Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Huyo binti hana akili kabisa...hata wenzie wanamshangaa siunaona kwenye picha wanavyomtazama? Huyo ni hasara...ametengeneza biff jipya yaani ningekua boss wake kazini akirudi anakula memo
kiburi cha pesa hicho. ila ajue anavuna alichopanda baba yake ... iwe funzo kwake naye asije akapanda ya hivi .. watoto wake nao watavuta hayo hayo
 
Mimi naona marehemu anastahili yote hayo. Kabla ya kumlaumu Makonda nendeni mahospitalini mwone kina mama na watoto wanavyopataa tabu kwa matatizo ambayo yangemalizwa kwa hela ambazo watu kama kabwe waliziiba kifisadi. Huyo kabwe kwa hela alizoiba ni wazi zingeweza kusaidia kuepusha vifo vingi vya wajawazito. Huyo binti nampa pole ila asijenge chuki na Makonda kwa makosa ya baba yake
 
Naichukia ccm kwa sababu ya ufisadi ila naanza kuichukia tena chadema. Kweli leo chadema wanalaumu kabwe kutumbuliwa, wakati walimuimba wakati wote kuanzia bungeni, nusura ampoke Wenje ubunge 2010, leo wanasikitika kutumbuliwa kwake. Dah wamenisikitisha sana.
Hakuna wanaolaumu Kakwe Kuwajibishwa, Ni Unafiki uliokuwa involved kwenye zoezi lenyewe sijui kama Unanielewa. Unaweza Ukamchinja Ng,ombe kwa ajili ya Kitoweo, Lakini Nikijua huyu Ng'ombe ulimfunga nyuma ya gari na mnyororo ukamburuza mtaa mzima, akichunika mpaka akafa, hiyo nyama yake tafadhali Usiniuzie! Ikumbukwe, UFISADI na WIZI wa KURA Zanzibar, UMALAYA, UNAFIKI, KUTAKA KUABUDIWA, KUPIGA WAZEE WAKO, Vyote Ni Dhambi sawa! Sisi Tunaona Ufisadi tu.
 
hili gazeti lina taarifa za umbea sana, sasa hii nayo ni habari ya kuweka front page ili ipeleke ujumbe gani kwa jamii?
Kama la UHURU eti eee!!!
Binti wa aliyekuwa mkurugenzi wa jijj la dar es salaam marehemu Kabwe amchunia RC Makonda.

Hata mim siyo kumchunia bali hata kwetu asingekanyaga. Naweza sema hata kama Kabwe alikuwa anaumwa but kifo chake kimesababishwa/kimeharakishwa na changamoto za kibinadamu alizozipata baada ya Makonda kusababisha atumbuliwe.

RIP KABWE.

Ni ujinga tu wa huyu makonda

Anajua fika kwenda kwake pale anawaongezea wafiwa maumivu

Kiherehere cha nini kujipeleka...si angeenda mkuu wa wilaya

Huu ni ukosefu wa Ubinadamu

Lile lilikuwa suala la kifamilia....Alitakiwa tu kutumia common sense
 
Mimi naona marehemu anastahili yote hayo. Kabla ya kumlaumu Makonda nendeni mahospitalini mwone kina mama na watoto wanavyopataa tabu kwa matatizo ambayo yangemalizwa kwa hela ambazo watu kama kabwe waliziiba kifisadi. Huyo kabwe kwa hela alizoiba ni wazi zingeweza kusaidia kuepusha vifo vingi vya wajawazito. Huyo binti nampa pole ila asijenge chuki na Makonda kwa makosa ya baba yake
Nikisema Wamama wanalala chini kwa sababu ya Safari zilizokuwa za Kijinga? Haya Makonda Kataja Kabwe na Mimi Nisichelwe Kupata Sifa, Namtaja ambaye pia anajulikana na Bunge limesema aadhibiwe. JPM eee, Mtumbue Chengeeee AKA Joka la Makengezaaaa JPM eee Mbona Muhongo Umemrudishaaa, JPM eee Mtumbue Prof. Anna T. aka Mama Escrow, Naomba na Mimi Nionekane Nimefichua Ufisadi wao Kama Makonda alivyomfuchua Kabwe. Nionekane na Mimi Kidogo Kuwa Nimekupa Taarifa mpya eti. So Funny!
 
Mchawi hakosi kuhudhuria kujua hali ya mchawiwa wake iwe mgonjwa au amekufa.
 
Kwa kumchunia Makonda ndio baba yake atafufuka?
Na angempa mkono ndiyo angefufuka , nafikiri dada kuna kitu kinamuumiza na nashukuru kwa kuonyesha kilichopo moyoni bila kificho , wengi wetu tumejawa na unafiki unampa mkono then akigeu kamnaanza kumnena
 
sijaongelea issue ya marehemu alikuwaje...however he was...yule ana familia yake ambayo wote wanamthamini kama mzazi na ndugu yao...however he was

Msibani ni sehemu familia inapata fursa ya kumwomboleza ndugu yao

Sasa limtu linajibeba tu linaenda kama vile pale pia ni shughuli ya serikali...Upuuzi na kutotumia common sense
wewe nimekukubali
 
Kwa kumchunia Makonda ndio baba yake atafufuka?
ukifikiria haraka kwa kutumia mata..ko ndo utacomment haraka na kipuuzi hivyo.hizi chipsi mnazokula wanaume wa dar muwe makini sana.mtaolewa wooote muda si mrefu.na wewe ni mchumba wangu kuanzia leo.sweet bujibuji
 
ukifikiria haraka kwa kutumia mata..ko ndo utacomment haraka na kipuuzi hivyo.hizi chipsi mnazokula wanaume wa dar muwe makini sana.mtaolewa wooote muda si mrefu.na wewe ni mchumba wangu kuanzia leo.sweet bujibuji
Usishangae. Kumbuka Bujibuji ni Mnyamanyafu.
 
Kwa kumchunia Makonda ndio baba yake atafufuka?

Hayo ni sawa na maeneo ya mtaani. Issue ni kwamba Makonda alichofanya sio sahihi. Taratibu za adhabu kisheria zinafahamika. Sio ustaarabu kumtuhumu mfanyakazi hadharani na sio sahihi kumfukuza mfanyakazi hadharani hata bila kumsikiliza. Hata kama alikuwa na makosa sheria zingepaswa kufuatwa. Makonda kujipeleka kwenye msiba wa mtu aliyeshiriki kifo chake ni mzaha. It is a matter of common sense.
 
Yaani wewe mpaka sasa hujajua ni ujumbe gani uliopelekwa kwa jamii kwa hili sakata la makonda na marehemu Kabwe?! utakuwa mvivu wa kufikiri.. tafsri moja ndogo tu nikupe, hakuna aijuae kesho, Makonda angejua hili asingefanya alilofanya.
Kwani makonda kafanyaje?
 
Kwani makonda kafanyaje?

Issue ni kwamba Makonda alichofanya sio sahihi. Taratibu za adhabu kisheria zinafahamika. Sio ustaarabu kumtuhumu mfanyakazi hadharani na sio sahihi kumfukuza mfanyakazi hadharani hata bila kumsikiliza. Hata kama alikuwa na makosa sheria zingepaswa kufuatwa. Makonda kujipeleka kwenye msiba wa mtu aliyeshiriki kifo chake ni mzaha. It is a matter of common sense.

C & P
 
Sasa huko kumchunia kutamsaidia nini? Baba yao atakuwa sio mwizi tena? Kwa hiyo ilitakiwa Makonda asimtaje Kuwa ni mbadhirifu? Cheo cha ukuu wa mkoa sio cha Makonda peke yake, muda wowote anaweza kutolewa na kuwekwa mtu mwingine, na ni jukumu la kila anaeshika hiyo nafasi, pamoja na zote zingine ambazo ni za kiutawala kutimiza majukumu yake kama inavyostahili na kama anavyotarajiwa.KKuingiza emotions kwenye hayo majukumu,ni kutokana na kutokuwa na ufahamu, ambalo si kosa vilevile. Pitia tena post yangu ya mwanzo.

hivi unajua kuwa msibani ni sehemu ya emotions?

Mimi sijapinga kuwa marehemu alikuwa Mwizi...alikuwa ni mwizi sana...na sisi CHADEMA tumesema hilo mara nyingi

Lakini kuna mipaka ya kutambua ...kwa hekima ya kawaida tu ...kutokuumiza ndugu wa marehemu...msibani kunakuwa na emotions kama hizo

Nimekuuliza....Kuna ubaya upi kama makonda angewakilishwa na mkuu wa wilaya...ili kuepuka kuwaumiza ndugu wa marehemu bila sababu

Kabwe alikuwa mwizi...lakini
[/QUOTE]








Uso wa nyoka

Ni kweli msiba ni sehemu ya emotions lakini kumconect Makonda na kifo cha huyo marehemu ni kukosa ukomavu kwani Makonda sie aliempa ugonjwa wa Ini,tezi dume,mapafu au hata kama ingekuwa pressure.
Makonda asingeenda, napo angesemwa tu kuwa alijisikia guilt kwa vile yeye ndie chanzo,wakati si kweli. Tunashauriwa Kufanya Mazoezi mara kwa mara na Kufanyiwa medical check up

SABABU ZA KIFO CHA KABWE HIZI HAPA


Wakati mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe ukitarajiwa kuzikwa Jumatano ijayo kijijini wake Mamba, Mpinji wilayani Same, chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni saratani ya tezi dume na kuharibika kwa ini.


Kabwe (pichani) alifariki dunia juzi alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Mauti hayo yamemkuta ikiwa ni siku 38 baada ya kusimamishwa kazi hadharani na Rais John Magufuli kwa tuhuma za kuingia mikataba iliyosababisha hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.


Mtoto wa marehemu, Geofrey Kabwe, alisema baba yake alianza kuugua maradhi ya tumbo Julai mwaka jana.


Alisema Ilipofika Desemba, alizidiwa na familia iliamua kumpeleka India kwa matibabu zaidi.


“Alipofika India waligundua kuwa alipata hitilafu ndogo kwenye ini, hivyo akafanyiwa upasuaji, madaktari India walisema chanzo cha tatizo hilo ni dawa alizokuwa akitumia,” alisema Geofrey.


Alisema mwishoni mwa Januari, mkurugenzi huyo alirejea nchini akiwa na afya njema na alianza kwenda kazini Februari huku akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Apollo nchini India.


Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda, hali yake kiafya ilianza kuzorota na ilifikia hatua familia ilitakiwa kukutana ili kushauriana kuhusu hali hiyo.


“Wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu nikiwa Arusha nikaelezwa kwamba hali yake kiafya siyo nzuri, tulimwona daktari wake na akabainika kuwa na Pneumonia (homa ya mapafu), akapewa dawa na sindano,” alisema Geofrey na kuongeza:


“Baadaye tulimpeleka TMJ kwa ajili ya kipimo cha CTScan, jana mchana majibu yalitoka yakionyesha kuwa ini lilikuwa limeharibika na tayari mwili ulikuwa umeanza kuvimba. Ilipofika saa mbili usiku hali ilibadilika akawa anakoroma na saa tatu usiku akafariki dunia,” alisema Geofrey.


Taarifa zilizopatika jana zimeeleza kuwa Kabwe amekuwa nje ya ofisi yake tangu alipoanza matibabu na siku ya kwanza kurejea kazini ilikuwa Aprili 19 ambako alikutana na rungu la Rais John Magufuli.


Msemaji wa familia, Dk Ez Machuve alisema mipango ya mazishi inaendelea: “Atasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwake Jumanne jioni baada ya kuagwa hapa nyumbani kwake. Mazishi tunatarajia kufanya kijijini Mamba Mpinji Jumatano.”


Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema katika kipindi chake cha kufanya kazi, hakubahatika kushiriki kazi yoyote na Kabwe kutokana na hali yake kiafya.


“Sikubahatika kufanya naye kazi, baada ya Rais kufanya uamuzi mgumu, aliondoka hivyo sikuwahi kushiriki naye,” alisema Mwita.


Kilichomwondoa kazini

Makosa yaliyosababisha Kabwe kusimamishwa kazi ni madai ya kusaini mkataba kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2004 kutoza magari yanayotoka kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) Sh4,000 huku akidaiwa kusaini mkataba mwingine wa Sh8,000 chini ya sheria ndogo ya mwaka 2009.


Pia, madai ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa UBT hasa kwenye utaratibu wa kutoa magari na kukodisha vyumba vya kupangisha kinyume na taratibu na kuongeza muda wa mzabuni iliyeingia mkataba na jiji wa maegesho ya magari kinyume na taratibu.
 
Back
Top Bottom