Ni kweli kabisa Mkuu , Watoto wa kike mara nyingi wanafikiri kuwa wanume wote wana tabia kama za baba zao, Wakiolewa ndio huona tofauti.
Na mara nyingi mabinti waliolelewa na Wababa "smart" hupata shida sana katika ndoa zao,maana hutaka kuwalinganisha waume zao na tabia za baba zao
Binti anakumbuka jinsi Mama alivyokuwa "well treated" na baba yake,anaona mbona huyu wangu hafanyi kama baba alivyokuwa anafanya kwa Mama??
Ndio maana unakuta kutwa kucha binti anasema "Aaa yani baba alikuwa anamfanyia Mama hivi na vile"
Ukizingatia Baba kama Kabwe,alikuwa anawalea watoto wake kwa maisha safi,shule unaenda kwa amani,hela ya matumizi,hupati shida uwapo shule au chuo nk
Lazima aumie,asononeke na hasa akiona baba anasemwa hadharani na "mtoto" kama Makonda.Maana Mzee anapokuwa anapiga madili hasemi kuwa hizi ni hela za madili.
Damu nzito kuliko maji,niliwahi kukaa na jamaa baba yake ni mlevi sana,lkn alikuwa hakosi kuwalea watoto wake vizuri,kuna siku tunapita sehemu tukakuta watu wanapiga kelele eneo la Bar,ikabidi tupite kutazama,kufika pale tukakuta baba wa jamaa amelewa chakari,kajikojolea na amelala fofofo
Barmaid anamvuta kumuamsha Mzee wafunge Bar...huku akitoa maneno makali na kumzaba makofi.Damu nzito kuliko maji,Jamaa alitembeza kichapo kwa bar maid na waliokuwa wanamgasi Mzee,akamchukua mzee kwenye Tax hadi home
Japo kiukweli mzee alichokuwa kafanya hakikuwa sahihi,lkn mtoto alipatwa na "damu nzito" akamsaidia.Binti yupo sahihi