Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,870
Farhan Jr
MTIBWA SUGAR, binafsi niseme baada ya miaka mingi ya kuibua ndoto, kufurahia vipaji, kuleta neema kwa familia zisizo na neema, kufuta machozi mkoa wenye vipaji vingi na kuwa mwangaza kwenye giza basi safari hiyo inaelekea kufikia tamati, ijapo bado sitaki kuamini kama tunashuka bado.
Kwetu sisi MOROGORO hii ni zaidi ya klabu, zaidi ya maisha ambapo watoto kutoka Bonde la Mto Kilombero walipata nafasi ya kuamini, Vijana kutoka safu za Milima ya Uluguru na maporomoko ya Udzungwa walipata sababu ya kuamini, kutoka nyika za Gairo mpaka Bonde la mpunga Mlimba na Mizimu ya Kolelo ilibariki mpaka Milima ya Ndororo huko Ulanga.
Muda unakimbia, ndoto zinafifia, nuru inapotea, historia inaenda kufutika? Nyumbani kwa soka la vijana, Mabingwa wa kihistoria wanaenda kupita njia ya Tukuyu Stars? Cosmo na Pamba? Wapi Reli ya Morogoro na Nyota Ndogo, Moro United za Morogoro? Soka la Mkoa wa Morogoro linaenda kuanguka, sifa inaenda kupoteza na nuru kwenye kiza imezima.
UNITED WE STAND, tutasimama wote mpaka mwisho kuimba wimbo wa ushindi, hakuna atakayekimbia kwakuwa hii ni timu yetu, utamaduni wetu na kielelezo chetu cha ubora, tutapigana mpaka nwisho wa pumzi yetu, ikitokea tumeondoka basi tunawaomba sana enzini yale mema yetu na ndoto za Vijana ziendelee, ikitokea tumeondoka naomba niseme its not a Goodbye, its a see you soon

Klabu ya Yanga, imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Lazarus Kambole. Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba. Yanga ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.