Makonda ni Trump wa CCM... Ole wetu!!

Makonda ni Trump wa CCM... Ole wetu!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,838
Reaction score
50,543
Kuna nyakati huwa sielewi ni kwa nini Kuna mfanano wa karibu sana Kati ya ambayo hutokea kwenye siasa za Tanzania na Marekani.

Tarehe 18/05/2009 Jakaya Mrisho kikwete akiwa Rais wa Tanzania, alikuwa ndiye kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukutana na Obama tangu alipochaguliwa mwaka 2008. Ilishangaza kweli kweli.

Kabla ya kukutana na Kikwete Obama alikutana na viongozi toka mataifa yale tu yenye manufaa na maslahi makubwa kwa Marekani.

Leo Marekani inaongozwa na Donald Trump mmarekani ambaye anavunja kila tamaduni ya kiuongozi iliyowekwa kwenye nchi hiyo.

Trump hajawahi kuwa na historia yoyote ile ya kimaadili wala kiungozi... Lakini wamarekani wamemchagua mara mbili.

CCM kwa sasa imepwaya Sana kihaiba na watu wenye sifa za kimaadili mbele ya jamii hawapo. Huwezi pata mtu ndani ya CCM anayeaminiwa na watanzania kwamba ana maadili yanayofaa kuwa kiongozi.

Lakini kama ilivyokuwa kwa Republicans wa Marekani kuwa na Trump, CCM nao wanaye Paul Makonda.

Watu wengi wasioyaangalia mambo kwa kina hawaoni jinsi Makonda anavyoichora ramani yake ya kufanya CCM isiwe na mbadala mwingine ndani ya chama hicho zaidi yake.

Pamoja na shutuma zote anazoelekezewa Makonda, bado yeye kila wakati anaonekana kama nyota ing'aayo ndani ya CCM.

Mzee njaa a.k.a Pascal Mayalla alishawahi kuandika bandiko lake kuhusu Makonda, ukilisoma ukiwa umemakinika, utaelewa ninachosema.

Hofu yangu tusiporekebisha mifumo yetu ya kiuchaguzi, iko siku Makonda atakuwa Rais wa nchi yetu. Na siku hiyo ikifika... OLE WETU!
 
Bashite akishika nchi na mimi nakimbia nchi atatudunda mangumi yule jamaa siyo kabisa
 
Makonda hana hiyo nyota wala nini ni kubebwa bebwa tu, ila kwenye chaguzi zilizo huru na haki hawezi penya.

Tatizo CCM imepoteza identity na siku zinavyokwenda inazidi kupoteza sura ya corporate organization inayo reflect stability and maturity bali imekua a rogue mafia fraternity.

Na haya yote bila kuandaa katiba mpya ya wananchi basi 2030 itakua worse na nchi itageuka Somalia!!
 
Makonda hamzidi Trump kwa kubebwa... Kama Maigizo anayoyafanya Makonda kujidai ni mtu wa dini, ndivyo naye Trump alifanya mapaka leo bado yupo Ikulu ya Marekani.

Juzijuzi tu hapa kabomoa sehemu ya jengo la Ikulu ya Marekani, kafanywa nini? Trump anabebwa Sana.
 
Makonda hana hiyo nyota wala nini ni kubebwa bebwa tu, ila kwenye chaguzi zilizo huru na haki hawezi penya.

Tatizo CCM imepoteza identity na siku zinavyokwenda inazidi kupoteza sura ya corporate organization inayo reflect stability and maturity bali imekua a rogue mafia fraternity.

Na haya yote bila kuandaa katiba mpya ya wananchi basi 2030 itakua worse na nchi itageuka Somalia!!
somalia katika muktadha upi
 
Trump ana maadili ya mlengo wa kulia(far right/reactionary) ambayo yamefanya wamarekani wengi wampende.

Makonda hana chochote zaidi ya ushawishi chamani. Hana cha kuwauzia wananchi.

Makonda hawezi kuchukua nchi kidemokrasia kama Trump.
 
Mzee Pascal Mayalla alishawahi kuandika bandiko lake kuhusu Makonda, ukilisoma ukiwa umemakinika, utaelewa ninachosema.

Hofu yangu tusiporekebisha mifumo yetu ya kiuchaguzi, iko siku Makonda atakuwa Rais wa nchi yetu. Na siku hiyo ikifika... OLE WETU!
Pascal Mayalla, njoo uthibitishe.
Nathibitisha
  1. Kwanza naomba kukiri, huyu dogo, mimi namkubali sana kitambo, ni mimi ndiye nilimuumbia u RC Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
  2. Ni mtu mwenye upako Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
  3. Ilikuwa Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!
  4. Ndipo JPM akaamua kurejea kupitia kwake Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?
  5. Ni mpakwa mafuta wa Bwana Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Anayeziweka serikali za mataifa ni YEYE, hivyo urais unapangwa na YEYE na unatolewa kwa yeyote YEYE aliyempangia, kama ni yeye ndie aliyepangiwa na YEYE, then ni yeye!.

P.
 
Thanks.
 
Back
Top Bottom