Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

ukiwa hujui kitu ndo unaishia kauli kama hizo ''UNASIKITISHA KWELI'' ndo mwisho wa ufikiri wake yaani hata kujituma kuutuma ubongo uchakarike upate fahamu hataki kabisaa!!
Hapo kashapigwa kwa logic na fact sana, mpaka kakosa cha kuandika.
 
huw najiuliza kabla sijazaliwa Inamaana mungu alishajuwa kuwa nitazaliwa. baada ya kuzaliwa maisha yangu yooote ntakayoishi ameyajua 100% mimi muhusika siwezi kujua hata litakalo tokea baada ya dkk 2 mbele
Kiranga CHARMILTON
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Mshana Jr upooo? hebu tiririka hapa tuweze kupata neno huenda nawe tukajua uko upande upi hapa
cc: pascal mayalla
 
Ili iweje?

Mjadala ni njia ya kufika Kilimanjaro kutoka Dar, unauliza bei ya nguruwe China.

Kwa minajili gani?

Ukiambiwa bei ya nguruwe elfu tano au elfu kumi, haikusaidii kujua njia ya kwenda Kilimanjaro kutoka Dar.

Swali lako lina mantiki gani?

Nakuonesha kwamba swali lako ni hanithi, halina mantiki katika mjadala, halina mazao, halina watoto, jibu lolote nitakalokupa halita prove chochote katika mjadala.

Wwewe tatizo lako si tu huwezi kujibu maswali yangu, hujui hata maswali mazuri ya kuuliza katika mjadala huu!
"Mimi nipo duniani kwa sababu mama na baba yangu walikutana kimwili kibaiolojia katika muda ambapo niliwezekana kuwa conceived"

Hapo umesema kuwa sababu ya wewe kuwepo duniani ni kukutana kimwili baba na mama ako,sasa nimekuomba uthibitishe hilo kuwa ni kweli wazazi wako walijamiana.

Kama hauwezi kuthibitisha ila bado unasema walijamiana iweje akili hiyo hiyo ikatae kuwepo kwa Mungu kisa hakuna uthibitisho?
 
Watoto wa siku akili zenu......bora tu mshua wako hili bao angepiga punyeto tu akumwage bafuni huko uende kwenye karo la maji taka....
 
"Mimi nipo duniani kwa sababu mama na baba yangu walikutana kimwili kibaiolojia katika muda ambapo niliwezekana kuwa conceived"

Hapo umesema kuwa sababu ya wewe kuwepo duniani ni kukutana kimwili baba na mama ako,sasa nimekuomba uthibitishe hilo kuwa ni kweli wazazi wako walijamiana.

Kama hauwezi kuthibitisha ila bado unasema walijamiana iweje akili hiyo hiyo ikatae kuwepo kwa Mungu kisa hakuna uthibitisho?
Unaelewa kwamba nikikwambia siwezi kuthibitisha, kutoweza kwangu kuthibitisha hakuthibitishi kwamba Mungu yupo?

Unaelewa kwamba hujathibitisha Mungu yupo?
 
Nilishamjibu siwezi kuthibitisha ila bado anaendelea kuniambia nithibitishe.

Ungekuwa wewe ungefanyaje hebu nisaidie.
Hujaona muendelezo wa hoja, kwa sababu hutaki kuona.

Nimekwambia huwezi kuthibitisha Mungu yupo, kwa sababu hayupo.
 
Unaelewa kwamba nikikwambia siwezi kuthibitisha, kutoweza kwangu kuthibitisha hakuthibitishi kwamba Mungu yupo?

Unaelewa kwamba hujathibitisha Mungu yupo?
Yeah ni kweli kabisa kutoweza kwako kuthibitisha hakuthibitishi kuwa Mungu yupo ila kunatoa jibu la kwamba kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu hakufanyi kuwa hakuna Mungu.
 
Mungu hajawahi kukosea na haitatokea kukosea.
Kila analolifanya ni kwa makusudi kamili na huwa ana maana yake.
 
Sijui.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Angekuwepo sio tu kifo kisingekuwepo, hata wazo la kifo lisingekuwepo.
Mungu anasema kila kiumbe kitakufa,wewe hayo ya kusema Mungu hayupo kwa sababu ya kifo na kwamba angekuwepo kusingekuwa na kifo umeyatoa wapi? Thibitisha.
 
Yeah ni kweli kabisa kutoweza kwako kuthibitisha hakuthibitishi kuwa Mungu yupo ila kunatoa jibu la kwamba kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu hakufanyi kuwa hakuna Mungu.

Unanileta ninakotaka.

Ni kweli kwamba kushindwa kuthibitisha kitu hakufanyi kitu kisiwepo au kisiwe kweli.

Ila, ni kweli pia kwamba kitu ambacho hakipo, hakithibitishiki kuwa kipo, kwa sababu hakipo.

Mtoto wa miaka 15 anaweza kushindwa kuthibitisha kwamba baba yake mzazi, mwenye miaka 45, ni baba yake mzazi.

Kushindwa kwa huyu mtoto kuthibitisha kwamba baba yake mzazi ni baba yake mzazi, hakumfanyi baba yake mzazi asiwe baba yake mzazi.

Kwa hiyo, ni kweli, kushindwa kuthibitisha kitu tu, hakufanyi hicho ambacho hakijaweza kuthibitishwa kisiwe kweli.

Tatizo lako si tu umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo tu, umeshindwa kuondoa contradiction pia.

Unakuwa kama mtu mwenye miaka 45, anayesema kwamba mtoto wa miezi mitatu ndiye mama yake mzazi aliyemzaa.

Akaombwa uthibitisho, akashindwa.

Huyu si tu kashindwa kuthibitisha, kashindwa kuthibitisha na kashindwa kuondoa contradiction.

Sasa far and above kuthibitisha tu kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.

Fanya hivi.

1. Thibitisha yupo
2. Ondoa contradiction ya problem of evil. Kama Mungu huyo yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kuwepo, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo?
 
Mungu anasema kila kiumbe kitakufa,wewe hayo ya kusema Mungu hayupo kwa sababu ya kifo na kwamba angekuwepo kusingekuwa na kifo umeyatoa wapi? Thibitisha.
Awali ya yote, kabla ya kuandika "Mungu anasema..." thibitisha Mungu yupo.

Kama hayupo, hawezi kusema.

Atasemaje akiwa hayupo?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya na kifo.
 
Mimi nishasema Mungu hayupo, kwa hiyo habari zozote za Mungu kuwepo, waulizwe wanaosema yupo.
Unaposema kuwa Mungu mwenye upendo asingeumba ulimwengu wenye maovu,unajua kuwa hapo unazungumzia habari za uwepo wa Mungu?
 
Unaposema kuwa Mungu mwenye upendo asingeumba ulimwengu wenye maovu,unajua kuwa hapo unazungumzia habari za uwepo wa Mungu?

Hapana, nazungumzia habari za kutokuwepo kwa Mungu.

Mtu kaniuliza, dhambi inakuwepo vipi kama Mungu yupo na anayajua maisha ya huyo mtu mwanzo mpaka mwisho kabla huyo mtu hajazaliwa?

Mimi namjibu, namwambia mimi si mtu sahihi wa kuniuliza swali hilo, kwa sababu mimi sikubali Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom