Makonda, Jitokeze hadharani utuombe radhi wanasheria

Makonda, Jitokeze hadharani utuombe radhi wanasheria

Hapo umetoka kidogo mkuu,utetezi wako hauna mashiko New York na kinondoni ni tofauti saaaaaaanaaaa

Umetoka wewe kwa kuogopa jina la New York wakati habari ni ile ile.

Kinondoni Pro bono haiwezekani?
 
William Malecela ....ni wewe umeandika haya au Mtu kaiba password ? Mimi nikifikiri umekulia " Ikulu " utajuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu ..Hivi DC akaajiri wanasheria kwa mshahara wake na ofisi ya mwanasheria wa wilaya inafanya nini ?? Ofisi ya Mwanasheria wa Manispaa ?? Ofisi za NGo za misaada ya kisheria zippo tele ....
Tiachenj cheap popularity ....Kama ubunge wa Kinondoni naamini atapata bila kufanya hayo ..kwa Kuwa Huyo Iddi Azzan hamuwezi

Makonda hajui anayoyaongea... Pengne anaweza asijue nini anayopaswa kufanya.
 
Mh. Paul Makonda,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,nakusalimu. Ndugu Makonda,umesikika ukisema kuwa umewaajiri wanasheria saba kwa kuwasaidia wananchi kwenye kuingia mikataba au kufungua kesi kwenye mahakama. Ingawa wazo na nia yako ni njema,umedhalilisha tasnia ya sheria.

Umesema kuwa unawalipa wanasheria hao asilimia sabini na tano ya mshahara wako kwa mwezi. Pamoja na kutojua mshahara wako kwa mwezi,nina hakika asilimia hiyo haiwezi kuwalipa wanasheria saba. Tasnia ya sheria ni moja ya tasnia kongwe,adhimu na ghali hapa duniani. Madai yako yanaidhalilisha tasnia hii ya sheria. Wanasheria saba walipwe asilimia 75 ya mshahara wako!? Hakika hiyo ni dharau.

Ndugu Makonda,najua wewe ni mwanasiasa na kiongozi wa kiserikali. Kauli zako zinapaswa kuchujwa vyema kabla ya kutolewa. Kwa taarifa yako,hakuna wanasheria saba wanaoweza kuajiriwa kwa mshahara wa kiudhalilishaji kama huo. Hata wanafunzi wa sheria huwezi kuwapata,seuse wanasheria.

Natoa rai kwako Ndugu Paul Makonda kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanasheria wa nchi hii kwa kauli yako ya kushusha thamani yao. Nikiwa mwanasheria,nimeshtushwa na kusikitishwa na kauli yako.
acha dharau. kwani hao aliokubaliana nao malipo hawana uwezo wa kufikiri. kwa nini unapinga hayo makubaliano yao. kama una proof ya ukweli tuambie lakini sio kutuambia mambo hewa mzee. kajipange tena wewe ndio umwombe radhi kwa kuingilia mkataba wao, kwani haukuhusu kabisa
 
acha dharau. kwani hao aliokubaliana nao malipo hawana uwezo wa kufikiri. kwa nini unapinga hayo makubaliano yao. kama una proof ya ukweli tuambie lakini sio kutuambia mambo hewa mzee. kajipange tena wewe ndio umwombe radhi kwa kuingilia mkataba wao, kwani haukuhusu kabisa


wanasheria waserikali tayari wameshaajiriwa... kwa nn asiwatumie waliokuwepo?

usitetee upuuz
 
Back
Top Bottom