Makonda is almost so damn right!

Makonda is almost so damn right!

Status
Not open for further replies.
Yaani huyo kijana andharau na ulimbukeni anavaaje nguo ya disco kwenye msiba alafu anaingia nayo kanisani?.
 
Wadau wa JF,

Habari za masiku wandugu, hongereni na changamoto za maisha. Kuna mambo yananifikirisha sana kuhusu kiongozi wetu mchapakazi na kipenzi cha watu.

Hasa baada ya kushutumiwa katika sekeseke la ubaguzi kutokana na kauli zake. Kwa kifupi katika msiba wa Daktari Mengi ambaye amelala kwenye nyumba yake ya milele, na Mungu ampuzishe salama, Amina. Msiba huu mzee wetu aliagwa karimjee na mkuu wa mkoa alisimamia msiba huu na mambo yakaenda vizuri ukiachana na kauli yake.

Sasa swali langu la kufikirisha ni kwa nini huyu kiongozi wetu aliuacha mkoa wake na kwenda kilimanjaro kumzika wakati alishamuaga dar? Maana picha zake na mavazi aliyovaa akiwa katika msiba tena kanisani, zinanifanya nijiulize kama kweli alidhamiria kwenda kumzika mzee wetu.

Fikra ingine ni kuwa hata mimi nilikuwa sipajui kwa mzee mengi kama amejenga ghorofa 3, kama ambavyo nimeshuhudia kwenye mtandao, pengine msiba huu unaweza ukawa ni fursa kujua makazi ya mengi aliyojenga ni kwamba pamekaaje.

Yangu ni hayo tu, tuendelee kuijenga tanzania ya viwanda kwa kumuenzi mzalendo na muungwana mzee wetu Daktari

Reginald Abraham Mengi
 
Ninadhani hata yeye sasa hivi anajiuliza ni kwanini alikwenda Kilimanjaro kwenye msiba wa Mengi. Tungeweza ku re wind muda sidhani kama kingetokea tena hili.
 
Wakuu, Kwa ujumla mimi huwa ni Mshabiki wa Makonda kindakindaki ila kufuatia Msiba wa Mengi! Makonda alikosea katika maeneo yafuatayo!

1. Hakupaswa kuhusisha Msiba wa Mengi na tabia za Wachaga!

2. Hakupaswa kutangaza Deni la Kubenea hadharani maana Mkopo ni Siri ya Mkopaji na Mkopeshaji, na kwa kuwa Mkopeshaji hayupo basi angemkumbusha mkopaji kwa njia ya kistaarabu.

3. Hakupaswa kuvaa Mavazi yale aliyovaa Msibani Maana yanaashilia Uhuni, Usanii, au tunawea kuuita Utoto.

4. Hakupaswa kujitetea Baada ya SG Bashiru kumuombea msamaha pale Kanisani.

5. Hakupaswa kusita kuitika wito Baada ya kuitwa na Askofu pale Kanisani.

Huo ni mtazamo wangu tu! Japo na sisi walalamikaji tungeweza kunyamanza kimya pasingekuwepo na Mjandala wowote na wala tusinge athirika kwa Sababu hakuna ubishi kwamba katika Makabila ya Tanzania Wachanga wanachukua nafasi ya 1 kwa Utafutaji wa Pesa

Mkuu naongezea no,6---- Hata alipopewa nafasi ya kujieleza/ kujitetea pale madhabauni alizidi kutonesha majeraha kwa walengwa kwa kusema; "Alimsifia mchaga miongoni mwa wachaga". na wala siyo "alimsifia marehemu miongoni mwa Watanzania".🤔🤔
 
Back
Top Bottom