amani ya kweli
Senior Member
- May 2, 2015
- 149
- 17
Hata msemeje ccm ni Chama dume
Hekima na busara ni kumbishia mtu na kuweka facts. Haya tuambie mshahara wa mkuu wa wilaya bei gani?
Hekima na busara ni kumbishia mtu na kuweka facts. Haya tuambie mshahara wa mkuu wa wilaya bei gani?
Mh. Paul Makonda,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,nakusalimu. Ndugu Makonda,umesikika ukisema kuwa umewaajiri wanasheria saba kwa kuwasaidia wananchi kwenye kuingia mikataba au kufungua kesi kwenye mahakama. Ingawa wazo na nia yako ni njema,umedhalilisha tasnia ya sheria.
Umesema kuwa unawalipa wanasheria hao asilimia sabini na tano ya mshahara wako kwa mwezi. Pamoja na kutojua mshahara wako kwa mwezi,nina hakika asilimia hiyo haiwezi kuwalipa wanasheria saba. Tasnia ya sheria ni moja ya tasnia kongwe,adhimu na ghali hapa duniani. Madai yako yanaidhalilisha tasnia hii ya sheria. Wanasheria saba walipwe asilimia 75 ya mshahara wako!? Hakika hiyo ni dharau.
Ndugu Makonda,najua wewe ni mwanasiasa na kiongozi wa kiserikali. Kauli zako zinapaswa kuchujwa vyema kabla ya kutolewa. Kwa taarifa yako,hakuna wanasheria saba wanaoweza kuajiriwa kwa mshahara wa kiudhalilishaji kama huo. Hata wanafunzi wa sheria huwezi kuwapata,seuse wanasheria.
Natoa rai kwako Ndugu Paul Makonda kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanasheria wa nchi hii kwa kauli yako ya kushusha thamani yao. Nikiwa mwanasheria,nimeshtushwa na kusikitishwa na kauli yako.
pamoja na kukosea kwake lakini mshahara wa mkuu wa wilaya hauwezi kuwa 2M,huyo mkuu wa idara tu anachukuwa 3M sembuse DC
sawa lakini ungepeleka jukwaa la sheria
wanasheria saba wanaolipwa na makonda wanaweza kuwa
1. petro mselewa
2. kimomogoro
3. prof. safari
4. kibatala
5. msemwa
6.nyange
7. Msando
kweli makonda unamshahara mkubwa aisee
Petro E. Mselewa
Kwani wanasheria hawawezi kufanya kazi kwa kujitolea na kulipwa mshahara mdogo?
Au bongo hamna Pro Bono?
Kuna wanasheria tunaendesha nao maguta huku mtaaani ,wanatamani hata job ya 350 kwa mwezi!!
WatashIndwa kuajiriwa Na Paul?
Acheni kujiona nyie waajabu sana!!
Petro E. Mselewa
Mr. Mselewa, na wewe sheria umejifunzia wapi? Kama mwanasheria unawezaje kutoa statement kama uliyotoa bila kuwa na facts? Umeshaona terms za contract ya Mh. Makonda na hao wanasheria? Kwa sababu wewe una assumption kuwa wanasheria wanalipwa hela nyingi sana umeshindwa kujua kuwa kibarua chochote ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anajua hicho. Nikiwa na kesi nitajitahidi kukwepa wanasheria kama wewe.
Nilifungua huu uzi kwa kasi nikitaka kujua Makonda ameongea nn tena. Mtoa mada sioni kama hoja yako ina mashiko sana, nafahamu fika ada za wanasheria ni kubwa. Na pia nafahamu inawezekana kabisa mwanasheria akatoa huduma kwa bei pungufu kutokana na utu/(bonafide) au harakati zake (hakuna bei maalum iliyopangwa). Katika mambo ya kukomalia kwenye hii nchi (maana ni mengi aisee) sioni sababu ya kumkomalia Makonda aombe radhi.
Huyu mwansheria wa JF kakurupuka.as long as huyo DC hajatoa specifics huwezi kum-pin down based on vague statements.hata hiyo kada ya sharia wana madaraka tofauti.sidhani kama paralegals wanalipwa sawa na advocates,n.k,au fresh graduates sidhani kama wana malipi sawa na wakongwe.ingehitaji ujue details za kutosha kabla ya kuna na hii conclusion kuwa taaluna imedhalilishwa.
Mh. Paul Makonda,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,nakusalimu. Ndugu Makonda,umesikika ukisema kuwa umewaajiri wanasheria saba kwa kuwasaidia wananchi kwenye kuingia mikataba au kufungua kesi kwenye mahakama. Ingawa wazo na nia yako ni njema,umedhalilisha tasnia ya sheria.
Umesema kuwa unawalipa wanasheria hao asilimia sabini na tano ya mshahara wako kwa mwezi. Pamoja na kutojua mshahara wako kwa mwezi,nina hakika asilimia hiyo haiwezi kuwalipa wanasheria saba. Tasnia ya sheria ni moja ya tasnia kongwe,adhimu na ghali hapa duniani. Madai yako yanaidhalilisha tasnia hii ya sheria. Wanasheria saba walipwe asilimia 75 ya mshahara wako!? Hakika hiyo ni dharau.
Ndugu Makonda,najua wewe ni mwanasiasa na kiongozi wa kiserikali. Kauli zako zinapaswa kuchujwa vyema kabla ya kutolewa. Kwa taarifa yako,hakuna wanasheria saba wanaoweza kuajiriwa kwa mshahara wa kiudhalilishaji kama huo. Hata wanafunzi wa sheria huwezi kuwapata,seuse wanasheria.
Natoa rai kwako Ndugu Paul Makonda kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanasheria wa nchi hii kwa kauli yako ya kushusha thamani yao. Nikiwa mwanasheria,nimeshtushwa na kusikitishwa na kauli yako.
Petro E. Mselewa
Huyu ndugu yetu Makonda kwa dharau zake hizi atakuja kuishia hewani Kama Rafiki yake Mrisho Ngumbo aliyepata kumtukana mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya korogwe kwa kuishuia elimu yake hadhi. Mbaya zaidi akawatukana wanaume na wana wake wote wa kaskazini kwamba hawana uwezo wa kuzaa mtu atakayeweza kuwa Rais kupitia ile kauli yake kongwe na iliyojaa kejeli alipokuwa na wenzake wa UVCCM mkoa Pwani kuwa " Rais hawezi kutoka kaskazini"
Hawa ni vijana wadogo Mungu awape busara na maisha marefu ili waweze kujifunza busara na kuweka akiba ya Maneno yao.