Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Mpuuzi tu..sasa kwa kumchunia inasaidia nini?baba yake hakuwa muadilifu,hilo halina ubishi.kote alikopita alikuwa analaumiwa.angekuwa muungwana angemwambia baba yake aache ubadhilifu..mjinga tu.kwanza hata makonda amefanya ubinadamu tu kwenda msibani.
Swadakta mkuu...Makonda kaiwakilisha serikali...tena angeamua angetuma mwakilishi...lakin katambua heshma yake serikalini ndomana akaenda.
 
Hivi Hiyo Binti anatakiwa ku - overcome kilicho tokea , bado yeye mwenyewe na familia WANa maisha marefu Huko mbeleni na hawajui wata kutana na changa Moto zipi na Nani atakuja wasaidia , ni sawa Kama ilivyotokea kwa Makonda , kwa kauli au vitendo vyake ambavyo baada ya hapo anatambua kuwa vitu haviendi Kama alivyosema au alivyo tenda, Tanzania Kama nchi tuna changamoto nyingi za kuzifikiria na kutatua , dhidi ya hizi za kiutu au Watu wawili au kifamilia .
 
Issue ni kwamba Makonda alichofanya sio sahihi. Taratibu za adhabu kisheria zinafahamika. Sio ustaarabu kumtuhumu mfanyakazi hadharani na sio sahihi kumfukuza mfanyakazi hadharani hata bila kumsikiliza. Hata kama alikuwa na makosa sheria zingepaswa kufuatwa. Makonda kujipeleka kwenye msiba wa mtu aliyeshiriki kifo chake ni mzaha. It is a matter of common sense.

C & P
Nimekupa bonge la LIKE mkuu, watu wanajitoa ufahamu sijui kwa nini? Na hapo marehemu kabwe bado ni mtuhumiwa tu wala haijathibitika ndio maana alisimamishwa kazi kupisha uchunguzi vipi ikibainika hakuwa na hatia huyu Makonda bado ataenda kuwapa mkono wa pongezi hao watoto kuwwa baba yao alikuwa msafi?
 
Swadakta mkuu...Makonda kaiwakilisha serikali...tena angeamua angetuma mwakilishi...lakin katambua heshma yake serikalini ndomana akaenda.
Katambua heshima yake tu lakini hakujua kuwa hana heshima mbele ya familia ya Kabwe! na amepata alilo stahili.
 
Tuna kazi kweli nchi hii. Madudu hayatokaa yaishe.

Ufisadi ni ufisadi tu labda kama huyo jamaa alikuwa anasingiziwa. Watu hawapaswi kuacha kufanya kazi zao au kutumbua yeyote kwa sababu yeyote. Lazima tuwekane sawa
 
kwani m
sijaongelea issue ya marehemu alikuwaje...however he was...yule ana familia yake ambayo wote wanamthamini kama mzazi na ndugu yao...however he was

Msibani ni sehemu familia inapata fursa ya kumwomboleza ndugu yao

Sasa limtu linajibeba tu linaenda kama vile pale pia ni shughuli ya serikali...Upuuzi na kutotumia common sense
kwani makonda haruhusiwi kuaga yeye na ulitaka afanyeje kama wewe ukigundua mtu ana fanya wizi umuache au ulitaka iweje embu fafanua
 
Watu wa natakiwa wafanye kazi zao inavyotakiwa.

Kurekebishana kuna gharama nyingi. Tuendelee kuwekana sawa. Madudu aka maufisadi yanayofanyika yana ua wengi kuliko mtu unavyoweza kutegemea
 
kwahio kumbe kumfichua fisadi ni chuki daaah sasa tukiwaacha jee itakuwajee mmmh
Hapana...Lakini just fikiria kibinadamu mzazi wako ndio amefariki alafu anakuja mtu aliyeamua kuonesha chuki za wazi kabisa na mzazi wako...eti anajipendekeza msibani kuwa anajali

Huo ni ujinga na Unafiki

Pia kumbuka watoto wa kabwe pia wana maumivu
 
Issue ni kwamba Makonda alichofanya sio sahihi. Taratibu za adhabu kisheria zinafahamika. Sio ustaarabu kumtuhumu mfanyakazi hadharani na sio sahihi kumfukuza mfanyakazi hadharani hata bila kumsikiliza. Hata kama alikuwa na makosa sheria zingepaswa kufuatwa. Makonda kujipeleka kwenye msiba wa mtu aliyeshiriki kifo chake ni mzaha. It is a matter of common sense.

C & P
Jamani hivi kumsimamisha kazi mtu ndio usiri unahitajika? Ila kuita kazini ndio hauhitajiki? Tujifunze kuwajibika huyo Kabwe majiji yamelia vya kutosha akiwemo Wenje alilia sana na huyu ndugu je walilia sirini au hadharani? Ndugu tusiwe wa nazi wa siasa za kitapeli kwamba akitendwa fulani sio sawa ila akitendewa yule potelea mbali
 
Kibaya ni kumuonea mtu. Kama Makonda kamuonea huyo jamaa yapasa alaumiwe. Lasivyo hii nchi tutaiharibu kama kila tutaendekeza ufisadi au kulinda au kutetea mafisadi. Hata wananchi wanaofisadiwa wana stahili maisha mazuri na kuishi
 
Ninyi kama sasa hivi mnasema mmemiss JK si wa kupuuzwa tu? JK mlimwita dhaifu na majina mengine mabaya lakini kwa unafiki wenu mnamwona ni bora sasa hivi. Mmekosa mwelekeo.
Nikisema Wamama wanalala chini kwa sababu ya Safari zilizokuwa za Kijinga? Haya Makonda Kataja Kabwe na Mimi Nisichelwe Kupata Sifa, Namtaja ambaye pia anajulikana na Bunge limesema aadhibiwe. JPM eee, Mtumbue Chengeeee AKA Joka la Makengezaaaa JPM eee Mbona Muhongo Umemrudishaaa, JPM eee Mtumbue Prof. Anna T. aka Mama Escrow, Naomba na Mimi Nionekane Nimefichua Ufisadi wao Kama Makonda alivyomfuchua Kabwe. Nionekane na Mimi Kidogo Kuwa Nimekupa Taarifa mpya eti. So Funny!
 
kwa wakubwa wataelewa na waliokulia kwa watawala au kuwa watawala:

Hii ni vita ya familia ya makonda na kabwe na sio serikali. hata vizazi vijazo yani watoto,wajukuu na vitukuu huko mbele vitaendeleza.
Sababu tayari mtu (kiini cha ugomvi na suluhisho) wa upande mmoja amefariki. hivyo huo ugomvi ulikuwa umalizwe na wao wawili lakini haiwezekani.na ni vigumu hata ndugu kuumaliza kwani kila ndugu ana lake moyoni juu ya makonda na familia yake.lait marehemu angetoa kauli ya kufuta mifarakano yao basi ndugu ilikuwa rahisi kutii na siyo mwingine atakaeeleweka sasa.
poleni sana hizi familia mbili.bila busara mtamalizana na kuumizana sana.
 
Huyo binti amekosa adabu kabisa. Afuatilie historia ya baba yake ajue. Na kama anahisi Mh Makonda amemuua baba yake amshitaki. Tunawaacha wazazi wetu wanafanya uharifu halafu siku ya siku tunawachukia watu pasina sababu useless
 
Kuna haja ya kujifunza kuhandle changamoto za kiofisi bila kuzihusisha na shughuli zetu za kijamii, inabidi mioyo yetu tuibadilishe na kama mtu amekutumbua ofisini kwa tuhuma ambazo unapata haina maana kwamba basi katika maisha yetu ya kijamii anakuchukia. (ila kwetu ndo inamaanisha hivyo kutokana na mitazamo ya walio wengi kwamba ukikosea au kutuhumiwa alafu ukatumbuliwa tayari hata kusalimiana hakuna)
 
Hakuna mtu ajuaye atakufa vip,lini na atafia wapi,Kabwe siku yake ilishafika na mahali pake pa kufia palikua India full stop.Huyo mtoto wa marehemu na wengineo mnaodhani Makonda ndo amesababisha kifo ni kutokana na imani za kishirikina mlizob nazo
 
Mazoea yana taabu. Watu wanasahau kuwa ufisadi ni mbaya na una ua sio tu mtu mmoja mmoja bali mustakabali wa jamii nzima
 
kuweka maneno hakiba hufanya mtu aamue jambo kwa hekima na busara,kwani maneno yana tabia ya kumuathiri mnenaji pale kutakopotukia jambo litakonasibishwa na maneno yaliyonenwa hata kama tukio halina uhusiano na maneno yaliyonenwa.
 
Back
Top Bottom