Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,028
- 59,657
poa tu....sasa ikitokea kua gari Zima wamepanda walimu maana watakua hawana uniform itakuaje?
poa tu....sasa ikitokea kua gari Zima wamepanda walimu maana watakua hawana uniform itakuaje?
Madaktari ni watu muhimu zaidi kuliko waalimu... nao wasafiri bure tena wakiwa ndani ya mabasi wasisimame!!Kuna watu wao kila kitu lazima akiponde...
Madaktari ni watu muhimu kwa wagonjwa na sio kwa kila mtu... Hata wewe kama ni fundi umeme una umuhimu wako.. Kwa sababu ukizima umeme hao madaktari watachajia simu zao kwenye nini?Madaktari ni watu muhimu zaidi kuliko waalimu... nao wasafiri bure tena wakiwa ndani ya mabasi wasisimame!!
Yes i got you!Madaktari ni watu muhimu kwa wagonjwa na sio kwa kila mtu...
Gotcha?
Wanajeshi, Polisi na Askari Magereza wanasafiri bure. Sasa inapendekezwa Walimu nao wasafiri bure. Baadaye kidogo itapendekezwa Madaktari na Wauguzi nao wasafiri bure. Hautapita muda mrefu kila mtu atakuwa na kitambulisho cha Mwl au Daktari/Muuguzi.
Nani atalipa nauli kwenye daladala?
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.
Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa Rais mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa ana majukumu mengi hasa ya kumsaidia mheshimiwa Rais.
Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.
You are a great thinker! ni kweli kwamba hakuna huduma ya bure lazima kuna mtu mahali fulani anailipia. sasa kuwa na mpango wa kuwalipia walimu nauli kwenda na kurudi kazi inawezekana kwa kuweka mipango thabiti kama kuongea na makampuni yatakayo wasafirisha kisha wakalipwa baada ya kutoa huduma.Siyo lazima kila kitu tuige kwa wenzetu, vingine sisi wenyewe tunaweza kuvianzisha na wengine wakatuiga kama vinafanyakazi vizuri. kujenga nyumba karibu na shule kwasasa ni jambo gumu kwani shule nyingi hazina maeneo lakini pia walimu ni wengi sana mathalani unaweza kukuta shule moja ina walimu zaidi ya 100! kujenga nyumba hizo unahitaji fedha nyingi na eneo kubwa sana.Sioni namna ya waalimu kusafiri bure na wala hakuna sababu.
Hata hivyo, katika mfumo wa kisasa wa mtandao wa usafiri ambamo mtu anaweza kukata tiketi hata ya mwezi mzima au muhula mzima. Kama DART wana mfumo wa kisasa wa kukata tiketi hili linawezekana. Maana yake ni kwamba Makonda kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya kinondoni wanaweza kutenga fungu kwa ajili ya kulipa DART/UDA ili waalimu wenye tiketi hizo za kipindi fulani wasafiri bila shida.
Bure haiwezekani kabisa; siku zote yuko anayelipia gharama. Kama Makonda mpaka leo hajui kuwa hakuna huduma za bure basi sijui namna JPJM anaweza kumbeba.
Ubunifu upi? kama angekuwa mbunifu si angenunua magari yake yatoe huduma hiyo kwani ni wazi wanafunzi wanatozwa nauli halafu eti walimu wasafirishwe bure hayo magari ya baba yake? Ni wazi ukurupukaji unaendelea kwa hawa wateule wa Magufuli na sidhani kama tutafika salama.Makonda mbunifu, tumpe mda kabla yakuponda
Mkuu unataka nao wapande magar bureNgoja tumuite kwenye hafla ya kumuaga secretary wetu hapa
na machangudoa?Mwalimu huyu huyu au mwingine? Hakuna kitu kibaya kama kuwa biased, hivi Madaktari na Manesi nao hawastahili? Na wengine je?
The man has an idea. Ila tumeshauri sana, hakuna haja ya walimu kusafiri bure. Jaman kuna nyumba za national housing zilizo karibu na shule au umbali mfupi tu kwa kwenda shuleni, kwann isifanyike reallocation walimu wakakaa hapo badala wa wahindi ambao hawatoi huduma kama public servant? Mfano pale buguruni na manespaa ya ilala kuna shule hapo hapo kuna national housing toa raia wale weka walimu na wakbaini maeneo yote yenye fursa hizo biashara imekwisha. kupanda bure gari tumelipia TRA, load lience, mwarabu n.k? Usifanye tuanze kudharirishwa aiseh
hongera kwa point maridhawa hii. watu wengine toka wajue duniani kuna upinzani basi wao watapinga kila kitu ilimradi tu kiwe kimetolewa na upande usio wake. kimsingi Nchi hii ni yetu sote.hata walimu siyo wote ni ccm ila Makonda ameamua kuwajali kama kundi muhimu sana kwenye jamii yetu.kumwambia amekurukupa haikusaidii wewe wala Makonda.toa wazo mbadala ambalo linaleta workable solutionhapo utakuwa umelisaidia Taifa.Povu lanini mkuu, relax haiwezekani unachofikiria wewe ndo sahihi. Tumpe mda au tumshauri namna nyingine yakufanikisha coz nchi hii yetu sote bila kujali vyama
Unamsaidia mwalimu kwa kumuumiza mwenye gari. kwa nini msaada usitoke kwa mwenye kutaka kuutoa?Hii itakuwa motisha au kumdhaalilisha mwalimu?Hebu fikirieni vizuri hili wazo.Walimu wajiandae kupachikwa majina ya hovyo hovyo na kudharaulika.