivyo ?

Ninapoweka masharti ujue naweka utaratibu mzuri endapo tukiuka tunakumbushana kurudi katikaasharti ili mjadala uende vyema,hapa haijalishi ilisemwa huko nyuma au la !

Soma masharti yangu useme kama kuna sharti unalikataa ili tujadili mada kielimu kuliko kupoteza muda.
 
Hiyo si sababu.

Hapo umekubali hujui sababu.

Hujui sababu kwa sababu hakuna sababu.

Hakuna sababu kwa sababu Mungu huyo hayupo.

Mungu huyo hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe kwa sababu upande mmoja ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, na upande mwingine kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Hivyo hawezi kuwepo katika uhalisi.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
Haya ndio niliyoysema jana kuwa hatuwezi kujadili. Ona sasa unaniuliza masuala ya kuhusu Mungu nakujibu unakataa jibu kwa kusema Mungu hayupo,kwahiyo lolote ambalo ningejibu usingelikubali hata iweje.

Ndiyo maana mie nataka ueleze ni vp hakuna Mungu? ila matokeo yake unakimbilia kujadili masuala ya upendo wa Mungu na ndiyo maana yanatokea haya.
 
Mungu na akusamehe, binadamu anawezaje kuhukumu, tena kumhukumu muumba wake "MUNGU", uhuru, utashi na neema ya Mungu tuitumie vizuri kwa kweli.
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?
 
Bro usipoteze muda,nani amesema hivyo ?

Ninapoweka masharti ujue naweka utaratibu mzuri endapo tukiuka tunakumbushana kurudi katikaasharti ili mjadala uende vyema,hapa haijalishi ilisemwa huko nyuma au la !

Soma masharti yangu useme kama kuna sharti unalikataa ili tujadili mada kielimu kuliko kupoteza muda.
Unaweka masharti ambayo hayahitajiki.

Hakuna mtu aliyekuzuia kurejea kitabu chochote, sasa sharti la kutaka turejee vitabu lina tija gani?

Na kurejea vitabu unakuwekea sharti kwa minajili gani?

Kwamba ukiniletea aya ya Quran haipingiki kwa sababu ni ya Quran?
 
Haya ndio niliyoysema jana kuwa hatuwezi kujadili. Ona sasa unaniuliza masuala ya kuhusu Mungu nakujibu unakataa jibu kwa kusema Mungu hayupo,kwahiyo lolote ambalo ningejibu usingelikubali hata iweje.

Ndiyo maana mie nataka ueleze ni vp hakuna Mungu? ila matokeo yake unakimbilia kujadili masuala ya upendo wa Mungu na ndiyo maana yanatokea haya.
Hujajibu swali.

Umekubali kwamba hujui jibu la swali.
 
Narejea namba2.Hata YESU,MUSSA,IBRAHIM,NUHU MOHAMEDI hawakumuona mungu kwa macho sembuse wewe?Charmilton lazima utakuwa msomi mzuri wa falsafa mada yako inafikirisha.Ila nina wasiwasi ilikuwa uwe padre au shehe wito ukagoma
 
Hoja hupingwa kwa hoja, thibitisha kutokuwepo kwake kwa kuwa pasi na shaka umekili kwamba nimedhihirisha ya kwamba MUNGU yupo.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeuumba ulimwengu huu, hayupo. Ni dhana potofu tu.

Ni dhana potofu kwa sababu ina contradiction. Contradiction ni kitu kujipinga chenyewe kwa namna ambayo haiwezekaniki kuwa katika uhalisi wa ukweli. Mathalani, nikisema pembetatu haiwezi kuwa duara na duara haliwezi kuwa pembetatu katika Euclidean geometry, halafu nikasema kuna pembetatu ambayo ni duara hapo hapo, katika Euclidean geometry, pembetatu hiyo ambayo ni duara hapo hapo haiwezi kuwepo, dhana ya kuwepo kwa hiyo pembetatu ambayo hapo hapo ni duara ina contradiction. Hivyo pembetatu duara hiyo haiwezi kuwepo.

Mungu naye ni kama pembetatu duara.

Upande mmoja tunaambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote (pembetatu). Upande mwingine tunaambiwa kauumba ulimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya, licha ya ujuzi wake wote, uwezo wake wote na upendo wake wote (duara).

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea? Ulimwengiu huo ungekuwa logically consistent na upendo wake. Usingekuwa na contradiction.

Huu ulimwengu tunaouona, ambao mabaya yanaweza kutokea, unam contradict huyo Mungu.

Kuamini Mungu huyo yupo, ni sawa na kuamini kwamba kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara katika Euclidean geometry planes.

Haipo, haiwezi kuwepo, kwa sababu ina an inherrent contradiction.

Mungu huyo naye hayupo kama hiyo pembetatu duara.

Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina an inherrent contradiction.
 
Unamlaumu asiyekuwepo? Anyways, Mtume Paulo aliyuhasa kutokuwa na mabishano ya kipumbavu hususan juu ya mambo ya kiroho, "mabishano". Kila lakheri.
 
Unaweka masharti ambayo hayahitajiki.

Hakuna mtu aliyekuzuia kurejea kitabu chochote, sasa sharti la kutaka turejee vitabu lina tija gani?

Na kurejea vitabu unakuwekea sharti kwa minajili gani?

Kwamba ukiniletea aya ya Quran haipingiki kwa sababu ni ya Quran?
Bro usiwe mjinga kiasi hicho na usipende kupoteza muda,nimeweka masharti ili tukubaliane. Wewe kama huyaafiki sema sharti hili silikubali kwa sababu hii na hii,weka sharti hili. Hivi ndio wanaume tunavyo yajadili mambo.

Sasa ukileta ujinga katika mambo ya msingi unazidi kukosea sana.

Jaribu kuwa na tabia za kielimu bro mbona rahisi sana.

Sasa ukitaka kuleta mada kabla ya mada husika huu ni upumbavu wa kujitakia.
 
Narejea namba2.Hata YESU,MUSSA,IBRAHIM,NUHU MOHAMEDI hawakumuona mungu kwa macho sembuse wewe?Charmilton lazima utakuwa msomi mzuri wa falsafa mada yako inafikirisha.Ila nina wasiwasi ilikuwa uwe padre au shehe wito ukagoma
Hawezi kuwa shekhe sababu sisi kwetu falsafa ni haramu.
 
Bro usiwe mjinga kiasi hicho na usipende kupoteza muda,nimeweka masharti ili tukubaliane. Wewe kama huyaafiki sema sharti hili silikubali kwa sababu hii na hii,weka sharti hili. Hivi ndio wanaume tunavyo yajadili mambo.

Sasa ukileta ujinga katika mambo ya msingi unazidi kukosea sana.

Jaribu kuwa na tabia za kielimu bro mbona rahisi sana.

Sasa ukitaka kuleta mada kabla ya mada husika huu ni upumbavu wa kujitakia.
Sasa nayajadili masharti, ili niyaelewe vizuri, nijue ninapoyakubali nakubali nini, na ninapokataa, ninakataa nini, unaniita mjinga?

Mimi kutaka kuyaelewa masharti kabla ya kuyakubali au kuyakataa ni ujinga?

Unategemea niyakubali au kuyakata masharti ambayo siyaelewi?

Huo ndio ujanja?

Hapa kati yangu mimi na wewe nani mjinga?
 
Back
Top Bottom