Makonda: Walimu kusafiri bure

Makonda: Walimu kusafiri bure

Mwalimu kwanza wengine wafuate, hata ww umepata kufahamu kusoma na kuandika kwa kufundishwa na Mwalimu, na hata hao Dr, nurses, Prof. Wote wmefundishwa na Mwalimu!!
so kama kuna mgonjwa yuko hatarini kupoteza maisha ni heri afe kuliko mwalimu anaye wahi shule kushika namba kwa walio wahi na ku chelewa?
 
dawa pekee ya haki na heshima kwa walimu ni kuwaongezea pesa ya nauli kwenye mshahara wao , hili jambo ni udhalilishaji mkubwa sana , mwanafunzi alipe 200/- halafu mwl na midevu yake bure !
Yaani hapo sipati picha konda anataka nauli yake alafu unamwambia we mwalimu, anaanza kugomba sasa kwa sauti kubwa watu wote wanakugeukia wewe, utatamani uwe sisimizi
 
na walimu wa private school nao vipi amewafikiria katika mpango wake huu?
 
Kawaida ya Walimu wanatakiwa kuishi kwenye mazingira ya shule, huko wanakoenda kuishi sidhani kama Serikali inawapangia Walimu wakaishi mtaani.
Umesahau kuna walimu wameolewa na kuoa maasikali/manesi/ nawatu wengine? amabacho ni kikwazo kukaa amzingira ya shule?
 
Hapo kuna ubunifu gani?naona mnaota tu nani akubali kusafirisha walimu kwa agizo la makonda?makonda ni nani ndani ya taifa la tanzania?
Itakuwa nchi ya ajabu. sana! Yaani mtu akurupuke atoe agizo litekelezwe tu
 
Hapo kuna ubunifu gani?naona mnaota tu nani akubali kusafirisha walimu kwa agizo la makonda?makonda ni nani ndani ya taifa la tanzania?
Itakuwa nchi ya ajabu. sana! Yaani mtu akurupuke atoe agizo litekelezwe tu
 
Labda anamaanisha walimu watapewa transport allowance
 
Mwalimu huyu huyu au mwingine? Hakuna kitu kibaya kama kuwa biased, hivi Madaktari na Manesi nao hawastahili? Na wengine je?
Tuwe tunafikiria nje ya boksi kabla hatujapinga mambo ya msingi. Bila Mwalimu hao Madaktari na manesi wangefikia hapo walipo!!?????
 
vipi kuhusu walimu wa wilaya ya ilala, temeke na bara nao watakuwa katika mpango huo wa makonda au ni kinondoni tuu ndo wahusika?
Hakuna kitu kama hicho, yeye kaamua kuongea kwa kuwa ana mdomo tu. Kuna walimu wanafundisha kinondoni lakini hawaishi kinondoni na pia kuna walimu wanaishi kinondoni lakini wanafundisha wilaya nyingine Labda atoe hela ya mfukoni kwake awape walimu wanaofundisha shule za kinondoni.
 
Mpango mzuri saana...unatarajia kuanza lini..????pia usiwasahau madereva wa serikali...wafanyakazi wanaohudumia kivuko..Ferry..pale magogoni na askari wa zimamoto.Kuwahi kufika kazini kwa barabara zetu hakuna Guarantee.
 
Hebu ongezeni mishahara wa wafanyakazi wote wa umma, achen ujinga huu wa huyu bure yule alipe. Hiyo kodi mtawasamehe? Wanafunzi je?
Ongezeko la mshahara linategemeana na Kiwango cha ukuaji wa uchumi hivyo tukaze kwanza buti kwenye uzalishaji na exportn
 
Ongezeko la mshahara linategemeana na Kiwango cha ukuaji wa uchumi hivyo tukaze kwanza buti kwenye uzalishaji na exportn
Mi sio mchumi hivyo siwezi kujifanya naelewa sana. Ila kwa akili za kawaid bila shule, kama mapata ya serikali yanaongezeka kupitia kodi kama tunavyoelezwa, je haiwezi saidia kuongeza mishahara? Kama unataka uadilifu na ufanisi, je? motisha si utasaidia kwa watumishi wa umma?
 
Mi sio mchumi hivyo siwezi kujifanya naelewa sana. Ila kwa akili za kawaid bila shule, kama mapata ya serikali yanaongezeka kupitia kodi kama tunavyoelezwa, je haiwezi saidia kuongeza mishahara? Kama unataka uadilifu na ufanisi, je? motisha si utasaidia kwa watumishi wa umma?
Kuna baadhi ya kazi ukiwaongezea mshahara wataacha hio kazi zenyewe...polisi, waalimu .. Wanatakiwa waishi hivyo hivyo...
 
Tuwe tunafikiria nje ya boksi kabla hatujapinga mambo ya msingi. Bila Mwalimu hao Madaktari na manesi wangefikia hapo walipo!!?????
Ulivyoanza kuandika hivyo nikajua unakuja na bonge la point kumbe unaleta hadithi za kuku na yai kipi kilitangulia! Nadhani wewe ndio unatakiwa kufikiri not only nje ya box but mbali na box! Kwa hali ilivyo ukishaanza kuwabagua watendaji wako kwa kiwango hicho ni hatari sana, labda angesema within Manispaa ndio kuwe na incentives katika idara ya elimu especially kwa Walimu; yaani baadhi ya mafungu ya Walimu wanayokusanya yaidhinishwe kupewa motisha ambapo mambo hayo yasingeweza kuwagusa wengine maana huo ni uamuzi wa idara moja. Ila ukitoka na kusema mtoto huyu atapanda gari bure na wewe utalipia nauli while wote ni wako utakua unakosea sana. Nadhani nimewaza "ndani ya box" eeeghh??? Good morning Mpwa
 
DC Makonda hiyo sasa sifa,ukuu wa mkoa umeshapata kwa usafiri wa Waalimu sidhani kama utaweza,Anyway ngoja tukupe muda.
 
Walimu hawajapandishwa madaraja yao huu mwaka wa 4 katika halmashauri ya kinondoni. Mkuu wa wilaya upo! Leo unakuja na kupanda daladala bure kwa walimu badala ya kuwawezesha madaraja yao kwanza.

Hili ni jipu kinondoni. Mkoa wa Geita naupongeza sana walimu walipo fikisha miaka 3 madaraja yao yakapanda kwa nini hapo kinondoni mnashindwa kupandisha madaraja walimu huu mwaka wa nne unakwenda 5 sasa. Walimu wakiuliza mnasema eti andika barua sasa majukumu yenu hapo ni yapi?
 
Back
Top Bottom