Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

hata ungelikuwa ndo muhusika kwa nachokimaanisha hiyo taarifa inastahili kukaa on front page? mbona kuna issues tena seriously za kitaifa na kimataifa? ok huyo binti kakataa mkono babake karudi? muandishi analenga nini juu ya taarifa hii katika jamii? think critically before u reply, or are you just learning how to quote?

Kwaiyo ni kosa kisheria kuweka iyo picture front page,sheria namba ngapi ya mwaka gani, halafu elewa kuwa magazeti yapo kibiashara,habari ambayo inauza ndo wanaweka kwenye front page,au unadhani hayo magazeti wanapewa rudhuku serikalini mkuu, kingine mi naomba kujua,iyo picha ni halisi au yakutengeneza
 
Kwa hiyo huyo binti anatuma ujumbe kwamba Makonda kwa namna fulani amechangia kifo cha baba yake? Au lugha nyingine kaonewa?
Pili nampongeza Makonda kwa kuonyesha uungwana.Na huyo binti nimkumbushe tu kwamba M/Mungu akipanga lake HALIPANGULI.Akubali tu Muumba ameshaamua.
 
TE="Freeland, post: 16298335, member: 67846"]so ...ulitaka makond apewe mkono ili iweje? who is he hadi iwe lazima apewe mkono? hasa katika shughuli ya mazishi..let say ya mzazi wangu[/QUOTE]
Sasa huko kumchunia kutamsaidia nini? Baba yao atakuwa sio mwizi tena? Kwa hiyo ilitakiwa Makonda asimtaje Kuwa ni mbadhirifu? Cheo cha ukuu wa mkoa sio cha Makonda peke yake, muda wowote anaweza kutolewa na kuwekwa mtu mwingine, na ni jukumu la kila anaeshika hiyo nafasi, pamoja na zote zingine ambazo ni za kiutawala kutimiza majukumu yake kama inavyostahili na kama anavyotarajiwa.KKuingiza emotions kwenye hayo majukumu,ni kutokana na kutokuwa na ufahamu, ambalo si kosa vilevile. Pitia tena post yangu ya mwanzo.
 
NAOANA WENGI MNACHUKULIA KUFIWA JAMBO JEPESI SANA HASA UNAPOPETEZA WALIO KTK FAMILIA YAKO YAONENI KWA WENZENU TU.
 
Hawa TANZANIA DAIMA wangekausha tu!

Sio kila jambo unapaswa kuripoti, tena front page!
 
Huyu mdada ana akili sana na kaamua kuweka unafiki pembeni. Ni vizuri ssns watz tujifunze kuwa wakweli kwa nafsi zetu. Maigizo hayana maana. Kitendo cha Makonda kwenda pale kimewaongezea machungu wafiwa badala ya kuwafariji.
Nilitegemea Makonda angekuwa na busara kutokwenda pale kwa sababu ya mazingira yaliyokuwepo tangu mwanzo. Wanafamilia hawakumtaka pale. Nadhan walishindwa kumfanyia fujo kwa sababu analindwa ma maaskari. Na nadhan Makobda alijua hawawezi kumfanya lolote kwa sababu ana ulinzi. Ni kiburi tu hakuna zaidi. Ingekuwa sio cheo chake asingedhubutu kukanyaga pale.
 
Jaman mambo mengine sio ya kupost humu, kwanza unapoandika vile ni dhahiri kuwa umefurahishwa na kitendo cha huyo binti, pia mi sioni kosa la makonda kusema makosa na ubadhilifu wa kabwe uliopelekea mpaka kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pia ieleweke kuwa kazi ya kutumikia umma huhitaji mhusika awe na uadilifu kwa umma.
Kabwe amefanya kazi kama mkurugenzi kwa mkoa wa mwanza, mbeya na dar lakini udhaifu mkubwa ulionekana ukiambatana na ubadhilifu, kusimamishwa kazi kusiwe sababu ya kumuona kuwa alikuwa mwema mno kiasi cha kumuona makonda kama kihelehele kwani naamini aliyafanya yote hayo kwa faida ya wanadaresalaam wote hata watanzania kwa ujumla.
Kila kifo kina sababu zake, kama inasemekana tayari alikuwa mgonjwa, je haikupaswa kumsimamisha kazi kisa mgonjwa kwa kuhofia atafariki? Tuacheni unafiki wa kuwa vigeugeu wasioeleweka, baadhi mlilalamika kuwa marehemu alikuwa tatzo leo tena lawama kwa makonda?
R.I.P KABWE

Mkuu Saguda47 mimi sidhani issue ni makonda kumchongea kabwe kwa JPM (ingawa mimi bado mpaka leo siafikiani na jinsi ule utumbuaji ulivyofanywa).

Issue hapa ni kwamba makonda alitumia busara gani kuja kwenye msiba wa mtu ambaye alishiriki kumtumbua? Hakujua kabisa kwamba familia katika hali yao ya majonzi huo uchungu wa kumpoteza mpendwa wao wangeuhamishia kwake? Yani kabisa hakufahamu kwamba hapa itakuwepo taswira ya unafiki? Alishindwa kumtuma basi hata DC Hapi kumwakilisha? Mbona hii ni common sense ambayo haya mtoto wa darasa la 5 anayo jamani!
 
Binti wa aliyekuwa mkurugenzi wa jijj la dar es salaam marehemu Kabwe amchunia RC Makonda.

Hata mim siyo kumchunia bali hata kwetu asingekanyaga. Naweza sema hata kama Kabwe alikuwa anaumwa but kifo chake kimesababishwa/kimeharakishwa na changamoto za kibinadamu alizozipata baada ya Makonda kusababisha atumbuliwe.

RIP KABWE.
mshahara wa dhambi ni mauti .... MAMBO YOOOOOOOOOOTE YATAPITA LAKINI NENO LA MUNGU HALITAPITA.
 
Huyu mdada ana akili sana na kaamua kuweka unafiki pembeni. Ni vizuri ssns watz tujifunze kuwa wakweli kwa nafsi zetu. Maigizo hayana maana. Kitendo cha Makonda kwenda pale kimewaongezea machungu wafiwa badala ya kuwafariji.
Nilitegemea Makonda angekuwa na busara kutokwenda pale kwa sababu ya mazingira yaliyokuwepo tangu mwanzo. Wanafamilia hawakumtaka pale. Nadhan walishindwa kumfanyia fujo kwa sababu analindwa ma maaskari. Na nadhan Makobda alijua hawawezi kumfanya lolote kwa sababu ana ulinzi. Ni kiburi tu hakuna zaidi. Ingekuwa sio cheo chake asingedhubutu kukanyaga pale.
TUKUBALIANE KATIKA HILI ... Tunaweza kutofautiana kwa mambo mengi lakini kwenye msiba huwa tunaungana tu.
 
Kabwe kaacha mtoto mmoja tu ambaye ni huyo aliyechuna?

Na wengine walimchunia? Vipi mjane naye alichuna?

Good for her!!!
 
Ila ingekuwa vizuri asingeenda,mtoto wa marehemu angeweza hata kumshambulia na ingeonekana ni ghadhabu tu na sio kosa,sasa ni bora akuparuze na kucha utapona ingekuwaje kama angmetia kidole kwenye jicho na likatumbuka!!
Duuuh! Mkuu mawazo yako yameenda mbali sana, kidole mpaka jicho kutumbuka hahaha nimejaribu kuimagine.
 
Haya mambo ya Suarez na Patrice Evra yapo mpaka kwenye misiba...Tulizoea kuona kwenye mpira ligi z Ulaya
Ndio maana mambo ya kuajiliwa ni kama "Utumwa",Mzee Kabwe "alitumbuliwa" na Makonda mtoto wake kabisa wa kumzaa
Maana mwaka 1982 wakati Mzee Kabwe anaanza Chuo Kikuu akisomea Sheria,Bwana Mdogo Makonda alikuwa hajazaliwa kabisa,nafikiri hii ya Kabwe ni moja kati ya kumbukumbu "mbaya" ya Makonda ktk utumishi wake na maisha yake ya kiroho.Makonda ni "kijana" wa yule Pastor Ndegi wa Kawe.Kwa ulimwengu wa Roho,hii kitu ina nafasi yake,kama tu "dhamira ya kiroho" ya Makonda bado i hai.
Kiroho Mkonda alikuwa anafanya upatanisho, hii inawezekana tu kama dhamira yako ni nyeupe na hamna element za visasi kabisa.
 
Kwa bond iliyopo baina ya mtoto wa kike na baba yake na jinsi wanawake walivyo emotional siwezi kumlaumu huyo mtoto wa kabwe alikua sahihi kabisa
 
TE="Freeland, post: 16298335, member: 67846"]so ...ulitaka makond apewe mkono ili iweje? who is he hadi iwe lazima apewe mkono? hasa katika shughuli ya mazishi..let say ya mzazi wangu
Sasa huko kumchunia kutamsaidia nini? Baba yao atakuwa sio mwizi tena? Kwa hiyo ilitakiwa Makonda asimtaje Kuwa ni mbadhirifu? Cheo cha ukuu wa mkoa sio cha Makonda peke yake, muda wowote anaweza kutolewa na kuwekwa mtu mwingine, na ni jukumu la kila anaeshika hiyo nafasi, pamoja na zote zingine ambazo ni za kiutawala kutimiza majukumu yake kama inavyostahili na kama anavyotarajiwa.KKuingiza emotions kwenye hayo majukumu,ni kutokana na kutokuwa na ufahamu, ambalo si kosa vilevile. Pitia tena post yangu ya mwanzo.[/QUOTE]

hivi unajua kuwa msibani ni sehemu ya emotions?

Mimi sijapinga kuwa marehemu alikuwa Mwizi...alikuwa ni mwizi sana...na sisi CHADEMA tumesema hilo mara nyingi

Lakini kuna mipaka ya kutambua ...kwa hekima ya kawaida tu ...kutokuumiza ndugu wa marehemu...msibani kunakuwa na emotions kama hizo

Nimekuuliza....Kuna ubaya upi kama makonda angewakilishwa na mkuu wa wilaya...ili kuepuka kuwaumiza ndugu wa marehemu bila sababu

Kabwe alikuwa mwizi...lakini that issue would have been handled properly kwa kufuata taratibu za ofisi...na kuheshimu walau utu wake....that's why hata wafungwa wanapewa chakula na sehemu za kulala
 
watoto wa magorofani muda mwingine nao wanakuwa waswahili.....uo ni uswahili uliotukuka hakuwa na sababu ya kufanya icho kituko hata ndugu zake apo wanamcheki kwa pembeni,kaendeleza kucheza ule mziki wa kisiasa uliokuwa ushaanza kuvuma mtaani na hapo ataibuka msemaji wa familia na kumuombea excuse kwa niaba ya familia.lol
 
Mkuu Saguda47 mimi sidhani issue ni makonda kumchongea kabwe kwa JPM (ingawa mimi bado mpaka leo siafikiani na jinsi ule utumbuaji ulivyofanywa).

Issue hapa ni kwamba makonda alitumia busara gani kuja kwenye msiba wa mtu ambaye alishiriki kumtumbua? Hakujua kabisa kwamba familia katika hali yao ya majonzi huo uchungu wa kumpoteza mpendwa wao wangeuhamishia kwake? Yani kabisa hakufahamu kwamba hapa itakuwepo taswira ya unafiki? Alishindwa kumtuma basi hata DC Hapi kumwakilisha? Mbona hii ni common sense ambayo haya mtoto wa darasa la 5 anayo jamani!
Ok, mkuu uko sahihi lakini hoja yangu ni kwa watu wasio wanafamilia wa marehemu kabwe, ambao wanajivalisha uanafamilia na kutoa shutuma nzito kwa makonda kwa kumsemea marehemu kwa mh. Rais, hii inaleta taswira ya unafiki kwa baadhi ya watu ambao miezi michache iliyopita kilio chao kilikuwa juu ya marehemu kabwe, kasimamishwa kazi na bahati mbaya mauti yamemkuta haohao wanaelekeza sababu za kifo moja kwa moja kwa makonda.
 
Hachana nao kwani wao ni madaktari?
 
Back
Top Bottom