General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,316
- 23,178
kwan kero za walimu ni kushindwa kulipa nauli?
Mkuu wa wilaya ya.kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.
Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa raisi mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa anamajukumu mengi hasa yakumsaidia mheshimiwa raisi.
Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu.au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
huyu mkuu wa wilaya ni bure kabisaHakuna kitu kama hicho, yeye kaamua kuongea kwa kuwa ana mdomo tu. Kuna walimu wanafundisha kinondoni lakini hawaishi kinondoni na pia kuna walimu wanaishi kinondoni lakini wanafundisha wilaya nyingine Labda atoe hela ya mfukoni kwake awape walimu wanaofundisha shule za kinondoni.
Kutekeleza wazo lake Walimu posho ya nauli kama wameshindwa kuwapa teaching allowances!
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.
Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa Rais mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa ana majukumu mengi hasa ya kumsaidia mheshimiwa Rais.
Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
sasa ikitokea kua gari Zima wamepanda walimu maana watakua hawana uniform itakuaje?Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
na hapo tukifuata haki , yule aliyetoa hela ambaye ni mwanafunzi ni lazima akae kwenye kiti na huyo mpenda vya bure ambaye ni mwalimu asimame .Yaani hapo sipati picha konda anataka nauli yake alafu unamwambia we mwalimu, anaanza kugomba sasa kwa sauti kubwa watu wote wanakugeukia wewe, utatamani uwe sisimizi