Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Ukiamini Mungu wa uongo huyu hata maendeleo ni vigumu kupata.

Wanasiasa waongo watakuchezea akili.

Watakwambia wao ni "chaguo la Mungu".

Na ukiamini hilo, hata kuwahoji utashindwa.

Watakupiga maisha yote, wakikuambia utalipwa peponi.

Huku hata wao wakijua hakuna pepo.

Ndicho kinachoendelea sehemu nyingi sana duniani.
Nakubaliana na wwe 100%
 
Moja ya sababu tunakufa nikutokanana ukweli kwamba hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezowote na upendo wote.

Mungu huyoangekuwepo, kwanini asingeumba ulimwengu ambao hauna kifowalaubaya wowote?

Uwezo angekuwa nao, ujuzi angekuwa nao, upendo angekuwa nao, kitu gani kingemzuia asiumbe ulimwengu ambao mabaya yoyote hayawezekani?

Kama angeweza kuwa na kitu kinachomzuia, je nikweli angekuwa na uwezo wote, mbona kungekuwa na kitu kinamzuia kuumba ulimwengu bora kabisa?

Kama hakuna ambacho kilimzuia, hakutaka tu, je, Mungu ambaye anaweza kutupotezea kirahisi hivyo, kutubania bila sababu, anaweza kuwa Mungu mwenye upendo wote? Mbona atubanie hivyo?

Ukichunguza sana unaona kuwa, Mungu huyo hayupo.

Ila watu wengi washakubalishwa yupo, wanafuata mapokeao tu.
Wewe hapo ndio unapowaongopea wajinga wajinga,kwanini usiseme Mungu hana sifa ya Upendo kama anavyoelezwa na ndio maana tunakufa au anao upendo ila hana Uwezo wote ndio ameshindwa kuondoa kifo? Hapo ndiyo ungekuwa umeonesha contradiction ni kwamba hayo yanayoelezwa kuhusu Mungu haiwezekani yote kuwa sahihi,ila ajabu wewe unakuja na hoja ya kuwa hakuna Mungu.

Umejuaje hakuna Mungu kwa kutumia hiyo contradiction tu ? Hapo ndio unapowaburuza wenzio.
 
Umekubali haiwezekani Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuwepo?
 
Kwa mtazamo wangu naona kama vile kuna malengo ameweka kabla hajafanya hitimisho anataka kuona ushindani ukiwepo kwa Jamii zote zenye akili timamu na ndio maana kuna ubaya na wema na ndio maana tunajiuliza maswali mengi majibu yapo mengi tu kichwani mwako na sio lazima upatie kujibu Wapo watakaopatia kujibu wapo watakaokosea hapa ndio kwenye hitimisho na kwa nini mungu alimuumba lucifa kwa mtazamo wangu naona alikusudia awepo ili kuwe na ushindani wa kifikra yeye mungu angeweza kumfanya lucifa akawa mpoole lakini dunia ingekua haina changamoto kusingekua na watu wajinga na wajanja hivyo dunia ingekua haina maana ya kuwepo kwake Ngoja niishie hapa maana sina Hakka nayo
 
Nachofurahia hii thread itawaunganisha wakristu na waislam, wapagan ndo watakuwa kivyao
Kufikiri Waislamu na Wakristo wana tofauti kubwa ni ufinyu wa mawazo tu.

Wote wanaamini ujinga ule ule tu.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
 
Kwa mtazamo wangu naona kama vile kuna malengo ameweka kabla hajafanya hitimisho anataka kuona ushindani ukiwepo kwa Jamii zote zenye akili timamu na ndio maana kuna ubaya na wema na ndio maana tunajiuliza maswali mengi majibu yapo mengi tu kichwani mwako na sio lazima upatie kujibu Wapo watakaopatia kujibu wapo watakaokosea hapa ndio kwenye hitimisho na kwa nini mungu alimuumba lucifa kwa mtazamo wangu naona alikusudia awepo ili kuwe na ushindani wa kifikra yeye mungu angeweza kumfanya lucifa akawa mpoole lakini dunia ingekua haina changamoto kusingekua na watu wajinga na wajanja hivyo dunia ingekua haina maana ya kuwepo kwake Ngoja niishie hapa maana sina Hakka nayo
Kama alimuweka ibilisi kwa ajili ya binadamu wapate changamoto sasa kwanini achukizwe na dhambi za hao binadamu baada ya kujaribiwa na huyo shetani? Wakati yeye alijua kabisa kua sisi ni viumbe ambao hatujakamilika hivyo ni rahisi shetani kuturubuni

wewe unaeza utengeneze ngalawa iliyotoboka na yenye mapungufu ya vifaa alafu ukijua kabisa kua haiko salama kwa kusafiri nayo then umpe mtoto wako asafiri nayo kwenye ziwa lenye mamba na viboko wakali kwa kusema kwamba nimefanya hivyo ili apate challenge kwenye hiyo safari yani asibweteke?

je utakua ni mzazi mwenye upendo wa kweli kwa huyo mtoto?
 
Hizi habari za Mungu ni kamba tupu.

Mungu amuweke Ibilisi ili watu wapate changamoto ili iweje? Haya mabaya yote yanayotokea, Mungu anapenda?

Na kama ni hivyo, kwa nini Ibilisi alaaniwe? Wakati kuwapo kwa Ibilisi ni mpango wa Mungu ili watu wapate changamoto?

Watu wasingepata changamoto, wangepeta tu katika dunia isiyo na ibilisi, dhambi wala mabaya kuwezekana, Mungu angepungukiwa nini?

Huyu Mungu yupo kweli? Aau ni stories tu?
 
Jibu rahisi hizo ni stori tu

Kwasababu huyo huyo mungu anasema siku ya mwisho atamchoma shetani kwenye moto wa milele wakati yeye mwenyewe ndiye aliye mtuma shetani kuwajaribu binadamu

Sasa sijui alitegemea kua shetani atashindwa kazi aliyotumwa maana mi naona shetani amefanikisha kazi aliyotumwa ya kujaribu binadamu sasa adlistshili tuzo kwa kufanya kazi yake kwa weledi, sasa badala ya tuzo eti atachomwa na moto wa milele hivi ina make sense kweli?
 
Hizi habari za Mungu ni kamba tupu.

Mungu amuweke Ibilisi ili watu wapate changamoto ili iweje? Haya mabaya yote yanayotokea, Mungu anapenda?

Na kama ni hivyo, kwa nini Ibilisi alaaniwe? Wakati kuwapo kwa Ibilisi ni mpango wa Mungu ili watu wapate changamoto?

Watu wasingepata changamoto, wangepeta tu katika dunia isiyo na ibilisi, dhambi wala mabaya kuwezekana, Mungu angepungukiwa nini?

Huyu Mungu yupo kweli? Aau ni stories tu?

Kibaya zaidi huyo mungu haiwezi kujithibitisha kwa watu mpaka atumie mtu

Alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu wangemjua bila kutumia mtu mwengine?

Kwanini kumjua mungu mpaka amtume mtu ?

Hapo ndipo utaona huyo mungu ni hadithi
 
Eti unaambiwa kujua neno la Mungu mpaka ujue Kiarabu, utafsiri mambo kutoka Kirabu.

Au ujue Kiyahudi. Utafsiri mambo kutoka Kiyahudi.

Huyo Mungu mbona kawatenga Wadigo hivyo?

Alishindwa kumshushia neno lake kila mtu katika namnanisiyo na shaka kwenye DNA?
 
Eti unaambiwa kujua neno la Mungu mpaka ujue Kiarabu, utafairi mambo kutoka Kirabu.

Au ujue Kiyahudi.

Huyo Mungu mbona kawatenga Wadigo hivyo?

Hapajawahi kutokea manabii au mitume walioandikwa ktk quran au bible kutoka nje ya wayahudi au warabu

Kwanini nchi nyingine kama China Hindus au wazungu hakuna walioandikwa ktk vitabu hivyo

Hivi huyo mungu kweli atakuwa anayo busara kweli?
 
Hivi huyo mungu ni me au ke? Akiwa ke mimi ntachagua motoni na kama ni me mbona sijawahi sikia hadithi za mke wa mungu? Au huko mbinguni wote ni CHAPUTA?
 
Hapajawahi kutokea manabii au mitume walioandikwa ktk quran au bible kutoka nje ya wayahudi au warabu

Kwanini nchi nyingine kama China Hindus au wazungu hakuna walioandikwa ktk vitabu hivyo

Hivi huyo mungu kweli atakuwa anayo busara kweli?
Hapo ndipo utakapoona hivyo vitabu si vitabu vitakatifu vya Mungu.

Ni vitabu vya watu, vilivyoandikwa kufuata muktadha wa tamaduni zao.

Nilikuwa nasoma kitabu cha Karl Evanzz, kinaitwa "The Messenger: The Rise Aand Fall of Elijah Muhammad".

Elijah Muhammad ni founder wa "The Nation of Islam", kundi la Waislamu wa Marekani ambao walikuwa na muamko mkubwa wa kisiasa na kupinga maovu mengi ya serikali ya Marekani, kundi hili ndilo lilimtoa Malcolm X na kum seduce Muhammad Ali mpaka akabadilisha dini.

Kuna sehemu Elijah Muhammad alikuwa anagombana na watu wa Orthodox Islam, wa Sunni, kutokana na mambo yake yaliyo controversial, kwa kutumia jina la Uislamu.

Elijah Muhammad akawaambia ma Sheikh wale wa Sunni kwamba, kama mnataka kuniletea habari za kutaka kunitawala, nitawaambia mamilioni ya Waislamu wanaonifuata mimi huku Marekani, waache kuswali huku waki face Mecca, wote wanze kuswali waki face Chicago, makao makuu ya Nation of Islam Marekani. Kwa sababu hata katika Uislamu kabla ya kwatu kuswali wakielekea Mecca, walikuwa wanaswali kuelekea Jerusalem, tutabadilisha tu.

Wwale ma Sheikh wakampoza, wakendelea naye uzuri, mpaka leo Natiuon of Islam misikiti yao wanaswali kuelekea Al-Qqabr Mecca.

Hili jambo linaonesha kwamba hizi habari ni tamaduni tu watu wanajiwekea.

Tena ni utumwa wa kimawazo.

Ukishaambiwa Mungu kashusha Quran kwa Waarabu, na ukisali lazima uelekee Mecca, automatically unajitoa utu wako, na kujiona wewe hufai, kwenu hakufai, lugha yako haifai.

Kiarabu ndicho kinafaa, Mecca ndiko kunafaa.

Kama wewe ungekuwa unafaa, kwa nini Al-Qqabr isingekuwa kwenu? Kama lugha yenu inafaa, kwa nini Mungu hakushusha Quran au Biblia kwa lugha yenu?

Ni utumwa wa kiutama duni tu.
 
Back
Top Bottom