Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Damu nzito kuliko maji,niliwahi kukaa na jamaa baba yake ni mlevi sana,lkn alikuwa hakosi kuwalea watoto wake vizuri,kuna siku tunapita sehemu tukakuta watu wanapiga kelele eneo la Bar,ikabidi tupite kutazama,kufika pale tukakuta baba wa jamaa amelewa chakari,kajikojolea na amelala fofofo
Barmaid anamvuta kumuamsha Mzee wafunge Bar...huku akitoa maneno makali na kumzaba makofi.Damu nzito kuliko maji,Jamaa alitembeza kichapo kwa bar maid na waliokuwa wanamgasi Mzee,akamchukua mzee kwenye Tax hadi home
Ni kweli tupu Mkuu,
Umenikumbusha matani ya utotoni, maisha ya kwenye Quarter, Kuna watoto walikuwa wanapigana wakitaniwa baba zao, Unakuta Baba analewa mchana kweupe halafu anakusanya watoto anatoa vituko, wengine hudiriki kwenda haja ndogo hadharani, wenye baba zao ilikuwa ni ugomvi kwa kwenda mbele wanapotaniwa. Mwingine unakuta baba kikojozi! Na mtaani watu wanajua, Hapo ilikuwa ni kushuhudia ngumi kila mara! Utani.
 
makonda anaweza kuwa raisi Wa ccm siku moja maana hana aibu...
 
Mi nafikiri masuala ya misiba na kazi ni tofauti kabisa. Yote yaliyotokea yalikua masuala ya kiofisi zaid, but kwenye msiba kwa vile makonda alifanya nae kazi yule mzee alikua na 7b zote kuhudhuria. Ata ivo kwa mtazamo wang mimi uyo bint nahis ndo hakua mstaarab kumkatalia kumpa mkono. Na ata hao wanaohisi kua makonda kakosea asingekwenda wangedai kafurahia msiba wa kabwe ndo mana hakwenda ata kwenye mazko ake. Mi nafikir tunatakuwa tumpongeze mh mskonda kwa kuonyesha uungwana wa hali ya juu na kuhudhuria mcbani kwa aliyekua mtumish wake.. Kwan kaonyesha kua yeye hakua na kinyongo nae bt yaliyotokea ilikua ni ishu za kazi tuuuu.. Big up man makonda...
 
Bakiza maneno. Kwa binti yule ni baba yake na alitumbuliwa hadharani na hilo hakufurahia na angekuwa mnafiki kama angetoa mkono. Ni wachache wetu wanaojua wazazi wao wanafanya nini na wawe na uwezo wa kuwadhibiti. Pia kuna issue ya Kabwe jinsi alivyotumbuliwa hasa kama walikua na taarifa ni mgonjwa (sisemi asingetumbuliwa). Makonda ana system amabayo nina hakika ilijua au ilikua na uwezo wa kupima aina ya mapokezi ambayo angepata kwa ya yeye kwenda pale. Kama kiongozi alifanya uamuzi akaenda hayo mengine ni historia. Bahati mbaya wengi hapa wanajadili kivyama zaidi. Familia ina watu wangapi na waliokataa kumpa mono ni wangapi? Je ni lazima kila mmoja ampe mkono hata yule anaeamini kwamba jamaa huenda kamuwahusha dingi safari au kamdhalilisha dingi?
Haiwezekani mtoto usijue nyendo za mzazi wako. Cha msingi watu wengi huwalinda wa kwao hata kama ni waharifu na hilo ni kosa. Tusiwe na mazoea ya kula tu na kutohoji unavyokula vinatoka wapi?
 
Binti wa aliyekuwa mkurugenzi wa jijj la dar es salaam marehemu Kabwe amchunia RC Makonda.

Hata mim siyo kumchunia bali hata kwetu asingekanyaga. Naweza sema hata kama Kabwe alikuwa anaumwa but kifo chake kimesababishwa/kimeharakishwa na changamoto za kibinadamu alizozipata baada ya Makonda kusababisha atumbuliwe.

RIP KABWE.
....kweli kuna watu wameksa mshipa wa aibu...huyu makonda hana aibu kabisa....na wengi huko ccm wako hivyo...Huwezi kuhudhuria msiba wa mtu uliyechangia kumfuta kazi kwa aibu mbele ya umma...alafu we bila chembe ya aibu unahudhuria msiba wake...unafiki wa ajabu....Nimemwelewa JPM kwa kutohudhuria msiba huu...Inauma kwa wanafamilia sana....
 
Nawashangaa wanao "msupport" Makonda. Unajua fika uwepo wako msibani utakuwa shida, kwanini asiende muwakilishi?

Kwanza huyo mtoto mstaarabu, kumuacha hata akanyage nyumbani kwao. Akili za darasani tukose na "common sense" pia? Tunajifanya malaika fulani...angekuwa yeye ndio huyo binti angejisikiaje?

Eti Mkuu wa mkoa? Ebooo.
Na ndio maana mkuu wa Kaya hajaenda kamtuma waziri wakati yeye huwa anaenda sana misibani
 
Hii ni vita ya familia ya makonda na kabwe na sio serikali. hata vizazi vijazo yani watoto,wajukuu na vitukuu huko mbele vitaendeleza.
Sababu tayari mtu (kiini cha ugomvi na suluhisho) wa upande mmoja amefariki. hivyo huo ugomvi ulikuwa umalizwe na wao wawili lakini haiwezekani.na ni vigumu hata ndugu kuumaliza kwani kil .
Uko saw a hata vijijini tunakotoka kuna familia haziongeo Kwa Ajili ya ugomvi wa vizazi ...Ndio maana wanashauri ukihisi ulimkosea mtu muombe radhi kabla hajakata roho,baadhi ya mila za kiarabu waliokosana na marehemu hugslagala na Kulia pembeni ya maiti kabla haijatolewa NJE kuzikwa
Makinda kama anaajua ali kosahakutakiwa kutoa Maneno matamu Msibani Bali angemfuata hospitali kutaka radhi
 
Mimi naomba niongee kitu kuhusu mtoto wa Kabwe kukataa kupokea salamu za mkuu Makonda, nadhani huyu dada hakufanya vizuri hata kidogo!!! Hivi Mtoto wako au Kaka yako au Hata baba, akifanya mambo mabaya inapaswa asiambiwe au asiadhibiwe?? Jamani Watanzania tunaenda wapi iwapo kila Siku tunalia haki hazitendeki kila idara sasa huyu Marehememu alitendewa haki au alionewa?? Jamani tunaenda wapi??je ukimuona mtoto wa Jirani yako anatenda mabaya ukamkanya ubaya unageuka kwa mkanyaji ndivyo ilivyo kweli !!!!
 
hakuna ilik
Mi nafikiri masuala ya misiba na kazi ni tofauti kabisa. Yote yaliyotokea yalikua masuala ya kiofisi zaid, but kwenye msiba kwa vile makonda alifanya nae kazi yule mzee alikua na 7b zote kuhudhuria. Ata ivo kwa mtazamo wang mimi uyo bint nahis ndo hakua mstaarab kumkatalia kumpa mkono. Na ata hao wanaohisi kua makonda kakosea asingekwenda wangedai kafurahia msiba wa kabwe ndo mana hakwenda ata kwenye mazko ake. Mi nafikir tunatakuwa tumpongeze mh mskonda kwa kuonyesha uungwana wa hali ya juu na kuhudhuria mcbani kwa aliyekua mtumish wake.. Kwan kaonyesha kua yeye hakua na kinyongo nae bt yaliyotokea ilikua ni ishu za kazi tuuuu.. Big up man makonda...
uwa aende alipokuwa Mgongjwa siyo alipokufa, angeweza kupigwa na watoto wenye hasira
 
Mimi naomba niongee kitu kuhusu mtoto wa Kabwe kukataa kupokea salamu za mkuu Makonda, nadhani huyu dada hakufanya vizuri hata kidogo!!! Hivi Mtoto wako au Kaka yako au Hata baba, akifanya mambo mabaya inapaswa asiambiwe au asiadhibiwe?? Jamani Watanzania tunaenda wapi iwapo kila Siku tunalia haki hazitendeki kila idara sasa huyu Marehememu alitendewa haki au alionewa?? Jamani tunaenda wapi??je ukimuona mtoto wa Jirani yako anatenda mabaya ukamkanya ubaya unageuka kwa mkanyaji ndivyo ilivyo kweli !!!!
it depends
 
Back
Top Bottom