Uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu ni wa kimaskini ndio maana unaona wanataka watu wapate huduma bure. Hawa ndio wakikaa ofisini wanajitahidi kuandika proposal za kusaidiwa na wafadhili. Kichekesho kinakuja siku huyo mfadhili anayekuja kukuletea huo msaada yeye anakuja na gari moja tena Rav4, huyo aliyeomba msaada anakuja na msafara wa maVX V8!! Nijuavyo mimi mafuta yameshuka bei sana duniani, ni kwanini asiibane serekali yake kuhakikisha mafuta yanashushwa bei hapa nchini ambapo itapelekea nauli kushuka, sambamba na kuboresha mishahara ya waalimu kila mmoja aweze kujilipia nauli? Ama kama ni mzalendo kweli auze shangingi lake litumike kulipia nauli za walimu na yeye apande daladala aone dhahama ilipo na wakati huohuo apendekeze mishahara ya wakuu wa wilaya ipunguzwe ili kupandisha mishahara ya waalimu, potelea mbali hata kama mapendekezo yake hayatatekelezwa lakini wangalau watu wataona uzalendo wake wa yeye kupakia daladala. Kama sio kusanifu watu na kutafuta sifa za kijinga ni nini. Wewe mkuu wa wilaya tena kijana unaenda kazini na kukata mitaa na shangingi linalokula mafuta kuliko tija yake, halafu ukawaombee watu wasafiri bure kwenye magari ya wafanya biashara na wakati huohuo unataka walipe kodi!!!