Wakuu, Kwa ujumla mimi huwa ni Mshabiki wa Makonda kindakindaki ila kufuatia Msiba wa Mengi! Makonda alikosea katika maeneo yafuatayo!
1. Hakupaswa kuhusisha Msiba wa Mengi na tabia za Wachaga!
2. Hakupaswa kutangaza Deni la Kubenea hadharani maana Mkopo ni Siri ya Mkopaji na Mkopeshaji, na kwa kuwa Mkopeshaji hayupo basi angemkumbusha mkopaji kwa njia ya kistaarabu.
3. Hakupaswa kuvaa Mavazi yale aliyovaa Msibani Maana yanaashilia Uhuni, Usanii, au tunawea kuuita Utoto.
4. Hakupaswa kujitetea Baada ya SG Bashiru kumuombea msamaha pale Kanisani.
5. Hakupaswa kusita kuitika wito Baada ya kuitwa na Askofu pale Kanisani.
Huo ni mtazamo wangu tu! Japo na sisi walalamikaji tungeweza kunyamanza kimya pasingekuwepo na Mjandala wowote na wala tusinge athirika kwa Sababu hakuna ubishi kwamba katika Makabila ya Tanzania Wachanga wanachukua nafasi ya 1 kwa Utafutaji wa Pesa