Jaman mambo mengine sio ya kupost humu, kwanza unapoandika vile ni dhahiri kuwa umefurahishwa na kitendo cha huyo binti, pia mi sioni kosa la makonda kusema makosa na ubadhilifu wa kabwe uliopelekea mpaka kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pia ieleweke kuwa kazi ya kutumikia umma huhitaji mhusika awe na uadilifu kwa umma.
Kabwe amefanya kazi kama mkurugenzi kwa mkoa wa mwanza, mbeya na dar lakini udhaifu mkubwa ulionekana ukiambatana na ubadhilifu, kusimamishwa kazi kusiwe sababu ya kumuona kuwa alikuwa mwema mno kiasi cha kumuona makonda kama kihelehele kwani naamini aliyafanya yote hayo kwa faida ya wanadaresalaam wote hata watanzania kwa ujumla.
Kila kifo kina sababu zake, kama inasemekana tayari alikuwa mgonjwa, je haikupaswa kumsimamisha kazi kisa mgonjwa kwa kuhofia atafariki? Tuacheni unafiki wa kuwa vigeugeu wasioeleweka, baadhi mlilalamika kuwa marehemu alikuwa tatzo leo tena lawama kwa makonda?
R.I.P KABWE