Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Mtu anakwambia soma vizuri maandiko.

Unamkubalia maneno yake, unatafuta wataalam kabisa wa maandiko.

Unakutana na mtu kama James L Kugel, mtaalam wa masomo ya Biblia aliyefundisha mpaka Harvard.

Jamaa kaandika kitabu kabisa cha jinsi ya kusoma maandiko, kinaitwa "How To Read The Bible: A Guide To Scripture Then And Now".

Unamsoma, mtaalamu anakwambia Biblia imefutwafutwa na kubadilishwa badilishwa na watu mara nyingi tu, kwa sababu zao.
Ni kitabu cha historia na hadithi za Wayahudi tu.

Halafu unakuta huyo anayekwambia usome vizuri maandiko, hao wataalam hata hawajui.

James Kugel

howToReadTheBible.jpg

How to Read the Bible
A Guide to Scripture, Then and Now

READ AN EXCERPT

Scholars from different fields have joined forces to reexamine every aspect of the Hebrew Bible. Their research, carried out in universities and seminaries in Europe and America, has revolutionized our understanding of almost every chapter and verse. But have they killed the Bible in the process?

In How to Read the Bible, Harvard professor James Kugel leads the reader chapter by chapter through the “quiet revolution” of recent biblical scholarship, showing time and again how radically the interpretations of today’s researchers differ from what people have always thought. The story of Adam and Eve, it turns out, was not originally about the “Fall of Man,” but about the move from a primitive, hunter-gatherer society to a settled, agricultural one. As for the stories of Cain and Abel, Abraham and Sarah, and Jacob and Esau, these narratives were not, at their origin, about individual people at all but, rather, explanations of some feature of Israelite society as it existed centuries after these figures were said to have lived. Dinah was never raped — her story was created by an editor to solve a certain problem in Genesis. In the earliest version of the Exodus story, Moses probably did not divide the Red Sea in half; instead, the Egyptians perished in a storm at sea. Whatever the original Ten Commandments might have been, scholars are quite sure they were different from the ones we have today. What’s more, the people long supposed to have written various books of the Bible were not, in the current consensus, their real authors: David did not write the Psalms, Solomon did not write Proverbs or Ecclesiastes; indeed, there is scarcely a book in the Bible that is not the product of different, anonymous authors and editors working in different periods.

Such findings pose a serious problem for adherents of traditional, Bible-based faiths. Hiding from the discoveries of modern scholars seems dishonest, but accepting them means undermining much of the Bible’s reliability and authority as the word of God. What to do? In his search for a solution, Kugel leads the reader back to a group of ancient biblical interpreters who flourished at the end of the biblical period. Far from naïve, these interpreters consciously set out to depart from the original meaning of the Bible’s various stories, laws, and prophecies — and they, Kugel argues, hold the key to solving the dilemma of reading the Bible today.

How to Read the Bible is, quite simply, the best, most original book about the Bible in decades. It offers an unflinching, insider’s look at the work of today’s scholars, together with a sustained consideration of what the Bible was for most of its history — before the rise of modern scholarship. Readable, clear, often funny but deeply serious in its purpose, this is a book for Christians and Jews, believers and secularists alike. It offers nothing less than a whole new way of thinking about sacred Scripture.
Asante sana kwa maarifa mkuu, hicho kitabu naweza kipata?
 
Unasikitisha kwa kweli.
Bado hujathibitisha Mungu yupo.

Na zaidi, unatoa ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Wwewe kuweza kusikitika ni ushahidi Mungu hayupo.

Angekuwepo, isingewezekana kusikitika.

Masikitiko yasingekuwepo.
 
Swali lako ni irrelevant.

Kwa sababu mjadala ni uthibitisho wa kuwepo Mungu.

Nikisema naweza ku prove habari za wazazi wangu, hilo halithibitishi uwepo wa Mungu.

Nikisema siwezi ku prove habari za wazazi wangu, hilo halithibitishi uwepo wa Mungu.

Swali lako tunaliita swali hanithi.

Halizai watoto.

Halina maana.

Unaliona lina maana kwa sababu ya ufinyu wa mawazo yako tu.

Jaribu kuuliza maswali yanayozaa maana badala ya kuuliza maswali hanithi.
Unaweza kuthibitisha kuwa wazazi wako walijamiana??
 
Unaweza kuthibitisha kuwa wazazi wako walijamiana??

Unarudia maswali niliyokwishajibu
Huu udhia daktari kashautibu
Sasa nikupe tenzi na vina
Nikutoe uanagenzi kwa kina
Hili ni swali hanithi
Halibadili jedwali la hadithi
Nikisema siwezi, uwepo wa Mungu haliukwezi
Nikisema naweza, uwepo wa Mungu linaubeza
Kazi kwako dhihirisha
Mungu yupo? Thibitisha
 
Sijajibu swali au sijajibu swali kama unavyotaka wewe nijibu?

Nirejee nini kwenye swali? Naona hutaki jibu kwa sababu limekuja tofauti na ulivyotaka wewe tu.

Mungu angekuwepo, kungekuwa hakuna viumbe wenye uwezo mdogo kifikra kama Mbuzi na Chura na viumbe wengine waliowazidi hao uwezo.

Kuwepo kwa madaraja haya ni kukosa usawa katika viumbe, ni kukosa haki, kunaonesha kutokuwepo kwa Mungu.

Mtu kushindwa kujibu swali ni dalili ya kutokuwepo Mungu, Mungu angekuwepo, kila mtu angeweza kujibu kila sali analoweza kulifikiria.

Kwa sababu Mungu hayupo.Tofauti hii ni ukosefu wa haki, ndiyo maana wewe unaweza kumchinja mbuzi lakini mbuzi hawezi kukuchinja wewe.

Hilo linaonesha Mungu hayupo, angekuwepo, ulimwengu ungekuwa wa haki zaidi na wote tungekuwa na uwezo sawa.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.

Mimi nimeshindwa kukuthibitishia kawa Mungu yupo kulingana na unavyotaka wewe.

Lakini Mungu mwenyewe ambaye ninaamini yupo basi inshaallah anaijua njia atakayoweza kujithibitisha mwenyewe mbele yako, wewe umechukua njia mbaya ya kumkana mbele ya wana jf, naye atakapojidhirisha mbele yako nusura yako itakuwa kuja hapa jf na kumkubali hapa hadharani kama jinsi unavyo mkana hapa hadharani.

Let's it be suffice, tuko katika harakati za kujenga taifa hivi sasa.
 
Bado hujathibitisha Mungu yupo.

Na zaidi, unatoa ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Wwewe kuweza kusikitika ni ushahidi Mungu hayupo.

Angekuwepo, isingewezekana kusikitika.

Masikitiko yasingekuwepo.
Halafu hapo anakuja mtu na kukusifia kwa kuandika hicho ulichokiandika,ni wazi kabisa kuna watu watu wanakucheka kwa ujinga.
 
Halafu hapo anakuja mtu na kukusifia kwa kuandika hicho ulichokiandika,ni wazi kabisa kuna watu watu wanakucheka kwa ujinga.
Kama mimi ni mjinga, hilo pia linaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao unawezekana kuwa na viumbe wake wakiwa wajinga.

Hata tukikubali jitihada zako za kuonesha mimi ni mjinga zina ukweli, jitihada hizo zinaonesha Mungu hayupo.
 
Unarudia maswali niliyokwishajibu
Huu udhia daktari kashautibu
Sasa nikupe tenzi na vina
Nikutoe uanagenzi kwa kina
Hili ni swali hanithi
Halibadili jedwali la hadithi
Nikisema siwezi, uwepo wa Mungu haliukwezi
Nikisema naweza, uwepo wa Mungu linaubeza
Kazi kwako dhihirisha
Mungu yupo? Thibitisha
"Nikisema...." Hili sio jibu maana hapo sijajua kuwa unaweza au hauwezi,nataka jibu kuwa unaweza kuthibitisha kuwa ni kweli wazazi wako walijamiana?

Mie uliniuliza kama naweza kuthibitisha nikajibu siwezi,sikuleta longolongo.
 
Mimi nimeshindwa kukuthibitishia kawa Mungu yupo kulingana na unavyotaka wewe.

Lakini Mungu mwenyewe ambaye ninaamini yupo basi inshaallah anaijua njia atakayoweza kujithibitisha mwenyewe mbele yako, wewe umechukua njia mbaya ya kumkana mbele ya wana jf, naye atakapojidhirisha mbele yako nusura yako itakuwa kuja hapa jf na kumkubali hapa hadharani kama jinsi unavyo mkana hapa hadharani.

Let's it be suffice, tuko katika harakati za kujenga taifa hivi sasa.
Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
"Nikisema...." Hili sio jibu maana hapo sijajua kuwa unaweza au hauwezi,nataka jibu kuwa unaweza kuthibitisha kuwa ni kweli wazazi wako walijamiana?
Ili iweje?

Mjadala ni njia ya kufika Kilimanjaro kutoka Dar, unauliza bei ya nguruwe China.

Kwa minajili gani?

Ukiambiwa bei ya nguruwe elfu tano au elfu kumi, haikusaidii kujua njia ya kwenda Kilimanjaro kutoka Dar.

Swali lako lina mantiki gani?

Nakuonesha kwamba swali lako ni hanithi, halina mantiki katika mjadala, halina mazao, halina watoto, jibu lolote nitakalokupa halita prove chochote katika mjadala.

Wwewe tatizo lako si tu huwezi kujibu maswali yangu, hujui hata maswali mazuri ya kuuliza katika mjadala huu!
 
Ungeweka kwanza makosa yako ingekuwa vizuri.
ndio maana ameumbwa sio kosa lake
cc: CHARMILTON
huw najiuliza kabla sijazaliwa Inamaana mungu alishajuwa kuwa nitazaliwa. baada ya kuzaliwa maisha yangu yooote ntakayoishi ameyajua 100% mimi muhusika siwezi kujua hata litakalo tokea baada ya dkk 2 mbele
SWALI: SAMBI SANGU SINAKUJAJE HAPOO kama maisha yalishapangwa yawe/yapitie humo?
mkuu CHARMILTON hebu tusaidiane hili hapa mie nimekwama na kukosa mwelekeo
 
ndio maana ameumbwa sio kosa lake
cc: CHARMILTON
huw najiuliza kabla sijazaliwa Inamaana mungu alishajuwa kuwa nitazaliwa. baada ya kuzaliwa maisha yangu yooote ntakayoishi ameyajua 100% mimi muhusika siwezi kujua hata litakalo tokea baada ya dkk 2 mbele
SWALI: SAMBI SANGU SINAKUJAJE HAPOO kama maisha yalishapangwa yawe/yapitie humo?
Mungu hayupo.

Angekuwepo angeumba ulimwengu ambao dhambi haiwezi kuwepo.

Mungu kuumba ulimwengu ambao dhambi inaweza kuwepo ni biggest ungodly architectural blunder.

How could God make such a blunder?
 
Mimi nimeshindwa kukuthibitishia kawa Mungu yupo kulingana na unavyotaka wewe.

Lakini Mungu mwenyewe ambaye ninaamini yupo basi inshaallah anaijua njia atakayoweza kujithibitisha mwenyewe mbele yako, wewe umechukua njia mbaya ya kumkana mbele ya wana jf, naye atakapojidhirisha mbele yako nusura yako itakuwa kuja hapa jf na kumkubali hapa hadharani kama jinsi unavyo mkana hapa hadharani.

Let's it be suffice, tuko katika harakati za kujenga taifa hivi sasa.
eti kujenga Taifa
 
Kama mimi ni mjinga, hilo pia linaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumbaulimwengu ambao unawezekana kuwa na viumbe wake wakiwa wajinga.

Hata tukikubali jitihada zako za kuonesha mimi ni mjinga zina ukweli, jitihada hizo zinaonesha Mungu hayupo.
Cha kusikitisha hoja kama hizo ndiyo huitimishia kuwa hakuna Mungu na ndiyo maana wengine wanaona hatuwezi kujua uwepo au kutokuwepo kwa Mungu.
 
eti kujenga Taifa
Nilivyokuwa naanza kazi, kuna jamaa mmoja aliniambia "mdogo wangu, katika kazi yetu hii, mara zote kitu kikikushinda, usiseme "hiki kimenishinda", ni lazima uwe na "exit strategy".

Ushauri ule ulikuwa mbaya, unachochea mtu kutokubali kushindwa.

Ila nilipata somo zuri. Kwamba kuna watu huwa hawataki kukubali kwamba wameshindwa, wakishindwa wanatafuta "exit strategy".

Wwote hapa tuna shughuli, lakini huwezi kunisikia naaga kwa "exit strategy" ya kujenga taifa.

Kwa sababu hakuna anayemlazimisha mwingine post ijibiwe dakika hii hi.

Tunaenda "kujenga taifa", tunarudi, tunakuta quotes, tunajibu maswali. Tunaendelea na mijadala.

Bila kutaja habari za "kujenga taifa".

Ukiona mtu anaanza kutaja habari za "kujenga taifa", ujue ni exit strategy tu hiyo.
 
si uthibitishe ili umsaidie huyu aliyepotea
Hahaaa,

Kishiwa na majibu kabai "unasikitisha kweli".

Hajui hata yeye kuweza kusikitika ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Aangekuwepo, asingekuwa mkatili sana kiasi cha kuumba ulimwengu ambao masikitiko yanawezekana kuwepo.
 
ukiwa hujui kitu ndo unaishia kauli kama hizo ''UNASIKITISHA KWELI'' ndo mwisho wa ufikiri wake yaani hata kujituma kuutuma ubongo uchakarike upate fahamu hataki kabisaa!!
 
Back
Top Bottom