Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Poor interpretation, You lack the theological knowledge. Huna ushahidi wa kutosha kuthibitisha hoja zako
 
Magu alisema wale walioimba 'wana imani na nani sijui' angewatimua wote siku hiyo hiyo... Mimi nasema kama ningelikuwa Mungu pindi tu kidole chako kinabonyeza kitufe cha kupost hapo hapo ningekugeuza senene!!

Unafanya dhihaka kama hizi na bado uko hai! Aisee Mungu ana uvumilivu wa hali ya juu sana... Mwacheni Mungu aitwe Mungu!!

Hahahaaaaaaa...daaaah!
 
Kwanza unapaswa ujue kuwa mambo unayotuhumu kuwa ni Makosa ya Mungu ni kwasababu aidha huyajui na au hujajishughulisha kuyafahamu.
Mungu hakuumba na hajaumba kitu chochote kibaya au chenye mapungufu. Hata shetani aliyeumbwa na Mungu alikuwa mwema. Na jina lake halisi aliitwa Lucifer (Linatokana na neno Luchem lenye maana ya mwanga au kuangaza)

Mwenyezi Mungu amekupa akili na utashi ili uweze kutofautisha mema na mabaya katika kufanya maamuzi huru. Maamuzi ambayo yeye hakuingilii, japo atakushauri tu kupitia dhamiri yako. Amekupa uhuru wa kutenda yale uyapendayo na yanayompendeza ila unapoenda kinyume chake, atakusamehe na kukuadhibu. Kama ilivyotokea kwenye gharika kuu, Sodoma na Gomora na kwingineko.

Uovu haupo duniani. Neno uovu lipo kuelezea ile hali ya ukosefu wa mema. [absence of "good(s)"] Kama ambavyo giza halipo, ila neno "giza" lipo kuelezea ukosekanaji wa mwanga (Wanafizikia nadhani wamenielewa zaidi).

Magonjwa na mabaya yote yaliyopo ni matokeo ya maamuzi mabaya tunayoyafanya, kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu kupitia dhamiri (conscience). Kutokutumia vizuri akili na utashi.

So to say, hakuna kosa ambalo Mwenyezi Mungu amewahi kulitenda so far, hatendi na hatakuja kutenda. Hakuna mwingine aliyemkamilifu kama Yeye. Ahsante.
 
Duu we jamaa naisi unailewa biology vizur asa topic ya evolution & bibble knowledge kwn naic ww unaamina asa steady state theory ila nikuulize swal tu what is ur CONCLUTION after identification of problem...
 
Argument yako ni very popular, traditional, widely trusted but too illogical.
Wajumbe wengi mno wamesema kitu ulichokisema.

Sasa nikuulize: Kwanini Mungu aumbe kiumbe kitakachokuja kumuasi mbeleni?

Halafu unavyosema mwenyezi Mungu amenipa utashi wa kujua mema na mabaya, napatwa na swali: je kwanini Mungu aumbe ulimwengu ambao mabaya yanaweza ku-exist ilihali yeye hapendi mabaya? kwanini asingeumba ulimwengu usiowezekanika mabaya?

Hebu nielezee ni kwa jinsi gani maovu ya binadamu yanavyochangia kutokea majanga asilia kama tetemeko za nchi, radi na vimbunga pamoja na milipuko ya volcano?
 
Mkuu nikubali kwanza umeuliza swali la msingi sana, hakuna mtu mwingine aliyeuliza hili swali.

Anyway, lengo la kuleta hii mada ni kutaka kupata logic kwenye idea ya uwepo wa Mungu pamoja na uhalali wa dini wa kumpromote Mungu.
Kama ningejibiwa hizi hoja kwa ufasaha, basi ningepata majibu ya kucover viraka vilivyopo kwenye mikanganyiko ya hii idea.
Kwa bahati mbaya sana, hadi sasa hakuna mtu aliyenipa jibu la kuridhisha kwenye hoja yoyote. Hivyo hadi sasa, issue ya uwepo wa Mungu pamoja na uhalali wa dini wa kumpromote Mungu kwangu ni illogical.
 
Apo have got you well & clear mkuu
 
Hi ni sawa na kuhoji kwa nini tuna vyama tawala na vyama vya upinzani ktk siasa za Dunia? au tuseme utawala wa ngano na utawala wa magugu... tutumie hekima zetu katika njia tuipendayo....
 
Argument yako ni very popular, traditional, widely trusted but too illogical.
Wajumbe wengi mno wamesema kitu ulichokisema.

Sasa nikuulize: Kwanini Mungu aumbe kiumbe kitakachokuja kumuasi mbeleni?

Halafu unavyosema mwenyezi Mungu amenipa utashi wa kujua mema na mabaya, napatwa na swali: je kwanini Mungu aumbe ulimwengu ambao mabaya yanaweza ku-exist ilihali yeye hapendi mabaya? kwanini asingeumba ulimwengu usiowezekanika mabaya?

Hebu nielezee ni kwa jinsi gani maovu ya binadamu yanavyochangia kutokea majanga asilia kama tetemeko za nchi, radi na vimbunga pamoja na milipuko ya volcano?

Kwanza mkuu naomba nikubaliane na wewe kuwa pengine suala la uwepo wa Mungu ni gumu sana kulielezea maana humo ndani tutaingiza na concept za predestination ambazo kuna baadhi ya vitu ndani ya hiyo concept mie mwenyewe sijavielewa vizuri bado na vingine ninavyovielewa ni vigumu kuvielezea vikaeleweka virahisi.

Pili, Mwenyezi Mungu alipomwumba Shetani, kama alivyoumba Malaika na binadamu alijua kabisa kuwa huenda wakamuasi.
Alipotuumba kwahiyo alitupa uhuru wa kuchagua aidha kumwabudu ama kutomwabudu.
Mungu hakulazimishi umwabudu. Hakulazimishi ufuate sheria zake.
Yeye atakueleza tu kuwa unachoamua ni kizuri au kibaya na kina faida au madhara gani.

Wewe ndio unachagua.
Mungu hawazi kama tuwazavyo.
Hata shetani alipoumbwa kama kawaida alipewa uhuru, ila akachagua kutokuwa mwema ndio maana yakampata yale yaliyompata.

Tatu, Mwenyezi Mungu hakuumba mabaya na kimsingi mabaya hayapo (do not exist). Yale tunayoona kama mabaya ni kutokuwepo kwa mema.
Hii ni sawa na kusema kuwa kuna kifo. Kimsingi kifo hakipo, ila kutokuwepo kwa uhai, ndio tunaelezea kama kifo.

Njaa haipo (doesn't exist) ila neno njaa lipo kuelezea kutokuwepo kwa chakula.
Hapo juu nilitoa mfano wa giza kuwa halipo, ila kutokuwepo kwa mwanga tunaelezea tu kwa kutumia neno giza.

Kiuhalisia mwanga una'exist na ndio maana wanafizikia wanaweza kuuelezea, uwe aidha kwenye visible au invisible range, tofauti na giza; halielezeki kwasababu halipo.

The same applies; basically, evil do not exist. We use the terminology to just explain the absence of good(s). Thus, God did not create evil.
Everything He created was good.
Lucifer became Satan when the goodness with which he was created, ceased its existance.
Tukubaliane kwanza kwa hili, kuwa Mungu hakuumba muovu au maovu.

Nne, kuna vitu vingi sana ambavyo ni vibaya vimesababishwa na sie wenyewe baada ya kukaidi kuiishi sheria na amri kuu ya Mungu ya upendo.
Angalia magonjwa kama UKIMWI ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na uzinzi via kuwa na wapenzi wengi, n.k.

Angalia hata kisiasa, vita zote zipo kwasababu hatupendani au upendo umepungua na ubinafsi umeongezeka.
Natural disasters kama ukame na mafuriko ni kwasababu tumeshindwa kutunza mazingira ambayo Mwenyezi Mungu alitupa na kutuamuru tuyatunze. Na kuna mengine mengi.

Kama upo tayari, nadhani utakuwa umeelewa kuwa Mungu hakuumba uovu, na kwamba uovu haupo. Aliumba vyema na wema, ila baada ya binadamu kwa hiari yake kuamua kuutupa wema, ndio tukapata msamiati uitwao uovu.
Hope umenipata mkuu.
 
Kwa hiyo kwa uelewa wako wewe ni kwamba ili uamini Kama Mungu yupo basi ni mpaka ajitokeze kila mtu amuone!! Umefeli. Ili upate majibu Kama Mungu yupo au hayupo, basi unapaswa uanze

kujiuliza wewe mwenyewe Kama una akili au Hauna?? Ukijibu kuwa unazo, basi itakupasa nawe ututhibitishie je, unazo akili ngapi?

Ni doctor yupi aliye kufanyia op ya kichwa Akathibitisha kuwa unazo??

Je! Unaweza kutuonyesha akili zako ili nasi tuamini Kama kweli unazo??

Ina Maana ukitujibu kuwa huna akili basi nasi hatuta kushangaa kwanini hauamini uwepo wa Mungu

Pia Kama utatujibu kuwa unazo akili bado tutaendelea kukushangaa kwa kule kuaminikwako kuwa unazo akili hali ya kuwa hukuwahi kuziona na ukashindwa kuamini uwepo wa Mungu Eti kisa haonekani??

Pia unapouliza kuwa Eti bila sayansi maisha yasingewezekana!! Unazidi kututatanisha kuhusu akili zako!! Kwa maana Mungu huyo ambaye wewe humuamini ndiye aliyeileta hiyo sayansi ulimwenguni, sasa wewe unaimini sayansi hali Yule aliyeileta hiyo sayansi hutaki kumuamini!!!!

Nitakuonyesha kwa uchache kuwa Allah ndiye aliyeanzisha hiyo sayansi

1) KUKUTANA KWA BAHARI MBILI (YA MAJI CHUMVI NA MAJI MATAM) QUR 55:19-20

19) "Anaziendesha bahari mbili zikutane.
20) baina yao kipo kizuizi zisiingiliane

2) MELI KUPITA BAHARINI NI KWA UWEZO WA ALLAH
Quran 22:65
"Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu amevizalilisha kwenu vilivyomo katika ardhi na merikebu zipitazo baharini kwa amri yake, na amezishika mbingu zisianguke Juu ya ardhi ila kwa idhini yake..... "

3) KUUMBA VIPANDO (VYOMBO VYA USAFIRI) NA ALIAHIDI KULETA VINGI ZAIDI YA VILE VILIVYOKUWA VINAFAHAMIKA KWA KIPINDI KILE, AMBAPO LEO TUNAONA KUNA NDEGE, MAGARI, TRENI N.K

QUR 16:8" Na farasi na nyumbu na punda ili muwapande na kuwa ni pambo. Na ataumba msivyovijua"

4) MWEZI NA JUA KWENDA KWA MPANGILIO WA HESABU MAALUM QUR 36:38-39

Kwa kifupi sayansi yote chanzo chake ni Mwenyezi Mungu. Anza leo kuisoma quran na tafsir yake utapata kufahamu mengi na hatimaye Allah akipenda atakuonyesha njia iliyo sahihi

Good night
Chamilton nilisha kujibu maswali yako, rejea hizi post
 
Kama lengo lako ni kutafuta Kiki basi imekula kwako. Kinyume cha hapo utubu kwa maana hicho ulicho kipost ni dhahiri umemkufuru Muumba wako!! Au labda km tayari umesha jiunga na kile chama hvyo unataka kuwaonyesha kuwa umeiva kiasi gani kwa kuwa mpinzani wa Mungu?? Huo sio ujanja.

Je umesahau amekuumba kwa kitu gani hata leo ukawa mkosoaji na mshindani wake?
Quran 16:4
"AMEMUUMBA MWANADAM
KWA TONE LA MANII. TAHAMAKI AMEKUWA MSHINDANI DHAHIRI (WA KUMKATAA MWENYEZI MUNGU)".

Bila shaka unafanya haya kwa kuwa huna ilmu nayo hvyo unataka upate wachache wa kuwapoteza. Imani yako iko wapi ndugu??

Qur 6:120
".....NA HAKIKA WENGI HUWAPOTEZA (WENGINE) KWA MATAMANIO YAO BILA YA KUWA NA ILIMU. BILA SHAKA MOLA WAKO ANAWAJUA VYEMA WALE WARUKAO MIPAKA".

Na hiki ulicho kifanya uliongozwa na SHETANI kwa malengo yako ya kuwashuhudia watu wakibishana kati ya wanao kuunga mkono na wanao kupinga. Allah anasema katika

Quran 6:121
".... NA KWAYAKINI SHETANI WANAWAFUNULIA MARAFIKI ZAO KUBISHANA NANYI (KATIKA MAMBO NAMNA HAYA, YASIYOKUWA NA MAANA). NA KAMA MKIWATII MTAKUWA WASHIRIKINA".

Kwa hiyo kila atakaye isoma hiyo posti yako kisha aka base kwenye upande wako wa kumkosoa Mungu na kumuona ana mapungufu basi naye atakuwa amejiingiza kwenye dhambi ya shirk chanzo ni wewe.

Mwisho nikukumbushe tu, hiki ulicho kifanya ni kitendo cha kumkufuru Mungu, hvyo tubu kwa Mola kabla haijafika siku yako ya kutolewa roho

ANAYE KUFURU

QUR 30:44 "Anaye kufuru, (madhara) ya kufuru yake ni Juu yake (mwenyewe). Na wafanyao mema, (hao) wanazitengeneza nafsi zao".

Ndugu yangu, wewe siyo wa kwanza kumkufuru Mungu, siku moja ukipata nafasi fanya safari ya kutembelea huko MISRI ukamuone FIRAUN ambaye alikuwa ni bingwa wa kumkufuru Mungu. Lakini Allah alimuahidi kuwa atautunza mwili wake ili uwe funzo kwa vizazi vijavyo. Kisa cha firaun ni ishara tosha kuwa Allah yupo, na muweza wa yote.

Quran 10:92 Allah akasema
"LEO BASI TUTAKUOKOA KWA MWILI WAKO ILI UWE ISHARA KWA AJILI YA WALIO NYUMA YAKO. NA HAKIKA WATU WENGI WAMEGHAFIRIKA NA ISHARA ZETU".

sasa ili uweze kumshuhudia firaun na ishara nyinginezo za Allah basi hunabud kusafiri Kama quran 30:42 inavyo tueleza.

"SEMA: SAFIRINI KATIKA ARDHI NA TAZAMENI JINSI ULIVYOKUWA MWISHO WA WALE WALIO TANGULIA. WENGI WAO WALIKUWA NI WENYE KUSHIRIKISHA.

nenda Misri ukauone mwili wa firaun/farao mpaka leo bado upo. Ni maoni yangu tu!!
Na hii
 
Back
Top Bottom