Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.
Pia awaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka. Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa mabasi hayo kwa ajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwa ajili ya kusubiri magari.
Chanzo: Michuzi