Ni kweli Makonda kama DC wa kinondoni ana timu ya wanasheria ofisini inayomsaidia kutatua kero za migogoro ya Ardh kwa jamii. Alipotangaza kuwasaidia wakazi wa wilaya yke kwa mwezi mmoja alijikuta anapokea wateja takribani 1,500 kwa mwezi. Kutokana na wingi wa watu wenye kero na migogoro pamoja uelewa Mdogo wa sheria alipokea ushauri kutoka kwa mawakili maarufu majina yao siyataji kuwaatafute timu ya wanasheria.Makonda alifanya hhivyo, akaunda timu ya wanasheria akawaomba wamsaidie kutoa HUDUMA YA KISHERIA. Kitaalam timu hiyo inatoa msaada wa kisheria ( legal aid) "probono". Naamini wanachofanya wanasheria hao siyo dhambi wala kinyume cha sheria. Timu hiyo awajapewa mikataba ya kazi au ajira na Makonda wala Wilaya.Nadhan alitumia maneno hayo kuongeza umaarufu wa kisiasa katka jamii na kupanua wigo wa kijulikana.Tusiwabeze wanasheria wanatoa HUDUMA kwenye jamii