Makonda: Walimu kusafiri bure

structuralist

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,230
907
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.

Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa Rais mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa ana majukumu mengi hasa ya kumsaidia mheshimiwa Rais.

Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
 
Hao askari pamoja na ubabe wao,uniform na mamlaka bado wanaitwa "maiti' kwani sio hiari yao wenye mabus ndio itakuwa walimu wetu?
Atafute njia nyingine kuliko hiyo ambayo walimu wetu watanyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa mpaka watauchukia huo ualimu bure!
Wazo lake laweza zuri lakini sio kwa wakati huu
 
Hao askari pamoja na ubabe wao,uniform na mamlaka bado wanaitwa "maiti' kwani sio hiari yao wenye mabus ndio itakuwa walimu wetu?
Atafute njia nyingine kuliko hiyo ambayo walimu wetu watanyanyaswa, kutukanwa na kudhalilishwa mpaka watauchukia huo ualimu bure!
Wazo lake laweza zuri lakini sio kwa wakati huu
Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
 
Hebu afikiri critically. Hivi walimu wanachohitaji ni kulipiwa mia nne za nauli kweli? Amwambie mkurugenzi wake wa manispaa awalipe walimu wake madai yao ya likizo za dec 2013 na 2014 hadi dec 2015. Aanzishe miradi ya ujenzi wa nyumba za walimu aachane na madarasa na madawati na hilo ndio suluhu ya kuwahi kazini. Aache kufikiri kiduchu.
 
Tangu amesifiwa anajitahidi kuzidi kujitutumua, mwishowe ataharibu, sekta gani haina umuhimu? Hapo ni sawa Makonda kaiambia serikali wawaongee mshahara na marupurupu walimu, kwa hiyo kilio chao kimefikishwa serikalini kwa njiaa ya fumbo.
 
Hii itakuwa motisha au kumdhaalilisha mwalimu?Hebu fikirieni vizuri hili wazo.Walimu wajiandae kupachikwa majina ya hovyo hovyo na kudharaulika.
 
...mtafanyaje ili kondakta aridhike kumsafirisha mwalimu bure? na kwa nini manesi nao wasisafiri bure?, kwani wao hawana umuhimu kwenye jamii? na kwa nini mtu mwenye mshahara asafiri bure?,na kwa nini isiwe wanafunzi ndio wasafiri bure?
 
Kutekeleza wazo lake Walimu posho ya nauli kama wameshindwa kuwapa teaching allowances!
 
Makonda mbunifu, tumpe mda kabla yakuponda
Sioni namna ya waalimu kusafiri bure na wala hakuna sababu.

Hata hivyo, katika mfumo wa kisasa wa mtandao wa usafiri ambamo mtu anaweza kukata tiketi hata ya mwezi mzima au muhula mzima. Kama DART wana mfumo wa kisasa wa kukata tiketi hili linawezekana. Maana yake ni kwamba Makonda kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya kinondoni wanaweza kutenga fungu kwa ajili ya kulipa DART/UDA ili waalimu wenye tiketi hizo za kipindi fulani wasafiri bila shida.

Bure haiwezekani kabisa; siku zote yuko anayelipia gharama. Kama Makonda mpaka leo hajui kuwa hakuna huduma za bure basi sijui namna JPJM anaweza kumbeba.
 
Kawaida ya Walimu wanatakiwa kuishi kwenye mazingira ya shule, huko wanakoenda kuishi sidhani kama Serikali inawapangia Walimu wakaishi mtaani.
 
Lipeni waalimu stahiki zao kuliko danadana hizo nchi zinazojitambua hazichezi na mtu anaeitwa mwalimu anapata heshima kubwa na status ya maisha yenye heshima ila bongo hata laana yaeza kua wakuu hawa imewapata mwl haishi kupunjwa,kuonewa n.k lkn hawajajua km mwl akaamua atengeneze wajinga taifa halina msomi TZ muone aibu loh
 
Mkuu wa wilaya ya.kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.

Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa raisi mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa anamajukumu mengi hasa yakumsaidia mheshimiwa raisi.

Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu.au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
Huyo yupo kwenye usingizi wa pono,labda aende msoga aombe magari ya uda
 
Wataanza kuitwa chenga...
Angeongea na wenye maduka mitaani wawe wanawapa discount.
 
Tusubiri tuone atakavyofanya. Nawaza mabasi ya DART huingii kwa kituo bila smart card ya malipo.
 
Back
Top Bottom