Makonda: Nauli za mabasi yaendayo haraka zitaanza kutozwa Mei 16

Makonda naye kwa kutaka sifa! Hili suala ni la kiuendeshaji zaidi; sio la kisiasa. Kiki zingine bana! Zinawafaa wehu tu.
Mimi kama mtumiaji wa kila siku wa barabara ya Morogoro, naona bado kuna changamoto katika utoaji wa huduma hii kwa ufanisi. Tusubiri. Muda utasema zaidi.
 
20160511025340%2Bcopy.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.

Pia awaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka. Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa mabasi hayo kwa ajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwa ajili ya kusubiri magari.

Chanzo: Michuzi

Kumbe RC ndo msemaji mkuu wa DART enhee??
 
Mkuu mbona unaonekana ni mtu mwenye jazba...na chuki kali kwa ndugu Makonda.....mambo hayapo hivyo mkuu....si vyema kumchukia binadamu mwenzako kwa kiwango hicho hata kama kuna mambo mnadhindwa kuelewana....tujiunze kuvumiliana....hata kama tunatofautiana itikadi na maoni.....wanadamu hatuwezi kuwa na mawazo na fikra zinazofanana.....
Siasa za vyama zinawaondolea uwezo wa kufikiri, yeye anajua Makonda na wasaidizi wake wamejipanga vipi?. Mtanzania ni mjuaji wa kila kitu.
 
ituko..jpg

Kwa ufupi
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitangaza kuongeza siku tano za majaribio ya mabasi yaendayo haraka ili kuhakikisha wakazi wa jiji hilo wanapata elimu ya usafiri huo, vituko vimeendelea kuibuka ikiwamo kuvunjwa vishikio vya abiria wanaosimama.

By Jackline Masinde na Kelvin Matandiko, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitangaza kuongeza siku tano za majaribio ya mabasi yaendayo haraka ili kuhakikisha wakazi wa jiji hilo wanapata elimu ya usafiri huo, vituko vimeendelea kuibuka ikiwamo kuvunjwa vishikio vya abiria wanaosimama.

Usafiri huo ulipangwa kuanza rasmi leo kwa kutoza nauli, lakini Makonda baada ya kujionea changamoto kadhaa ikiwamo matumizi ya kadi, aliamua kuongeza muda huo.

Kabla ya uamuzi huo, mkuu huyo wa mkoa alishiriki kupanda mabasi hayo kwa kuanzia kituo cha Kariakoo hadi Kimara na Kimara hadi Morocco ili kujionea hali halisi.

“Nashangaa kuna watu wanapanda kwenye basi kuanzia asubuhi mpaka jioni wanazunguka tu na basi wengine wanaharibu baadhi ya vitu vikiwamo vishikio…Tujifunze kuwa na ustarabu mabasi yapo mengi hakuna haja ya kugombania,” alisema Makonda.

Alisema ameongeza muda huo kutokana na uelewa mdogo wa wakazi pia waendesha bodaboda, hata kwa watembea kwa miguu wanaokatiza barabara, bado wanahitaji kupata elimu ya kutosha.

Makonda aliwaonya madereva wa bodaboda na magari binafsi kuwa watachukuliwa hatua za kisheria wakiendelea kutumia barabara za mabasi hayo, ili kuepusha ajali.

Waandishi wetu walishuhudia wananchi wakigombana na kusukumana wengine waking’oa vishikio vya abiria wanaosimama ndani ya mabasi hayo, huku wengine wakibonyeza kengele za kuomba kushuka bila kukusudia.

Miongoni mwa vituko vilivyoonekana ni pamoja na abiria mmoja aliyekuwa akitoka Kituo cha Moroco Kwenda Kimara kuvunja kishikio hicho wakati akisukumana na mwenzake.

“Tangazo abiria tunaomba msiguse hizo kengere, ukibonyeza hapo unaonyesha unataka kushuka, pia msikae kwenye hiyo alama ya rangi ya bluu unahatarisha maisha yako,” alisema Jonathan Ng’andu dereva wa basi lililokuwa linatoka Kariakoo kwenda Kimara.

Mbali na vituko ndani ya basi, baadhi ya abiria walionekana wakivutana na walinzi wa Kampuni ya China-Tanzania Security (CTS) wakipinga kutumia madaraja makubwa kwa kuingia na kutoka katika vituo vya usafiri wakidai ni “usumbufu kupita juu ya daraja.”

Kila abiria aliyekuwa akitaka kuingia kwa njia ya mkato alirudishwa na walinzi, huku baadhi yao wakitoa kauli chafu za kutoridhishwa na utaratibu huo licha ya maofisa wengine kuendelea na utoaji elimu kwa wakati huo.

“Kaka hurusiwi kupita chini ya hizi mashine zinatumia umeme unaweza kusababisha hitilafu,” alisikika mmoja wa walinzi hao akimzuwia mwananchi aliyekuwa anawahi kupanda basi na kupita chini ya mashine hizo.

Siku tatu zilizopita, Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), Ronald Lwakatare alisema kuna wastani wa mabasi 140 yaliyotarajiwa kuanza kubeba abiria.

Hata hivyo, mbali na kuongezwa kwa siku hizo, abiria waliozungumza na gazeti hili jana, walitofautiana mtazamo baadhi wakitaka wachukuliwe hatua wanakiuka taratibu huku wengine wakiridhia.

Mkazi wa Tabata Kimanga, Rashid Hassan aliyekuwa akitokea Kariakoo kwenda Kimara alisema hatua ya kuongeza siku ni nzuri ili kujifunza kwa kuwa mfumo wa usafiri huo ni mpya hapa nchini. chanzo.Vituko mabasi yaendayo haraka Dar

WADANGANYIKA BADO TUKO NYUMA SANA ULAYA USAFIRI KAMA HUO ULIOKO NYUMBANI

NI KITU CHA KAWAIDA HAKUNA KUGOMBEA MABASI. LAKINI NYUMBANI TUNAGOMBEA

MABASI? AMA KWELI NG'OMBE MASIKINI HAWEZI KUZAA................
 
Unajua sababu za kugombea kupanda???
Unadhani enzi hizo yanaanza kutumika huko ulaya na wao walikuwa hawagombei????
TUNAGOMBANIA KUPANDA KWA SABABU NI BURE NA SIO USHAMBA
 
Huwa nasema kila siku, Tanzania tuna kila kitu lakini akili hatuna.

Kwanza napenda ieleweke, kwa sisi wa zamani mabasi makubwa kwa usafiri wa mjini Dar si kitu kipya, kipya ni hizo barabara tu kutenganishwa na kuwa za mabasi tu ili kuondoa msongamano.

Wale wenzangu wa zamani watakumbuka, kabla ya UDA kuleta ma Ikarus ambayo baadhi yalikuwa makubwa kama haya ya sasa na mengine yalikuwa marefu zaidi Ikarus "kumba kumba" yalikuwa ni basi na trailer lake yameunganishwa kitaalam hata ukiwa ndani au nje ya basi unaweza ukaliona ni refu tu lakini usihisi kama ni basi na trailer. Naam, kabla ya hapo tulikuwa na DMT, wazee wenzangu wanajuwa kirefu chake. Mabasi ya DMT yote yalikuwa makubwa na wale wengine watakumbuka mabasi ya ghorofa kama ya London. Nikiwaambia wanangu na wajukuu zangu kuhusu mabasi ya ghorofa kuwepo zamani Dar na kuwa nimeshayapanda huwa wananishangaa.
 
Sisi bure kabisa.
Hapo kwenye hizo machine za umeme,waachiwe wapite,akinaswa mmoja itakuwa fundisho.
Atakayenaswa maiti yake ipigwe picha halafu ibandikwe hapo wanapokomalia kupita
 
Mie jana nimepanda..., sasa yule dereva anatangaza jamani msishike mlango wala kusimama kwenye mstari wa njano haya Magari yanatumia umeme....

Milango hiyo inajifunga, huyp kaka yeye akaona anhaa wapi inakuwaje mlango ujifunge wenyewe, kwanino tusishike akashika.... sijui nini kilimpata full kupiga makelele.... wengine kubonyeza zile button kila mara sijui wanapenda kusikia inavyolia.. dereva wana kazi kwakweli...

Ila nimefurahia nimewahi kufika...muda mchache tu nimefika kwenye destination yangu
 
Huwa nasema kila siku, Tanzania tuna kila kitu lakini akili hatuna.

Kwanza napenda ieleweke, kwa sisi wa zamani mabasi makubwa kwa usafiri wa mjini Dar si kitu kipya, kipya ni hizo barabara tu kutenganishwa na kuwa za mabasi tu ili kuondoa msongamano.

Wale wenzangu wa zamani watakumbuka, kabla ya UDA kuleta ma Ikarus ambayo baadhi yalikuwa makubwa kama haya ya sasa na mengine yalikuwa marefu zaidi Ikarus "kumba kumba" yalikuwa ni basi na trailer lake yameunganishwa kitaalam hata ukiwa ndani au nje ya basi unaweza ukaliona ni refu tu lakini usihisi kama ni basi na trailer. Naam, kabla ya hapo tulikuwa na DMT, wazee wenzangu wanajuwa kirefu chake. Mabasi ya DMT yote yalikuwa makubwa na wale wengine watakumbuka mabasi ya ghorofa kama ya London. Nikiwaambia wanangu na wajukuu zangu kuhusu mabasi ya ghorofa kuwepo zamani Dar na kuwa nimeshayapanda huwa wananishangaa.
Kuna moja walikuwa limewekwa UDSM kama kumbukumbu. Naamini bado lipo
 
Wewe huna akili sio wote
 
Naomba kujuzwa hayo mabasi abiria wanaruhusiwa kuingia na mizigo manake niliona pale kivukoni watu wamebeba mavifurushi ya samaki.
 
Mie jana nimepanda..., sasa yule dereva anatangaza jamani msishike mlango wala kusimama kwenye mstari wa njano haya Magari yanatumia umeme....

Milango hiyo inajifunga, huyp kaka yeye akaona anhaa wapi inakuwaje mlango ujifunge wenyewe, kwanino tusishike akashika.... sijui nini kilimpata full kupiga makelele.... wengine kubonyeza zile button kila mara sijui wanapenda kusikia inavyolia.. dereva wana kazi kwakweli...

Ila nimefurahia nimewahi kufika...muda mchache tu nimefika kwenye destination yangu
Mpaka ipite kama mwaka ndo wataacha bwembwe
 
Huwa nasema kila siku, Tanzania tuna kila kitu lakini akili hatuna.

Kwanza napenda ieleweke, kwa sisi wa zamani mabasi makubwa kwa usafiri wa mjini Dar si kitu kipya, kipya ni hizo barabara tu kutenganishwa na kuwa za mabasi tu ili kuondoa msongamano.

Wale wenzangu wa zamani watakumbuka, kabla ya UDA kuleta ma Ikarus ambayo baadhi yalikuwa makubwa kama haya ya sasa na mengine yalikuwa marefu zaidi Ikarus "kumba kumba" yalikuwa ni basi na trailer lake yameunganishwa kitaalam hata ukiwa ndani au nje ya basi unaweza ukaliona ni refu tu lakini usihisi kama ni basi na trailer. Naam, kabla ya hapo tulikuwa na DMT, wazee wenzangu wanajuwa kirefu chake. Mabasi ya DMT yote yalikuwa makubwa na wale wengine watakumbuka mabasi ya ghorofa kama ya London. Nikiwaambia wanangu na wajukuu zangu kuhusu mabasi ya ghorofa kuwepo zamani Dar na kuwa nimeshayapanda huwa wananishangaa.
Leo umezungumza ukweli mtupu, upo msikitini nini
 
ni kweli mkuu...basi moja la ghorofa kama yale ya London bado lipo pale UDSM. Lipo karibu na mabwawa yale ya maji machafu...huwa nikiliona nakumbuka jinsi tulivorud nyuma kwenye sector ya usafir wa uma Dar es Salaam
 
Huwa nasema kila siku, Tanzania tuna kila kitu lakini akili hatuna.

Kwanza napenda ieleweke, kwa sisi wa zamani mabasi makubwa kwa usafiri wa mjini Dar si kitu kipya, kipya ni hizo barabara tu kutenganishwa na kuwa za mabasi tu ili kuondoa msongamano.

Wale wenzangu wa zamani watakumbuka, kabla ya UDA kuleta ma Ikarus ambayo baadhi yalikuwa makubwa kama haya ya sasa na mengine yalikuwa marefu zaidi Ikarus "kumba kumba" yalikuwa ni basi na trailer lake yameunganishwa kitaalam hata ukiwa ndani au nje ya basi unaweza ukaliona ni refu tu lakini usihisi kama ni basi na trailer. Naam, kabla ya hapo tulikuwa na DMT, wazee wenzangu wanajuwa kirefu chake. Mabasi ya DMT yote yalikuwa makubwa na wale wengine watakumbuka mabasi ya ghorofa kama ya London. Nikiwaambia wanangu na wajukuu zangu kuhusu mabasi ya ghorofa kuwepo zamani Dar na kuwa nimeshayapanda huwa wananishangaa.
Hayo mabas ya ghorofa huwa nikiwaambia rafiki zangu huwa wananibishia!
 
Dah umenikumbusha mbali sana mzee mwenzangu, nayakumbuka mno
 
Back
Top Bottom