Makonda: Hii dunia sio mali ya Mungu

Makonda: Hii dunia sio mali ya Mungu

Kwa mujibu wa biblia Makonda yuko sahihi maana ni biblia hiyohiyo imemtaja Shetani kuwa baba wa ulimwengu huu. Maana ya baba wa ulimwengu ni mwenye mamlaka ya juu hapa Duniani. Tusome biblia zetu vizuri jamani. Ni kweli kuwa Mungu aliumba mbingu na nchi/Dunia lkn baada ya uasi shetani alijitwalia sehemu kubwa ya uongozi wa Dunia hii na ndomana hata katika biblia hiyohiyo baada ya Yesu kutoka mlimani kwenye mfungo wa siku 40 alijaribiwa na shetanji kwa namna tofautitofauti ikiwa ni pamoja na kuahidiwa Mali zote za Dunia hii endapo angekubali kumuabudu shetani! Ni nani aweza kuahidi kutoa mali asiyokuwa na mamlaka nayo!!? Mpaka hapo tunagundua kuwa shetani alikuwa na ana mamlaka ya juu hapa Duniani, maana kama ameweza kumjaribu na kumshawishi Yesu kristo ambaye kwetu Wakristo ni Mwana wa Mungu, Bwana na mwokozi wa maisha yetu basi shetani yu'na mamlaka ya juu sana hapa Duniani.
Tusome biblia zetu jamani.
tatizo walokole mnamtaja sn shetani mpka mnajisahau mnadhani ndiye mtawala wa ulimwengu.... Yesu ameukimboa ulimwengu kwa kuteswa, kufa na kufufuka kwake, sasa wewe huyo shetani wako anatawala wapi?
 
Wapo viongozi wakubwa waliotoa kauli kama hizi mwisho wa siku wakatembelea ndala, Mungu hadhihakiwi aisee! Mwambieni vyote alivyojikusanyia ni vya kupita tu!
 
Bado miaka nane tu....JPM ataondoka....mkuu wa mkoa nae ajiandae kuondoka nae...JPM mwenzake atakua anastaafu..sijui yeye atakua anaenda kufanya nn?
Kwa hizi sifa wanazotaka kwa pupa hata miaka hii mitano kuimaliza ni kiza kinene. Tuwape muda.
 
Vita vyetu si vya damu na nyama....ni juu ya nini vile!he may be right .
 



Mpelekeeni taatifa Mkuu wa mkoa wa dar es salaam mwambieni kwa niaba ya watumishi wote duniani nampinga kwa maandiko zaidi ya saba yanayokanusha uongo aliouongea hadharani:-

1.kwanza hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na dunia.

2.Baba anaitwa Muumba wa mbingu na nchi (dunia)

3.Isaya 45:18
Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

4.Isaya 66:1
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu......

5.Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

6.Paulo anasema katika Waefeso 3:14-15
Kwa hiyo nampigia Baba magoti,ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,

7.makonda asichanganye maandiko ,MUNGU anasema anatawala mbinguni na duniani ,maana yake utawala wake upo hapa tayari,dola ipo hapa,usalama wa taifa la duniani tuko hapa tukishirikiana na usalama wa mbinguni......mwambieni aendelee
tu na siasa ,mambo ya MUNGU atuachie tunaotetea maslahi ya MUNGU wa mbingu na dunia!

Nukuu toka kwa Kuhani Philemon Mwansepe

(Zab 24:1)Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

The earth is the LORD' s, and the fulness thereof; the world, and they that dwell therein.

MITHALI 16:18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.

Huyu jamaa nikilaza to the maxmum
 
Huyu bwana mdogo ameenda mbali kwa kusema hii dunia sio ya mwenyezi Mungu. Je nani muumba wa dunia hii na viumbe vilivyomo. Ni kosa kutafuta kiki za kisiasa kwa kumhusisha Mwenyezi Mungu.
Mtu akishajiita Mungu ogopa sana kumsikiliza kauli zake.
 
Dunia na vyote vijazavyo dunia ni mali ya BWANA.

Anataka kutuambia kuwa dunia imeumbwa na yeye pamoja na baba'ke wa kufikia??

Anayepinga hilo amelaaniwa yeye na ukoo wake wote!
 
Sijui ni msaada wa Albadir au inatokea tu. Tunaweza kuwa tunaishi na watu huku 95% tukijua dunia ni ya Mungu wakati huo huo kuna 2% wanaomjua mmiliki mwingine, kibaya haya ni kuchanganyika hizi aina mbili.
 
"Dunia na vyote viijazayo ni mali ya Mungu asema Bwana" kumbe Bashite zero hadi kwenye Bible!
 
Na bibi yako

Ya bibi yangu, ni miaka mi2 tu na sehemu ndiyo aliyobakisha na hii ni iwapo to miungu yake itapenda na kuendelea kumvumilia.....

Hiyo minane nasisitiza tena kuwa labda ni ya kwako na kwa mujibu wa katiba ya ukoo wako....!!

The fact ni kwamba, hakuna terms za miaka nane nane ya Rais wa Tanzania kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977 kukaa madarakani kabla ya uchaguzi mwingine kufanyika....!!

Kubali tu kuwa umechemka boss na mimi kukukosoa kwa kukusanifu kidogo....
 
Ya bibi yangu, ni miaka mi2 tu na sehemu ndiyo aliyobakisha na hii ni iwapo to miungu yake itapenda na kuendelea kumvumilia.....

Hiyo minane nasisitiza tena kuwa labda ni ya kwako na ukoo wako....!!

Hakuna terms za miaka nane nane ya Rais kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977 kukaa madarakani before the next election....!!

Kubali tu kuwa umechemka boss na mimi kukukosoa kwa kukusanifu kidogo....
Mkuu endelea kujitoa ufahamu tu na kubishana vitu vidogo......
 
Back
Top Bottom