Makapuku Forum

Malengo ya Mtibwa Sugar msimu ujao ni kushika nafasi ya tatu au nafasi ya pili, ikiwezekana hata kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ili kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kimataifa.

Thobias Kifaru, Afisa Habari Mtibwa Sugar.
Screenshot_20210923-102521_Instagram.jpg
 
KAZE KATUA DAR USIKU MZITO

Cedric Kaze tayari yupo nchini, ametua usiku wa kuamkia leo na huenda wakati wowote akatambulishwa kama Kocha Msaidizi.

Inaelezwa Kaze ataanza majukumu yake mara moja na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi Septemba 25.
Screenshot_20210923-102927_Instagram.jpg
 
OMOG ATUA MTIBWA
.
Hatimaye kocha wa zamani wa Simba na Azam FC, Joseph Omog ametua nchini jana Jumatano kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na Mtibwa Sugar.
.
Kwa mujibu wa ofisa habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru, Omog alitua nchini saa tisa alasiri na mara moja akapokewa na mwakilishi wao
Screenshot_20210923-103235_Instagram.jpg
 
WANASOKA WANAOPIGA PESA NDEFU MSIMU HUU:
.
Cristiano Ronaldo: $125m
Leo Messi: $110m
Neymar: $95m
Kylian Mbappé: $43m
Mo Salah: $41m
Robert Lewandowski: $35m
Andrés Iniesta: $35m
Paul Pogba: $34m
Gareth Bale: $32m
Eden Hazard: $29m
.
Forbes
Screenshot_20210923-103341_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

PEP GUARDIOLA, NJIA NYINGINE YA USHINDI - PART ONE

Ilikuwa ni dakika nane ya mchezo ni usiku wa Mei 27, 2009! Ni fainali ya UEFA kati ya Barcelona na Manchester United, moja kati ya fainali bora kwenye nyasi kijani za Olympico

Waitaliano wenye siasa za mlengo mkali wa kushoto walisema wazi kabisa kuwa baada ya kifo cha Benito Musollini mwenye sauti ya mamlaka na mwenye uwezo wa kumuogopesha hata nzi aliepo Roma Italia, basi ilifata usiku huo

Ulikuwa usiku wa kumtazama Kijana mdogo kutoka Santpedor huko Kaskazini Mashariki mwa Hispania anaitwa Pep Guardiola dhidi ya Mskochi Sir Alex Ferguson! Naam ni usiku ambao Pep alikuja kukileta kitu kipya kwenye uso wa dunia

Ilikuwa dakika ya nane ya mchezo! Wakati Barcelona bado wanasaka form yao, kila Mchezaji yupo eneo sahihi lakini bado hawapo kwenye ubora! Kifupi Manchester United walikuwa wametawala kila eneo

Tayari Cristiano Ronaldo ameuwasha sana! Akasimama sasa Pep Guardiola kuja kuionesha dunia nini alikuwa anawaza! Alimtazama Tito Vilanova na kusema "Ni muda sasa wa kuitengeneza dunia yangu ya mpira"

Aliitazama kwanza pattern ya Giggs, Carrick na Anderson wa United kwa sauti kali ya mamlaka kwenye dimba lililojaa Mashabiki akaanza kutoa maelekezo yake rasmi

Akamwambia Lionel Messi aingie katikati mbele kwa mabeki akae kama False 9 kisha Etoo akaenda pembeni! Kila mtu akawa amepigwa na butwaa, anafanya nini Pep Guardiola? Lakini Vilanova alielewa, Zubizareta ambae alikuwa TD wa Barca pia alielewa

Kwenye kitabu chake cha ANOTHER WAY OF WINNING aliita hii alichofanya kuwa "The Camp Nou revolution" kifupi dunia haikuwa tayari kushuhudia, Messi namba tisa? Etoo anatokea pembeni?

Hapo sasa mbungi ikaanza! Messi anamsaka Iniesta, kisha Iniesta anampa pass Xavi, ambae Xavi anampa tena Messi! Tayari ndani ya sekunde Manchester United ishapoteana

ITAENDELEA..... Simulizi hii ni kwa msaada wa kitabu cha maisha ya Guardiola
Screenshot_20210923-105801_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

TAKWIMU ZA MASHABIKI UWANJANI VPL 2020/21

Nimeziona takwimu za Mashabiki waliojitokeza uwanjani kwa msimu uliopita, ni pongezi kubwa kwa bodi ya ligi wamepiga hatua haswa

Nini kimenivutia zaidi? Binafsi ni Dodoma Jiji na Pamba ya Mwanza, kwa wale watu wa MARKETING mmepata simple survey kuwa mnaweza pia kuwekeza kwenye hao

Kuna suala la Simba na Yanga, nani ana Mashabiki zaidi?

Nadhani hili limeibuliwa kupitia hii data lakini hii haihusiani na IDADI YA MASHABIKI bali WAHUDHURIAJI wa mechi uwanjani! Wapo wangapi wanaenda uwanjani kumzomea mpinzani?

Wangapi wanaenda tu uwanjani kwa mapenzi ya mpira? Basi yoyote aendaye basi anahesabika kuwa amehudhuria bila kujali lengo lake! Derby inaweza kuwa ya Simba ila Yanga wakajaa au Derby ya Yanga ila Simba wakajaa

Ngoja niwape mfano mwepesi kidogo kuhusu idadi ya Mahudhurio viwanja vya nyumbani pale EPL (ENGLAND) kwa msimu wa 2019/20 kabla ya COVID 19 kuingia msimu uliofata

Manchester United (57K), Arsenal (47K), West Ham (44K), Tottenham (43) na Liverpool (41) hii ni orodha ya TOP 5 pale EPL! Umestaajabu baadhi ya miamba kutowepo? Umeshangaa kuna timu zimeingia ijapo hazina mafanikio makubwa?

Well Watalaam wa Uchumi wanasema kujaza Mashabiki uwanjani kuna vitu vingi ikiwemo pia COMMODITY DEMAND! Mfano Simba kacheza game nyingi sana nyumbani, imeonekana sana, ile kiu ya Mashabiki inapungua tofauti na wengine

Hapo kwenye Demand pia! Mfano Yanga walicheza Arusha na uwanja mwingine wa mkoani siukumbuki wakitumia kama uwanja wa nyumbani, huko mikoani DEMAND ni kubwa kuziona hizi timu, ni rahisi kuipata namba kubwa kama hiyo

Kuna kitu kingine pia ambacho kinaingia kwenye namba ya SIMBA vs YANGA! nayo ni LIVE SPECTATORS vs ONLINE (ELECTRONIC VIEWERS) hapa kuna kitu kikubwa sana, Kwa ruhsa yenu nitatumia mfano wa Real na Barca

Itaendelea....
Screenshot_20210923-110203_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

DIDIER GOMES NA SIMBA, KIPI NI KITUO KINACHOFUATA?

Pep Guardiola baada ya kubeba ubingwa wa UEFA 2009 mbele ya Manchester United alijifungia chumbani akawauliza maswali matatu Wasaidizi wake akiwemo Marehemu Tito Vilanova

Swali la kwanza! Mafanikio haya yatadumu kwa muda gani? Swali la pili! Tutaweza kutengeneza timu nyingine ya ushindi? Swali la tatu! Naweza kuwa na timu ya kutwaa tena UEFA? na mwisho! Tutaweza kumudu kwenye kiwango hiki?

Pep aliwahoji wenzie na alisema wazi kuwa ikitokea amepambana na amefeli na haoni njia mbadala basi ataaga na kuondoka Barcelona! Bila shaka mnakumbuka Pep baada ya miaka minne aliondoka Catalunya

Well nimeitazama Simba, nimeona kabisa Didier Gomes anajiuliza na kuwauliza wenzie maswali yale yale manne ambayo Pep aliwauliza wenzie pale Stade de Olimpico, Roma nchini Italia, Mei 27, 2009

Nimegundua kupitia mechi na TP MAZEMBE, Mwalimu analijibu swali la pili kwa namna gani ataendelea kuwa na kikosi cha ushindani! Kwanza alianza na Rally Bwalya akicheza juu ya Thadeo Lwanga na Saido Kanoute

Mwalimu alimtaka Rally awe huru na mpira acheze free role! Lakini baadae kwenye press alisema wazi kuwa kuna vitu Bwalya hakuvitimiza kwa ufasaha ila akasema hakuanza vibaya sana

Well wakiwa na Clatous Chama hii Simba ilikuwa inacheza mpira wa pass mpaka wafike golini kwa mpinzani! Bahati mbaya sasa Chama hayupo na ni wazi Mwalimu anaitaka Simba icheze soka la haraka kufika kwa mpinzani

Alipowaanzisha Chris Mugalu, Dennis Kibu na Bernard Morrison ni wazi anataka timu itembee, waondoke kwenye pass nyingi na kufika langoni mapema ndio maana hata Mugalu alikuwa anaenda pembeni na chini kuomba mipira

Mwalimu anataka kuyalinda mafanikio yake na tayari anajua watu alonao! Anajua Duncan Nyoni ni myumbufu na Peter Banda ni mnyumbufu pasi na kusahau Ousmane Sakho! Wote wanatembea kwenye chaki na timu lazima ikimbie

Naona Ousmane Sakho ataenda kuwa Mtu muhimu kwenye hii timu, naona Simba itaondoka kwenye pass nyingi na kuelekea mpira wa kasi na kufika langoni kwa haraka! Ndio njia ya kulinda mafanikio

Benchi linajua halina Chama tena, hivyo wameamua kuuvua mfumo ule na kuanza mfumo mpya

Screenshot_20210923-110433_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom