Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Sasa kilichokutuma kutaja elimu yako ya Marekani ni kitu gani??.

Ungeniambia ulipata hiyo A+ hapa bongo labda ningekubali "uongo" wako huo kwa mbali sana, lakini huko The US "it is even very flabagasting issue".

Kamwe huwezi kumkana Mungu ukawa salama, mbaya zaidi unamkana Mungu ndani ya kadamnasi ya takriban watu 400,000, na unawashawishi wakubali uongo wako bila woga na haya eti, Prof, wako wa falsafa "alikuzawadia" A+ kwa kutoa hoja zilizokonga moyo wake na akasema fikra zako ziko juu ya fikra zao na hivyo hakukua na haja ya kufanya mtihani wa falsafa!!!??[emoji16][emoji16][emoji16],Kiranga hilo darasa ulikuwa unasoma peke yako??, wewe upewe an A+credit wenzako wawe kimya[emoji16][emoji16][emoji16], tena katika moja ya American university/college na wanafunzi wa kizungu wapo!!, huyo prof, hataki kazi??,


Kiranga, mimi sikuelewi hili jambo halijakaa sawa unatakiwa ujisafishe kwanza na jambo hilo.

And do not lose temper ukaanza kutukana ujue umesema unaye mke na watoto na usitake tuamini kama "you behaves the same while at your home with your wife and kids."

Halafu kumbe ulisoma "culculus", ni advanced au ordinary?? na ulisomea huko huko The US au ulipokuwa bongo ??, labda nikitumia "integration" utajua kuwa Mungu yupo[emoji16][emoji16].
Thibitisha Mungu yupo.
 
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao magonjwa yanaweza kuwepo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao magonjwa hayawezi kuwepo?
Kwa sababu yeye ndiye mwenye ujuzi wote na hivyo ni yeye ndiye mwenye kujua zaidi hekima ya kuumba au kufanya hivyo.
 
Kwa sababu yeye ndiye mwenye ujuzi wote na hivyo ni yeye ndiye mwenye kujua zaidi hekima ya kuumba au kufanya hivyo.
Hiyo si sababu.

Hapo umekubali hujui sababu.

Hujui sababu kwa sababu hakuna sababu.

Hakuna sababu kwa sababu Mungu huyo hayupo.

Mungu huyo hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe kwa sababu upande mmoja ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, na upande mwingine kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Hivyo hawezi kuwepo katika uhalisi.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Watu povu za mdomo mimacho na misuli ya shingo imewatoka, eti, wanasema:- "thibitisha kama Mungu yupo!!"

Hiyo Misuli na midomo na mimacho wanayotumia kumkanusha huyo Mungu utadhani walijiumbia wao wenyewe🤔🤔 na mbaya zaidi wanajaribu kutumia uongo wowote
wanaoupata kudanganya umma ili waonekane "they are brainy" kumbe wapo kaputi (cuput) kwa wenye akili na watiifu kwa Mungu mtukufu.

Hawana sababu zenye mashiko mbele ya wenye akili waliojaliwa na Mungu.
 
Mbwa anaweza kutambua muda si kwa kumuuliza si mbwa peke yake wanyama wote wanatambua muda au wewe hujawahi kufuga kuku jogoo Swalaaa yeye anawika huoni kama kajua kumekucha

Sasa wewe unataka kuuongelea muda gani ? Wakati kila mtu ana ufahamu muda kutokana anavyouelewa na anavyouona yeye mwenyewe
Bro naona unazidi kudhihirisha ujinga wako na udhaifu wako wa kushindwa kutofautisha mambo.

Nasubiri jibu la swali langu.

Mwenzako Kiranga alikiri wazi kabisa ya kuwa swali limemshinda hili.

Muulize mmbwa muda ni nini kama atakujibu. Msipende kupotezea watu muda kwa kauli za kitoto kama hizi.
 
Mbwa anaweza kutambua muda si kwa kumuuliza si mbwa peke yake wanyama wote wanatambua muda au wewe hujawahi kufuga kuku jogoo Swalaaa yeye anawika huoni kama kajua kumekucha

Sasa wewe unataka kuuongelea muda gani ? Wakati kila mtu ana ufahamu muda kutokana anavyouelewa na anavyouona yeye mwenyewe
Hivi nikiuliza kuhusu maji. Je kuna mtu au kiumbe kinaulewa tofauti na unavyoelewa wewe kuhusu maji ?

Mbona mnayakosea adabu maumbile kiasi hicho ?
 
Mbwa anaweza kutambua muda si kwa kumuuliza si mbwa peke yake wanyama wote wanatambua muda au wewe hujawahi kufuga kuku jogoo Swalaaa yeye anawika huoni kama kajua kumekucha

Sasa wewe unataka kuuongelea muda gani ? Wakati kila mtu ana ufahamu muda kutokana anavyouelewa na anavyouona yeye mwenyewe
Au mfano mwingine kuhusu kifo,hivi kuna maana nyingine ya kifo zaidi ya roho kutengana na mwili ?

Mnataka tuwaeleweshe vipi kuhusu suala la muda ili muweze kujibu ?

Mfano wa muda ni kama vile kifo,kadhalika maji.

Sasa ukibabatiza maneno naona wewe hauko kielimu bali kupotezeana muda tu.
 
Hakuna aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.
Mara ngapi bro,uthibitishiwe ?

Nataka nikufundishe namna ya kuthibitishe jambo.

Narudi...?! Kisha upime kwamba je hujathibitishiwa kama Mola mlezi yupo na ili upime wewe upande wako je umeshawahi kuthibitisha kutokuwepo kwake ?

Somo hili nilitaka nilitaka nilihudhurishe jana nikahisi hakuna haja. Ila comment yako hii inanishawishi kuleta somo hili.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Mungu na akusamehe, binadamu anawezaje kuhukumu, tena kumhukumu muumba wake "MUNGU", uhuru, utashi na neema ya Mungu tuitumie vizuri kwa kweli.
 
Mara ngapi bro,uthibitishiwe ?

Nataka nikufundishe namna ya kuthibitishe jambo.

Narudi...?! Kisha upime kwamba je hujathibitishiwa kama Mola mlezi yupo na ili upime wewe upande wako je umeshawahi kuthibitisha kutokuwepo kwake ?

Somo hili nilitaka nilitaka nilihudhurishe jana nikahisi hakuna haja. Ila comment yako hii inanishawishi kuleta somo hili.
Wapi umethibitisha?

Wweka link hapa tujadili uthibitisho wako.
 
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao magonjwa yanaweza kuwepo wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao magonjwa hayawezi kuwepo?
Mola anaumba kwa ukamilifu,huko unakofikiri wewe si ukamilifu ndio maana Allah akaumba mambo mengi kwa uwili.

Yaani ukiambiwa Mola ni mbora wa kuumba ndio hivi sasa.

Ameleta ugonjwa na akaleta na dawa,akaleta huzuni halikadhalika akaleta raha.

Akaleta usiku na kadhalika mchana. Sasa ukiwa unafikiri kwa kuhisi udhaifu bali fikiri kwa kinyume chake,kwani ukweli uko ndani yako kama ukiwa wewe ni mpembuzi wa mambo kweli kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom