Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

They say There is power in the darkness and you did the best to find it. But you are on their trap trust me those are not human being thoughts bt they talk by using your mind. Free ideas free masons. The mind has a limit capacity of thinking when it comes to God and when you cross the line you are no longer a believer bt the Illuminati agent
I question everything and believe none of them unless there's doubtless evidence.

If you believe God created us with the mind capable of questioning everything including him/her self [to be honest I don't know God's gender] then why should we stop?
If limits exist, then are within your mind........I think the mind is limitless and we should make sufficient use of it.
Concerning what you've said about the Illuminati and the way they manipulate man's ability, that's fault number one.
 
Rejea post ya kwanza nilichoandika. Hii mada humu haiwezi kujadilika kwa mapana vizuri. Needs a variety of time and references that can't be well attached here.
Una hoja Nzuri elewa kuwa nimeipenda lakn not affordable to be answered in this way.
Sasa kama haijibiki hapa itajiwa wapi?
 
Maswali yamekuwa magumu kujibu.
Tusipojua nini tunakijadili basi tutaweza kuulizana maswali hata wiki nzima,hebu tizama huu uzi ni wa muda mrefu lakini bado unaonekana kama mpya..ni maswali mangapi yameulizwa toka uanze huu uzi lakini hakuna kilichobadilika.
 
Sasa kama haijibiki hapa itajiwa wapi?
Ukijibiwa kisimple huwezi kuelewa tutaishia kuweka mabishano yasotija. Mahali kwa kujibia kupo kwingi tu na si mimi pekee yangu mwenye uwezo wa kujibia hata karibu yako wapo nina imani hiyo.
Humu hatujuani yawezekana pengine ni jirani yangu ila humu huwezi kujibiwa efficiently utajaza page zote peke yako.
 
I question everything and believe none of them unless there's doubtless evidence.

If you believe God created us with the mind capable of questioning everything including him/her self [to be honest I don't know God's gender] then why should we stop?
If limits exist, then are within your mind........I think the mind is limitless and we should make sufficient use of it.
Concerning what you've said about the Illuminati and the way they manipulate man's ability, that's fault number one.
What you argue is right only when it comes to what you believe bt my faith and my religion teaches me there is a limit of asking when it comes to God. Example if i do the research on what is the nature of God or asking questions like "if God can create a creature who has ability like him or more than him'' Totally by doing such what you think is using my mind to find facts i will no longer be a believer and finally i will conclude by saying once upon a time God was created by human being in order to threaten people, reduce crimes and make the world a better place for living.
My side on this is to stop reasoning God's decisions and am still stand on this, human being has a limited mind when you want to expand it you will no longer be a believer then you will be a free minded. Free mind=free person = free mason and those both are also free to find the secret that found in the darkness.
 
Ila sema ndiyo hivyo tu kujifanya wanajua sana na sie wengine tunaonekana hatujui kitu,ila kiukweli maswali yanayoilizwa hayana mchango katika mjadala wa uwepo wa mungu.

Huwezi ukataka kujua kila kitu kuhusu mungu ili et ndiyo ukubali uwepo wake,hata katika maisha ya kawaida haipo hivyo kwamba ili umjue mtu lazima ujue kila kitu.

Sasa hapa mtu haamini mungu ila anahoji mambo ya kuhusu mungu ambayo hayatoweza kusaidia ubishano wa uwepo wa mungu.
 
Nami nimerudi hapa.
Wanaoamini wanasema mungu hujua nini tunachowaza na nini kitatokea. Kama alimuumba ibilisi ina maana alijua ibilisi atakuwa shetani, sasa kwanini alimuumba huyo ibilisi wakati kabisa alijua atakuwa shetani?
Na hilo ndilo swali lililokuwa linafatia,
Hawezi lijibu hilo.
 
Ndugu nimesoma post yako na nimesikitika sana tena sana, lakini MUNGU, akusamehe bure kwa kumlaumu bila sababu na bila kujua ukweli uko wapi. Nakushauri rudia kusoma "maandiko"(Biblia) utaelewa tu nia ya Muumba wetu ilikuwa ni ipi baada ya kutuumba.

Mimi nitajaribu kukujibu hoja zako kifungu kwa kifungu kama vile wewe ulivyoandika. Na majibu yangu kwako, nitatumia vifungu vya kutoka kwenye "Biblia" kwani ndio maandiko matakatifu ninayo amini mimi. Nakuomba ili uweze kuelewa kile nilichoandika, uwe na "Biblia" yako pembeni ili uweze kulinganisha yale niliyokuandikia.

1.KUMUUMBA SHETANI
Ndugu yangu, Bwana Mungu, ameumba viumbe wengi sana na wa kila namna, na kila alichokiumba MUNGU, tazama kilikuwa ni chema kabisa. Soma kitabu cha MWANZO 1 : 31. MUNGU, hakumuumba "shetani" kama "shetani" alivyo leo, Mungu alimuumba malaika aliyekuwa anaitwa "Lusifer". Neno shetani {Satan}, maana yake ni Adui. Lucifer alikuwa kama malaika wengine walioko Mbinguni, isipokuwa tu aliamua mwenyewe kuwa adui ya Mungu.Inasemekana kwamba Lucifer kwa sababu ya uzuri aliokuwa nao alijawa na majivuno na dharau,kiasi kwamba akajawa na kiburi na kujiona yeye ndio yeye na hakuna mwingine zaidi yake. Fahamu kuwa MUNGU alipowaumba viumbe wake, hasa wale aliowapa uwezo wa kujitambua, yaani malaika na wanadamu, aliwapa pia uhuru wa kuamua nini cha kufanya{free will}. Soma MWANZO 2: 15-17. MUNGU, hakuumba mashine wala Robots, MUNGU aliumba roho na kuzipatia uhuru wa kuamua nini cha kufanya, ili mradi tu, roho hizo zimtambue yeye kuwa ni BWANA MUNGU, na zimtii Yeye, na akaweka pia hukumu na sheria, kwamba roho zitakazo mtii atazitunza na kuzihifadhi milele na roho zitakazo asi ataziangamiza kwa muda aliopanga Yeye. Soma UFUNUO 20:11-13 Pia unaweza ukasoma SEFANIA 3:1-2 Soma pia MATHAYO MTAKATIFU 24:36

2.KUISHI MAFICHONI
Ndugu yangu umeandika eti, MUNGU, anaishi mafichoni, hapana hata kidogo. Mwenyezi MUNGU, haishi mafichoni, anaishi Mbinguni. Soma ISAYA 66 :1-2 Fahamu kwamba, baada ya BWANA, MUNGU, kumuumba Adamu, alikuwa na kawaida ya kwenda kumtembelea bustanini kila siku jioni na kuongea nae, Soma MWANZO 3: 8-9. Hapa utaona kwamba BWANA MUNGU, alikuwa akiongea na Adamu kama vile mtu aongeavyo na baba yake. MUNGU, hajajificha, bali sisi ndio tumejificha baada ya kutenda dhambi. Dhambi zetu ndio zimetuficha tusiuone uso wa MUNGU, Soma ISAYA 59: 1-4. Kwa sababu BWANA MUNGU ni mtakatifu sana tena sana, binadamu mwenye dhambi hawezi akauona uso wa MUNGU na akabaki hai. Uso wa MUNGU ni kama moto uwakao na binadamu mwenye dhambi ni kama majani makavu yaliyomwagiwa mafuta ya petrol, ukiusogeza moto uwakao kwenye petrol nini kitakachotokea?? Soma; WAEBRANIA 12:29. Fahamu pia kwamba BWANA MUNGU, ametenga siku ya hukumu, na wale wote waliotenda mema na kuitii sauti yake na kufanya kama alivyowaagiza, basi atawachukua na kuishi nao milele. Soma UFUNUO 22:12. Kitu kingine ndugu yangu, usimchukulie MUNGU poa tu ukadhani amenyamaza kimya na hataongea kabisa au hatatokea. Siku ikifika utamuona, kwani hata yeye amesema hivi; "Bwana atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu. Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja". Soma ISAYA 42 :13-16.
Ndugu yangu MUNGU hajajificha, ni kwamba anatuonea huruma sana, kwani akisema ajitokeze sasa hivi hakuna atakayebakia hai sababu sisi wote ni wenye dhambi, wote tutateketea kwa moto, sababu Yeye ni moto ulao. Soma ISAYA 33: 14-16.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU
Ndugu yangu, ukisoma maandiko hakuna mahali imeandikwa kuwa gharika ilikuwa ni suluhisho la kuondoa ama kukomesha kabisa dhambi duniani. Kama wewe kuna mahali umeona imeandikwa hivyo, basi nijulishe na mimi nisome. Sababu kubwa iliyopelekea BWANA MUNGU, kukiangamiza kizazi kile ilikuwa ni baada ya baadhi ya malaika kuwatamani wasichana siku zile kwa kuwa walikuwa ni wazuri, basi wakaacha makao yao Mbinguni, na kushuka duniani na kujitwalia mabinti waliowapenda na kuwaoa na kuzaa nao watoto. Hii ilipelekea maovu yakazidi sana duniani ndio maana Bwana Mungu akaghairi kumfanya mwanadamu, akaapa kumuangamiza. Kumbuka hapa aliapa kumuangamiza mwanadamu, hakuapa kuufuta uovu kabisa {kwa wakati huo lakini}, tena alihuzunika sana moyoni mwake kwa nini alimuumba mwanadamu. Lakini kwa sababu MUNGU, ni mwenye haki, akamuona Nuhu hana hatia ya kuangamizwa, hivyo Nuhu akapata neema machoni pa BWANA. Soma MWANZO 6:1-8. Fahamu pia kwamba lengo la BWANA MUNGU, kuumba dunia ni ili ikaliwe na watu, hakuumba dunia ili iwe ukiwa. Soma ISAYA 45:18-19. Fahamu pia kwamba BWANA MUNGU, ametenga siku maalumu atakapokomesha kabisa uovu duniani na kuufutilia mbali. Siku ambayo atamkamata Shetani(Lusifer) na kumtupa kwenye moto. Shetani pia anajua vizuri kabisa kuwa kuna siku ambayo atatupwa kwenye moto na hata toka tena milele ndani ya moto huo. Soma UFUNUO 12: 12. Pia unaweza ukasoma UFUNUO 20:10.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAEL
Unasema eti, kwanini MUNGU, aliwapeleka wana wa Israeli kuangamiza mataifa mengine ili wao wachukue nchi za mataifa hayo. Ndugu yangu, fahamu kwamba BWANA MUNGU, hakuwaondoa wale mataifa mengine kwa kuwaonea, hapana, hata kidogo, mataifa yale yalifutiliwa mbali kwasababu ya maovu waliyokuwa wanafanya watu wa mataifa hayo, Soma KUMBUKUMBU LA TORATI 9: 4-5. Lakini pia ndugu yangu, nikuulize swali; wewe u, nani hata umuulize BWANA MUNGU, wako eti, kwanini alifanya hivi ama vile?? Wewe ni nani mpaka umuhoji BWANA MUNGU, maswali?? Fahamu kwamba imeandikwa "Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; unafanya nini? Soma ISAYA 45 : 9-10. Ndugu yangu, BWANA MUNGU, ana haki na uhuru wa kufanya chochote kile juu yetu kama vile "mfinyanzi" alivyo na uhuru wa kufanya juu ya vile vitu alivyovifinyanga au alivyotengeneza. Mfinyanzi akitengeneza chungu cha udongo au kikombe au bakuli ama chochote kile akitengenezacho, ana uhuru na haki ya kuvitunza vitu hivyo au kuvivunja vunja vipande kama akiona havimpendezi machoni pake. Soma YEREMIA 18:5-7. Fahamu kwamba, ukiwa kama binadamu, huna haki wala ruhusu ya kuhoji kazi ya MUNGU, wala huna ruhusa ya kusema eti, MUNGU, alikosea.
Vilevile unapaswa kuelewa lengo la BWANA MUNGU, kuwaondoa wana wa Israel kutoka Misri na kuwapeleka nchi ya ahadi. Hakuwaokoa Waisraeli sababu walikuwa ni watu wasio na dhambi, hapana, aliwaokoa na kuwapeleka katika nchi ya ahadi ili baadaye kwa kutumia uzao wao(yaani Yesu Kristo) auokoe ulimwengu wote kutoka katika dhambi, na hili limekwisha fanyaika tayari, kwani baada ya Yesu kuzaliwa na kufa na kufufuka, ameuokoa ulimwengu wote kutoka katika dhambi. Soma YOHANA MTAKATIFU 3:16-18

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAMU
Ndugu yangu, niliposoma haya maneno ya hichi kifungu chako nilisikitika sana sababu inaonyesha ni jinsi gani hujui maana ya maandiko na ahadi ya BWANA MUNGU, kwa Abrahamu. Ndugu yangu, imeandikwa, "Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye MUNGU wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki". Soma ISAYA 40:28. Ahadi ya BWANA MUNGU, kwa Abrahamu hakumaanisha kuwa uzao wake utakuwa ni ule tu utakaotoka kwenye viuno vyake, hapana, BWANA MUNGU, alimaanisha kuwa uazo wa Abrahamu utajumuisha watu wote watakao mpokea YESU na kumwamini ya kuwa ni Mwana wa MUNGU na alikuja duniani kutoka kwa MUNGU ili auokoe ulimwengu kutoka katika dhambi. Ndio maana YESU alisema kuwa wale wote watakao amini na kuzaliwa upya yaani kubatizwa, atawafanya kuwa watoto wa MUNGU. YESU ingawa ni mwana wa MUNGU, lakini alizaliwa duniani kutoka kwa uzao wa Abrahamu, sasa kama YESU ni uzao wa Abrahamu, na wale wanaoamini na kubatizwa wanafanywa na YESU kuwa watoto wa MUNGU, huoni kwamba ahadi ya MUNGU kwa Abrahamu imetimia na bado inaendelea kutimia? Abrahamu alizaa watoto kwa njia ya mwili, na YESU ambaye pia ni uzao wa Abrahamu amezaa watoto wengi zaidi kwa njia ya imani na wokovu wala sio kwa njia ya mwili bali imani. Soma YOHANA MTAKATIFU 10:14-16 Pia unaweza ukasoma UFUNUO 7:9-17.

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY)
Unasema eti kwanini watu wema wanapata allergy(mzio) wakila baadhi ya vyakula? Kwanza kabisa nikuambie duniani hakuna mtu mwema hata mmoja. YESU mwenyewe alisema hakuna aliye mwema ila ni mmoja tu naye ni "BWANA MUNGU" peke yake. Soma LUKA MTAKATIFU 18:19. Pia kwenye Zaburi imeandikwa hivi; "Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna MUNGU; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema. Toka Mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye MUNGU, wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja". ZABURI 14: 1-3.
Kuhusu eti kwanini BWANA, aliruhusu kuwepo kwa allergy na mimea yenye sumu? Mbona jibu lake liko wazi, hata ukimuuliza mtoto wa darasa la 3 atakujibu. BWANA MUNGU, aliruhusu yote hayo sababu ya dhambi zetu. Baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi, dunia ililaaniwa na vyote vilivyomo ndani yake, fahamu kwamba mpaka ardhi unayoikanyaga ili laaniwa pia. Soma MWANZO 3:17-19. Kwa maana rahisi tu, sio MUNGU, anayetuletea shida na matatizo, bali, anayeleta shida, matatizo, na kila aina ya udhaifu unayoijua wewe ni "shetani". Ibilisi ndiye aliyeleta dhambi duniani, na dhambi ikija haiji peke yake, dhambi huambatana na matatizo ya kila namna, dhambi imebeba kila aina ya shida na kubwa zaidi dhambi imebeba kifo. Lakini licha ya hayo yote bado MUNGU, ametoa nafasi nyingine ya kusamehe dhambi zote kwa sharti moja tu, "kutubu, kuacha kabisa kutenda dhambi na kumkubali au kumpokea YESU kama Bwana na Mwokozi wako." Wale wote watakaompokea YESU, watasamehewa na kupewa uzima wa milele na wataishi katika dunia mpya kabisa ambayo ndani yake kutakuwa hakuna cha allergy, wala kifo, wala mmea wowote ule wenye sumu. Soma UFUNUO 3:20-22

7.MAJANGA ASILIA
Kama ambavyo nimekueleza hapo juu katika kifungu namba sita, hapa napo umerudia kuuliza eti, kwanini MUNGU, anaruhusu majanga asilia kama matetemeko ya ardhi, mafuriko, na vimbunga? Ndugu yangu mpaka sasa naamin unajua tayari kwanini hayo yote yameruhusiwa kutokea duniani. Yote hayo majanga yanatokea na yametokea na kuua watu wengi sana kwa sababu ya dhambi zetu sisi wanadamu. Hakuna sababu nyingine, ni "dhambi". Kama nilivyokuambia, hii kitu inaitwa dhambi haiko peke yake, dhambi ni balaa kubwa sana. Dhambi inaambatana na kila aina ya matatizo na mabalaa ya kila namna. Dhambi ni kitu mbaya sana. Tena kwa taarifa yako kuna mambo mabaya sana ambayo bado hayajatokea. Imeandikwa; "siku za mwisho kutakuwa na dhiki kubwa mno ambayo haijawahi kutokea duniani", tena YESU, akasema, "kwa kuwahurumia wanadamu, MUNGU amezifupiza siku hizo za dhiki kuu, maana kama asingezifupisha, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka wakati huo. Lakini kwa ajili ya wateule, zitafupizwa siku hizo". Soma MATHAYO MTAKATIFU 24:21-24

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI
Ndugu yangu nafikiri hapa pia swali lako limejirudia tu. Lakini fahamu ya kwamba BWANA MUNGU, aliweka baraka kama tutayashika na kuyatenda maagizo yake na amri zake. Vile vile aliweka laana kama tutakwenda kinyume na maagizo yake na mafundisho yake na amri zake. Na laana alizoweka ni pamoja na magonjwa ya kila namna, njaa, vita, na kila namna ya matatizo ambayo unayajua wewe, Soma KUMBUKUMBU LA TORATI 28:15-43 Ukisoma vizuri kuhusu laana hizo utagundua kwamba zilielekezwa kwa wanadamu wote wasiotaka kumtii BWANA MUNGU, wao.

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE
Hapa pia umenisikitisha sana unaposema kwanini MUNGU, ameweka Jehanamu ya moto kwa ajili ya kumchoma shetani na watu wote waovu. Tena umesema eti, kwanini MUNGU, hana msamaha? Sio kweli kama MUNGU, hana msamaha. BWANA MUNGU, ana roho ya kusamehe na tayari ameshasamehe ndio maana alimtoa Mwanaye YESU, afe kwa niaba ya wanadamu wote. Rudia tena kusoma YOHANA MTAKATIFU 3:16-18. Tena imeandikwa; "dhambi zote watakazofanya wanadamu chini ya jua watasamehewa isipokuwa dhambi ya kumkufuru roho Mtakatifu haitasamehewa kamwe, sio katika ulimwengu huu tu, hata katika ulimwengu ujao" Soma MATHAYO MTAKATIFU 12:31-32.
Hivyo, kwa maneno hayo, shetani hawezi kusamehewa sababu tayari amenena maneno makubwa sana ya makufuru dhidi ya MUNGU, maneno ambayo hayawezi kutamkwa, Soma 2 WAKORINTHO 12:2-4. Pia unaweza ukasoma; UFUNUO 13:5-7
Mimi binafsi, nakushauri ndugu yangu, tubu dhambi zako, omba msamaha, mwamini YESU KRISTO, kwa kuyashika mafundisho yake na kutenda kama alivyokuagiza na wewe utasamehewa dhambi zako. Lakini kumbuka kila kitu kina mipaka yake, MUNGU, pia ameweka mipaka ya dhambi, kuna dhambi ukizitenda, kama dhambi ya kumtukana MUNGU, hutasamehewa milele.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU
Kifungu hichi nacho ni kama kimejirudia tu, na maelezo yake nimeshakufafanulia kwenye vifungu hivyo hapo juu. Bwana, MUNGU, alimuumba mwanadamu aliyekamilika kabisa. Tatizo lilianza baada ya wazazi wetu wa kwanza yaani, Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi. Kama nilivyokuambia awali, dhambi imeleta matatizo mengi sana kwa mwanadamu. Kwasababu ya dhambi, ndio maana leo hii wanazaliwa watu wenye kasoro mbali mbali kwenye miili yao. Ukisoma vizuri maandiko utaelewa. Kwasababu binadamu alimruhusu shetani kuingia kwenye maisha yake, shetani naye akaitumia hiyo nafasi kupandikiza kasoro kwenye miili ya wanadamu ili tu awagombanishe wanadamu na Muumba wao na katika hilo amefanikiwa, sababu leo hii wewe unamlaumu Muumba, wako kwasababu ya kasoro zilizoko kwenye miili yetu. Ukweli ni kwamba kasoro zilizoko kwenye miili yetu zimepandikizwa na Ibilisi. Kumbuka lile tunda walilokula Adamu na Hawa, lilikuwa ni sumu na sumu hiyo imesambaa kutoka kizazi hadi kizazi. Na ndio maana BWANA MUNGU, aliwaambia "msile wala kugusa kabisa matunda ya mti ule kwani siku mtakapokula, mtakufa hakika". Na shetani akasema mkila matunda ya mti huu hamtakufa, Je! Ni kweli kwamba hatufi?? Leo hii Adamu na Hawa wako wapi? Hawajafa? Watoto wao hawajafa? Mimi na wewe hatutakufa??
Ndugu yangu, fahamu kwamba, aina yoyote ile ya udhaifu kwenye mwili wa binadamu, umepandikizwa na Ibilisi yaani shetani. Soma LUKA MTAKATIFU 13:10-13

Hitimisho la yote niliyokuandikia ni wewe unayejiita CHARMILTON ufahamu ya kwamba ni kosa kumuuliza Muumba wako eti, kwanini alifanya hivi ama vile. Kumbuka mimi na wewe ni mavumbi tu, mimi na wewe ni kama unyasi tu, unao mea leo na kesho kunyauka na kuliwa na mchwa. Ibilisi anafanya yote anayofanya ili kutufanya sisi wanadamu tumchukie Muumba wetu, na tuamini kwamba shida, mateso, magonjwa na kila aina ya matatizo yanayotupata hapa duniani yamesababishwa na MUNGU. Kumbe sio kweli hata kidogo, matatizo yote yameletwa na huyo Ibilisi. BWANA, MUNGU, hapendi kuona mwanadamu aliyemuumba anateseka. Na ndio maana ameweka siku ya hukumu, siku ambayo atayamaliza haya yote na hayatakuwako tena milele. Imeandikwa "maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu, wala kuwahuzunisha". Soma MAOMBOLEZO 3:31-33.

Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nawe.

 
Mungu atakupa laana kuanzia wew na uzao wako wote
Nadhani Ndio mara yako ya kwanza kusoma Mambo kama haya,
Nalazima ushituke tu,Sasa unaanza kutoa vitisho.
"Et laana" huu Ndio Woga unaojengwa tangu utotoni katika vitabu vyenu.
 
Mungu ataendelea kuwa Mungu tu hata kama hajatenda unavyotaka. Cc ni wanadamu ww ni nan mpka uthubutu kusema mambo hayo! Kasome mithali ``Ulimi ni kiumbe kidogo sana lkn"!! Utamaliziaaa
 
Na hilo ndilo swali lililokuwa linafatia,
Hawezi lijibu hilo.
Haha yani hakuna mnachoweza zaidi ya kuuliza tu maswali na ni faraja kwenu mtu kushindwa kujibu maswali yenu.

Na ndiyo maana hizi mada hazina mafanikio yeyote.
 
Huyu jamaa watu mmemchukulia kama mhalifu hivi lakini anapaswa kueleweshwa yooooote haya aliyoyasema chanzo chake ni mbinguni

Na dhambi ilianzia huko (mbinguni) na ndio maana kwenye anasema wazi

"Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni"

Isaya 65 : 17

Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

2 Petro 3 : 13

Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

Ufunuo wa Yohana 21 : 1

Si unanona hayo maneno?? Kwa sababu Mungu ni mtakatifu baada ya ile dhambi tu akafanya mbingu mpya na nchi mpya

Swali langu huwa moja tu Mungu hakujuaaa????
 
Back
Top Bottom