Wewe Astro nomaaa, hujui ni kwa sababu gani Mungu huwa anatuma manabii kwa watu, ungalijua wala usingali uliza hilo swali.
Mungu alikuwa akipeleka manabii kwa watu waovu ili manabii wawaonye. Sasa kama hakukuwa na nabii Mswahili au Mzungu nk, maana yake watu hao walikuwa ni wema na safi.
Lakini ukisoma Qur'an, Allah anamuambia mtume (saw) kwamba kuna manabii wengine hajamsimulia habari zao, kwa maana hiyo duniani kulikuwa na manabii wengi waliopita ambao habari zao hatuzijui.
Kuna hadithi moja ya mtume (saw) inaunga mkono hiyo aya kwa kusema:- duniani walipita manabii laki moja na elfu ishirini.
Lakini wewe huamini uwepo wa Mungu, sasa unataka kujua habari za mitume wake ili iwe nini??.